Mohamed Said alifungwa wakati wa Nyerere, asamehewa wakati wa Rais Samia

Mohamed Said alifungwa wakati wa Nyerere, asamehewa wakati wa Rais Samia

Aache porojo na kutafuta huruma kwa baadhi ya makundi! Kimsingi huyu alikuwa ni mhalifu tu kama wahalifu wengine. Ashukuru alipata hata huo msamaha.

Yaani kirahisi tu uende na silaha bar, huku umeiweka kwenye begi! Unakunywa pombe! Unalewa! Baadaye unaondoka kwenda kujisaidia, huku begi umeliacha mezani! Unarudi na kuendelea tu kunywa! Mwishoni unakuta begi na silaha havipo!!

Uzembe wa aina gani huu kwa mtu anayeitwa Mwanajeshi?
 
Usiku wa Februari 24 mwaka 1982 utabaki kwenye kumbukumbu ya kudumu kichwani kwa Mohamed Said (70) kutokana na tukio kubwa lililomkuta siku hiyo na kumfanya akae gerezani kwa miaka 40.

Kama angejua kinachokwenda kumtokea siku hiyo huenda angebadilisha mwelekeo, lakini kwa kuwa hakutambua alijikuta akifuata starehe iliyokatisha uhuru wake akiwa kijana na kurejeshewa tena uzeeni muda mrefu ukiwa umeshapotea.

Mzee huyu aliyeingia gerezani akiwa kijana wa miaka 30 na kutoka akiwa na miaka 70 ni miongoni mwa wafungwa waliopata msamaha wa Rais Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa mwaka jana wakati maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru.

Mwananchi limefunga safari hadi Chamazi, Dar es Salaam kukutana na mzee huyo ambako amepata hifadhi baada ya kutoka gerezani na kukuta hana ndugu yeyote uraiani huku wanafamilia wake wengi wakiwa wameshaaga dunia.

Mohamed, ambaye alikuwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akifanya kazi ya kuangalia usalama kwenye ghala la chakula la jeshi, alikutana na tukio saa chache baada ya kumaliza majukumu yake na kwenda uraiani kwa ajili ya kujiburudisha.

Akiwa amevaa kiraia na begi lake dogo alilohifadhi silaha na vitambulisho vyake, alitoka kazini kwake Lugalo na kwenda kupumzisha akili Manzese kabla ya kurejea nyumbani kwake Mwenge.

Huko Manzese alikwenda kwenye baa maarufu wakati huo ilikuwa ikifahamika kama Matunda Bar ambapo aliweka begi lake mezani na kuanza kupiga kinywaji.

Kwa kuwa eneo hilo alikuwa mwenyeji hakuna na wasiwasi na kile alichoweka kwenye begi, aliendelea kunywa na kuna wakati alinyanyuka kwenda msalani na hata aliporudi hakuwa na wazo la kuangalia begi lake kama lipo.

“Ilipofika saa tatu na nusu kuelekea saa nne nikaona sasa pombe imeshatosha, niondoke zangu kurudi nyumbani, hapo ndipo nikapata akili ya kuangalia begi langu pale mezani sikuliona, nilishtuka na kitu cha kwanza kuwaza ni kuhusu ile silaha, pili ndani ya lile begi kuna vitambulisho vyangu, jambo hili lilinifanya nichanganyikiwe.

“Nilijaribu kutafuta pale kwa muda bila mafanikio, nikiwauliza niliokaa nao wanasema hawajamuona mtu aliyechukua begi na huwezi kumuwajibisha muuzaji ilibidi nirudi kambini, kule nilipoelezea mazingira ya tukio zima ikabidi niende polisi kutoa taarifa, huko nikakuta tayari taarifa zangu zimefika askari wananigeuzia kibao na kuniambia mimi ni mhalifu.

Hilo lilitokana na vitambulisho vyake kukutwa pamoja na silaha iliyotumika kwenye tukio la wizi wa gari na mauaji.

Kadiri alivyojaribu kuelezea kuwa silaha yake iliibiwa, hivyo hausiki na tukio hilo hakueleweka na hatimaye akawekwa chini ya ulinzi na rasmi akabadilika jina kutoka kuwa askari hadi mtuhumiwa.

Alikaa kituoni hapo kwa takribani siku saba ndipo alipopelekwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kesi kuanza kutajwa akiwa na wenzake watatu waliokamatwa na kuhusishwa na tukio hilo.

