Mobhare Matinyi ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari–MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali

Mobhare Matinyi ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari–MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali

Huyu jamaa hata hajawahi kusikika popote duuuh hii noma sasa si atakua ana-mute tu mda wote maana sio mpigadomo km Ally Kamwe Mo Ally na wengine ambao ni 'Wasemaji' huwezi kua msemaji alafu haujui kupigadomo
Huyu si aliteuliwa juzi juzi kuwa DC ?
 
Mbona mnakariri sana?! Na serikali waliacha hiyo nafasi wazi kwa makusudi wakijua wananchi wajinga watashupaza shingo kumbetia huyo muhuni wa london na sinza. Kumbe hamjui ndo mlikuwa mnamuharibia


Ni makosa kutabiri nyadhifa za serikalini na hata kama unajua kaa kimya! Serikali hawapendi target zao ziende sawa na mtabiri. Hata kama ilikuwa sawa watafanya mabadiliko tu! Huyo Kikeke apewe tu mkataba TBC au AZAM aanze kazi aache uzwazwa atakuja kufulia achekwe. Maana wabongo hawachelewi
Kuna kukariri, kutabiri, kukisia, kudhania, kubashiri na mengineyo mengi, na ni kawaida ya binadamu sometimes inaweza kuwa sawa nyingine isiwe sawa

Anything can happen anytime
 
Kuna kukariri, kutabiri , kukisia, kudhania , kubashiri na mengineyo meeengi, na ni kawaida ya binadamu sometimes inaweza kuwa sawa nyingine isiwe sawa

Anything can happen anytime
Yote hayo mmeshiriki mpaka kumfanya huyo bwana akose kazi, na kuna wapuuzi watamnyima January na Majaliwa urais kwa kukazana na utabiri wao wa hovyo!
 
Kwa hiyo yule SK wa Diaspora ndio basi tena?, Dah nikatagemea Dada Nyota wa Jumba jeupe sababu walitokea dojo moja, atampigia pande kwa Bi Mkubwa, anyway kupanga ni kuchagua, na kuteua ni kuteua.
Inawezekana labda alishateuliwa ila kutokana na wapiga kelele kuwa wengi kabla ya kutangazwa ikabidi mamlaka ya uteuzi ipige chini jina lake. Au labda yeye mwenyewe SK alitaarifiwa kuhusu uteuzi akaanza kupata wenge na habari kuanza kuvuja.
 
Inawezekana labda alishateuliwa ila kutokana na wapiga kelele kuwa wengi kabla ya kutangazwa ikabidi mamlaka ya uteuzi ipige chini jina lake. Au labda yeye mwenyewe SK alitaarifiwa kuhusu uteuzi akaanza kupata wenge na habari kuanza kuvuja.
Hawez kiteuliwa mtu hata elimu yake haieleweki,serikali kati ya vyote inazingatia zaidi sifa za kitaaluma!!

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
3272D150-D3F1-42D7-9937-568704135CD6.jpeg


Na Kevin Lameck

Kama ipo sehemu ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amepatia katika teuzi zake za karibuni, bhasi miongoni mwake ni uteuzi wa sasa wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Gerson Msigwa.

Bwana Mobhare Matinyi, Mkuu wa wilaya ya Temeke ameteuliwa kuwa Msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari - Maelezo.

Kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya mwezi wa saba mwaka huu, Mwanahabari huyu kitaaluma, alikuwa akitumika kwenye jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika maarufu kama SADC.

Muda mfupi kabla ya uteuzi huu, wiki iliyopita, nikiri kuwa nilibahatika kuzungumza naye kupitia kipindi chetu cha runinga kiitwacho #TheBantu sambamba na mazungumzo mafupi baada ya kipindi.

Bahati iliyoje kuwa tuligusia pia kuhusu sehemu muhimu ya mawasiliano na mahusiano ya umma kwa serikali ya Rais Samia na namna ilivyo muhimu katika kujenga picha na sifa nzuri ya serikali.

Nitasema machache kumuhusu ili kuchagiza maoni yangu ya awali kuhusu ubora na uzuri wa uteuzi huu wa Bwana Matinyi.

Mosi, Mh. Matinyi ana exposure ya juu sana ambayo ni nadra kuikuta kwa viongozi wengi wa sasa. Nafasi alizopita awali kuanzia kwenye uandishi wa habari, Uhariri mkuu wa magazeti kadhaa na kwenye jumuiya za kimataifa kumemfanya kuwa na utashi,m na mwenye kujaa maarifa na taarifa nyingi zilizomjengea upekee wa aina yake.

Pili; Mh. Matinyi ana uelewa mpana kuhusu siasa za ndani ya nchi, za jumuiya za kimataifa pamoja na hadhira yake kwa ujumla. Suala hili litampa wakati mzuri kuwa msaada kwa Rais na Chama chake katika kushauri na kuupasha umma taarifa zenye kujitosheleza katika urari wa habari na mawasiliano ya umma.

Tatu; Mh Matinyi ni mzungumzaji mzuri sana. Anajua kupangilia na kuumba maneno vyema akiongozwa na hekima ya kufahamu cha kusema na kisemwe wakati gani.

Nne;Mh Matinyi ni msikilizaji mzuri sana wa maoni ya watu. Kwa takribani muda wote niliokuwa naye alielekeza masikio yake zaidi kwangu kusikiliza na kujaribu kupata mtazamo na maoni mbalimbali na kutamani kusikia ninavyoyaangalia mambo.

Mwisho,Niliuona uwezo wake pia mkubwa katika nidhamu na kufuatilia masuala mbalimbali yahusuyo kazi yake. Sio kiongozi wa kukaa ofisini. Wingi wa taarifa alizonazo kuhusu wilaya yake kwa miezi mitatu tu aliyotumika kama Mkuu wa Wilaya ulitosha kuonesha namna ambavyo si kiongozi wa kupokea taarifa tu ofisini.

Kwa muda wa miezi mitatu ya uDC ameiacha Temeke ikiwa kinara wa usafi miongoni mwa wilaya tano za Dar es salaam, Amefanikiwa kuhuisha data za kodi kwa wafanyabiashara wote wa Temeke, amewezesha pia ongezeko la makusanyo ya kodi na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.

Aidha Mobhare aliwezesha mpangilio mzuri wa wafanya biashara wadogo maarufu kama Machinga , bila ya kutumia nguvu na hatukumsikia popote akilumbana na wahusika ama waathirika wa mageuzi mbalimbali huko wilayani Temeke.


Msingi wake mkubwa umekuwa ni kutoa elimu ya ufahamu kwa wananchi na kuacha wahusika wajiongoze na kujiiamulie mambo yao katika namna nzuri kulingana na matakwa ya serikali.


Kila la Kheri Comrade Matinyi Mobhare.


🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Huyu atakuwa msemaji wa kikweli kimataifa tofauti na Gerson Msigwa ambaye taarifa zake zilikuwa kwa ajili ya kujulisha umma wa ndani tu kipropaganda, wakati nchi hii imefunguka kimataifa pia lakini Gerson Msigwa amepwaya kimataifa .


Matinyi amepitia mengi kimataifa UNISA, SADC na uandishi wa nyuzi hapa JF n.k

TOKA MAKTABA :
1696208153440.png

Tukio la kukumbukwa lilitokea siku ya Jumapili 23,2007 mjini New York katika hoteli ya Grand Hyatt ambapo uongozi wa TADI ulipata fursa adimu kukutana na mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete.
 
Back
Top Bottom