Mi binafsi sijasikia chama alichosema ila kama kweli aliamua kumsifia Manara hadharani inaonesha ni jinsi gani moyo wake haupo sawa na uongozi.
Hii ni dalili mbaya sana na ninaanza kuhisi huenda ni mmoja wa wachezaji aliyetumika na Manara kuihujumu Simba.
Mambo haya yanaanza kidogo kidogo lakini master planner wa hii inaonekana amejipanga kuibomoa Simba kweli.
Bahati mbaya naona haitakuwa kazi ngumu kutokana na Mo mwenyewe kukosa hekma na uvumilivu.
Hapa naona Bakhresa ama GSM wanaanza kufanikiwa michezo yao.Mo ataondoka sio muda mrefu.
Tunaanza na kupoteza ngao ya hisani.Yajayo yanatia shaka mno.Chama hawezi kuwa sawa tena baada ya ujinga aliofanya leo.Naanza kuona mgomo baridi kwa wachezaji wanaomuunga mkono Chama ambaye anataka kujipambanua kama timu Haji.
Simba inavunjika kwa ubinafsi mkubwa na tamaa za Manara,kukosa hekma kwa mwekezaji wa Simba,na fitna zilizoenda shule zinazoandaliwa na washindani wa Mohammed enterprises. Kumbe pesa sio kila kitu