Kupelekwa kwake mahakamani kukamfanya kupelekwa katika gereza la Keko kama mahabusu ambako alikaa kwa miaka 10 kabla ya kuhukumiwa rasmi na kuanza kutumikia adhabu yake.

Anasema tofauti na ilivyo sasa ambapo kesi zinaendeshwa ndani ya muda mfupi, wakati huo rushwa ilikuwa ikitumika kuchelewesha upelelezi hivyo, walijikuta wakisota kwa muda mrefu kwa sababu kuna wengine waliohusishwa na kesi hiyo walikuwa nje.

Katika kipindi chote cha miaka 10 aliyokuwa mahabusu bado aliendelea kuhesabika kama mwanajeshi na akapandishwa cheo kuwa sajenti akiendelea kupata stahiki zake zilizoelekezwa kwa familia yake hadi pale alipohukumiwa ndipo ilipokoma rasmi.

“Kesi ilitajwa kwa muda mrefu kabla ya kuanza kusikilizwa, hivyo tuliendelea kusota mahabusu hadi pale iliposikilizwa na hatimaye baada ya miaka 10 ikaonekana tuna hatia. Nakumbuka ilikuwa Mei 20 mwaka 1992 ndiyo hukumu yetu ilitoka tukahumumiwa kunyongwa.

“Siku hiyo ilikuwa ngumu mno kwangu, moyoni nilikuwa kama nimechomwa na msumari wa moto yaani najua kabisa sihusiki, lakini nakumbana na adhabu kali namna hii. Ile sauti ya kwamba wamehukumiwa kunyongwa ilikuwa ikijirudia masikioni mwangu, sikuamini kwamba hili linanikuta mimi.

“Wazazi wangu walipatwa na mshtuko, hawakutegemea kama ningekutwa na jambo zito kama hilo, sikuwa na la kufanya nikamuomba Mungu anipe moyo wa ujasiri kuweza kukabiliana na hilo kwa kuwa niliamini kwa akili na nguvu zangu mwenyewe siwezi.”

Si yeye wala wenzake wawili waliokubaliana na adhabu hiyo, hivyo wakafikia uamuzi wa kukata rufaa, hilo likafanyika kwa haraka na wakawasilisha maombi yao kunakohusika.

Baada ya kuhukumiwa, Mohamed akapangiwa kwenda gereza la Ukonga kusubiri siku ya adhabu kama ilivyoamuriwa huku kichwani mwake akijua kinachofuata ni kunyongwa.

Pamoja na ukweli huo bado alikuwa na matumaini ya rufaa waliyokata ambayo hata hivyo haikuwa na matokeo chanya kwa wote, mmoja ndiye aliyeshinda na kuachiwa huru.

Hivyo gerezani wakabaki wawili hapo ndipo alipotambua na kukubaliana na ukweli kuwa hayo ndiyo makazi yake rasmi hadi pale utekelezaji wa adhabu yake utakapofanyika.

Maisha mapya baada ya kuhukumiwa

Akiwa gerezani alijitahidi kuwa mtiifu na kushirikiana na wafungwa wenzake kwa kila hali na akifuata maelekezo ya askari magereza huku akijiweka zaidi karibu na Mungu akiamini yeye ndiye anayejua hatima yake.

“Kiukweli ilifika wakati nikaona sina uwezo wa kufanya chochote nimuachie Mungu, nijiweke karibu zaidi naye anijalie afya njema wakati wote nikiwa pale gerezani na hata akiamua kunichukua, niwe katika mazingira mazuri. Nilikuwa nasali na kitu msichojua kule watu wanasali mno yaani uwepo wa Mungu upo kwa kiasi kikubwa,” alisema. Je nini kilitokea wakati akiwa gerezani kusubiri hukumu yake ya kunyongwa?

Fuatilia kesho.

Mwananchi
Yaani utoke Lindo uingie mtaani kulewa na silaha?,halafu aseme alionewa kwa kuibiwa silaha halafu ikatumike kufanyia uharifu?

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Mohamed Said aseme tu ukweli kuwa alikodisha silaha na vitambulisho vyake Kwa ma-jambazi wakatekeleza tukio!
Huwezi kukodisha silaha na vitambulisho, no way. Theory ni kwamba alikimbizwa au aliondoka eneo la tukio kwa haraka kiasi begi lenye vitambulisho likabaki, na pia silaha ikabaki. Lakini najiuliza, hao wahudumu wa Bar hawakwenda kutoa ushahidi kwamba walimuona akija na hilo begi na ghafla hawakuliona? Pengine ingemsaidia
 
Aache porojo na kutafuta huruma kwa baadhi ya makundi! Kimsingi huyu alikuwa ni mhalifu tu kama wahalifu wengine. Ashukuru alipata hata huo msamaha.

