Bosspraise
Member
- Feb 10, 2020
- 98
- 74
- Thread starter
- #21
VITU VYA KUWA NAVYO ILI UPATE KIBALI CHA UJENZI
👇👇
Kuwa na michoro ya ramani ya jengo iliyo kamilika,
iwasilishwe ikiwa kwenye majalada kwa namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka.
Michoro hiyo iwasilishwe ifuatavyo:-
• Seti tatu za michoro ya jengo (Archectural drawing)
• Seti mbili za michoro ya vyuma/mihimili (structural drawings) kwa michoro ya ghorofa
MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI
Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-
👉🏻 Namna jengo litakavyokuwa (plans, sections, elevations, foundation and roof plan)*
👉🏻Namba na eneo la kiwanja kilipo
👉🏻 Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
👉🏻Jina la mchoraji, ujuzi na anwani
👉🏻Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
👉🏻 Ujazo wa kiwanja (Plot coverage)
👉🏻Uwiano (Plot ratio)
👉🏻 Matumizi yanayokusudiwa
👉🏻Idadi ya maegesho yatakayokuwepo
👉🏻 Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks)
👉🏻 Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo
VIAMBATANISHO
👉🏻Fomu za maombi zilizojazwa kwa usahihi
• Hati ya mmiliki wa kiwanja au barua ya toleo
👉🏻Kumbumbuku nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo, makabidhiano n.k
👉🏻 Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo
👉🏻Mabadiliko ya matumizi ya ardhi
P.s Blchomes tutakuandalia documents zote zinazohitaji kupata kibali cha ujenzi ... zinazotakiwa kuandaliwa na msanifu wa majengo ..
. Na kufatilia kibali cha ujenzi kama utahitaji hiyo huduma dar es salaam.
Wasiliana nasi zaidi 0742892195