Mobhare Matinyi ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari–MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali

Kuna nchi jeshi linaamua kuchukua madaraka... na hawana hitaji la kujenga chama chochote kiuchumi!
Ila umefanya vizuri kuliweka bayana... kumbe ccm inajijenga kwa Kodi za waTanzania.
Kwaiyo unafananisha jeshi na chama cha siasa tena cha upinzani ambacho hata hakijawai kushuka dola ?AMKA KIONGOZI UMELALA
 
Kuna nchi jeshi linaamua kuchukua madaraka... na hawana hitaji la kujenga chama chochote kiuchumi!
Ila umefanya vizuri kuliweka bayana... kumbe ccm inajijenga kwa Kodi za waTanzania.
Ccm ilishajijenga muda mrefu ni tofauti na chama kinachoenda kuanza moja
 
Hongera kwake sana tu ila
 
Nawaza tu endapo nchi hii itachukuliwa na chadema au upinzani ,je itachukua miaka mingapi kukijenga chama hicho kiuchumi kwa pesa ya walipa kodi wa Tanzania ndio maendeleo ya nchi yaje badae?nikiyakumbuka haya naamua kusimama na mama 2025
Ningesema una fikra potofu kama wengi wasiokuwa na uelewa, lakini kwa mtu kama wewe, siyo fikra potofu, bali ni kupigania maslahi yanayopatikana toka huko CCM.

CHADEMA kuiondoa CCM haina maana na wao wabakie madarakani kwa ung'ang'anizi kama wanavyofanya CCM.
Kipaumbele sasa hivi ni jinsi ya kuiondoa CCM madarakani, ili tuanze safari mpya bila ya CCM.
Hata chama cha mzee Rungwe kingejitutumua na kuiondoa CCM, ni bora zaidi.

Sasa najua kwa mtu kama wewe huwezi/hutaki kuyaelewa haya.

Sasa mnataka hadi iweje, tuwalilie ili ya Gabon yaje hapa?
 
Hujanielewa sehemu mkuu wasiwasi wangu ni kwamba je hicho chama pinzani kikija unahisi kitaweka maendeleo ya nchi mbele kuliko maendeleo ya chama?wote ndo walewale kujilimbikizia mali ndio kipaumbele
 
Hujanielewa sehemu mkuu wasiwasi wangu ni kwamba je hicho chama pinzani kikija unahisi kitaweka maendeleo ya nchi mbele kuliko maendeleo ya chama?wote ndo walewale kujilimbikizia mali ndio kipaumbele
Nilikuelewa vizuri tu, ila naona ni wewe hutaki kuelewa ninayoeleza mimi.
Ni hivi: Tuweke "maendeleo ya nchi" pembeni kwanza; kwani tayari tunajua, chini ya CCM hata ikiendelea kuwepo madarakani miaka mia moja, kama ilivyo hivi sasa maendeleo ya nchi itabaki kuwa hadithi tu.

Nasema kuwa CHADEMA, au chama kingine chochote cha siasa, au hata nje ya siasa, kipaumbele kwa sasa ni kuiondoa CCM, ambayo imekataa kuondoka kwa hiari, kwa kutumia njia mbalimbali zisizo halali kubaki madarakani.

Kwa sasa hivi, ni CHADEMA pekee wanaoonyesha dalili kidogo ya kuwa na uwezo huo, wa kuiondoa CCM. Hiyo ndiyo kazi tunayotaka waifanye.
Hayo ya kuleta maendeleo, tutashughulika nayo baada ya hili la kutokuwepo madarakani CCM.
 
Hakudhaniwa kuwa msemaji mkuu wa serikali. Kikeke alambishwe tu ukuu wa wilaya and then aje apate appontment nyingine kubwa kulingana carier yake. TBC ipo anaweza kuwa bosi huko na Rioba akapanda ngazi ya juu
 

Ndugu yangu. Hizo sifa zote ulizompatia kama hana ushawishi “orator” wa kusikilizwa ni kazi bure. Ndo maana unaona ZnZ walimchukua Charles Hilary. Salim Kikeke alikua mtu sahihi kwa sababu ana ushawishi wa kusikilizwa na kifuatiliwa
 
Huyu jamaa hata hajawahi kusikika popote duuuh hii noma sasa si atakua ana-mute tu mda wote maana sio mpigadomo km Ally Kamwe Mo Ally na wengine ambao ni 'Wasemaji' huwezi kua msemaji alafu haujui kupigadomo
Mobare matinyi ni mwandishi nguli labda wewe ndio hujamsikia ,usemaji wa serikali hauhitaji domo kama wafanyavyo kina kamwe na manara ile ni nafasi ya kuisemea serikali mambo ya msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…