Yaani kirahisi tu uende na silaha bar, huku umeiweka kwenye begi! Unakunywa pombe! Unalewa! Baadaye unaondoka kwenda kunisaidia, huku begi umeliacha mezani! Unarudi na kuendelea tu kunywa! Mwishoni unakuta begi na silaha havipo!!

Uzembe wa aina gani huu kwa mtu anayeitwa Mwanajeshi?
Kwamba aliporudi hata hakugundua kwamba begi halipo, hadi baadaeeee, hapo ndio nimechoka; maana yake huyu hata angeweza kurudi nyumbani bila hilo begi, akalala hadi asubuhi ndio akashtuka kaacha begi bar..
 
Askari baada ya kazi unapaswa kukabidhi lindo na silaha zote

Ilikuaje yeye akatoka na Silaha?

Ilikuaje utoke Lugalo uende Manzese 'ukapumzishe' akili ukifahamu ukishalewa hutoweza kuwa na udhibiti wa Silaha yako?

Lugalo kwenda kwake Mwenge ni karibu kuliko kwenda Manzese tena enzi hizo za usafiri wa shida kwanini ali opt kuanza kwenda Manzese ndio arudi home akiwa na Silaha?

Binafsi siamini kama hakuwa na nia ovu
Adhabu aliyopewa alistahili
 
Mimi nina maswali ambayo ningemuuliza , ambayo haya maswali nahisi kama hakuwa na majibu mazuri, hakuna taahira yeyote angeweza kumuachia huru, hata kama hana hatia.

1.) Kutoka Lugalo kwenda Manzese inabidi upite Mwenge kwanza ambako ni nyumbani kwake, kwanini hakuacha mizigo yake hapo Mwenge ndio aende Manzese akapate starehe?

2.) Kwa akili za kawaida za kibinadamu, unaweza ukaacha begi la silaha za kijeshi na vitambulisho vyako juu ya meza ya bar na kwenda msalani bila kukabidhi hata kaunta? Ukizingatia bar wanaingia watu wa kila aina?

3.) Muda wa kupoteza begi lake hadi ripoti ya ujambazi kufika polisi ilikuwa ni masaa mangapi? Yaani mtu ambae hajui ndani ya begi lako kuna nini aibe begi, awe anajua jinsi ya kutumia hiyo silaha, awe alishapanga tukio la ujambazi, maana tukio kama hilo hukurupuki tu, inatakiwa angalau siku 1 kabla uwe umepanga, aweze kutekeleza wizi na mauaji, polisi wafike wachukue ushahidi , hayo yote wamewezaje kutokea ndani ya muda mfupi hivyo? Halafu baadae wewe ndio unaenda kuripoti? How?!

Inafikilisha kwa kweli.. watu waliiba kibegi chake siku hiyo hiyo na wakaenda kupigia tukio siku hiyo hiyo.. jamaa inabidi amshukuru MAMA
 
Huwezi kukodisha silaha na vitambulisho, no way. Theory ni kwamba alikimbizwa au aliondoka eneo la tukio kwa haraka kiasi begi lenye vitambulisho likabaki, na pia silaha ikabaki. Lakini najiuliza, hao wahudumu wa Bar hawakwenda kutoa ushahidi kwamba walimuona akija na hilo begi na ghafla hawakuliona? Pengine ingemsaidia
Anasema kulikuwa na watu wengine waliohusika na tukio walikuwa nje so pengine ndio waliocheza na mashahidi.
 
Askari baada ya kazi unapaswa kukabidhi lindo na silaha zote

Ilikuaje yeye akatoka na Silaha?

Ilikuaje utoke Lugalo uende Manzese 'ukapumzishe' akili ukifahamu ukishalewa hutoweza kuwa na udhibiti wa Silaha yako?

Lugalo kwenda kwake Mwenge ni karibu kuliko kwenda Manzese tena enzi hizo za usafiri wa shida kwanini ali opt kuanza kwenda Manzese ndio arudi home akiwa na Silaha?

Binafsi siamini kama hakuwa na nia ovu
Kuna ukweli kaamua kuuficha.Nahisi alikuwa mhalifu
 
Back
Top Bottom