Mohamed Said alifungwa wakati wa Nyerere, asamehewa wakati wa Rais Samia

Mimi nina maswali ambayo ningemuuliza , ambayo haya maswali nahisi kama hakuwa na majibu mazuri, hakuna taahira yeyote angeweza kumuachia huru, hata kama hana hatia.

1.) Kutoka Lugalo kwenda Manzese inabidi upite Mwenge kwanza ambako ni nyumbani kwake, kwanini hakuacha mizigo yake hapo Mwenge ndio aende Manzese akapate starehe?

2.) Kwa akili za kawaida za kibinadamu, unaweza ukaacha begi la silaha za kijeshi na vitambulisho vyako juu ya meza ya bar na kwenda msalani bila kukabidhi hata kaunta? Ukizingatia bar wanaingia watu wa kila aina?

3.) Muda wa kupoteza begi lake hadi ripoti ya ujambazi kufika polisi ilikuwa ni masaa mangapi? Yaani mtu ambae hajui ndani ya begi lako kuna nini aibe begi, awe anajua jinsi ya kutumia hiyo silaha, awe alishapanga tukio la ujambazi, maana tukio kama hilo hukurupuki tu, inatakiwa angalau siku 1 kabla uwe umepanga, aweze kutekeleza wizi na mauaji, polisi wafike wachukue ushahidi , hayo yote wamewezaje kutokea ndani ya muda mfupi hivyo? Halafu baadae wewe ndio unaenda kuripoti? How?!
Ningeweza kumsaidia kujibu jibu la kwanza tu, hayo mengine mawili ndio yaliyomtia hatiani.
 
Sheria za kazi zinasemaje? Maana kama kila mtu anaondoka na vitendea kazi akitoka ofisini, halafu vikaishia kupotea, nini kinaweza kutokea? Popote duniani, kazi zina taratibu na sheria zake. Ukivunja taratibu hizo pia kuna gharama zake. Pole sana kwake
Kumbe Manzese uhuni ulianza siku nyingi
Sasa hivi uhuni umepungua, Magomeni, Manzese na Mburahati kulikuwa na uhuni sana, na makundi ya wezi na vibaka.
 
Huyo mzee asitafute huruma tu aseme tu ukweli alishiriki na anajutia alichotenda BC hata jamii itaona amejirekebisha Sasa kuanza kudanganya danganya haileti sense yyte yani mtu unasilaha unapitikiza mwenge Mpaka manzese Kirahisi tu na unafika bar unaiacha sehem ya wazi bila ya uangalizi foolish kabsa tena ingekua mm ningemrejesha jela tena akafie huko huko, kpnd cha jiwe Kuna yule mzee alikiri kabsa kwamba alimuua mkewe na akasamehewa fresh tuu,, asitafute huruma ya watu Shenz kabsa
 
mleta mada,
nimesoma bandiko lako mwanzo mwisho, nimebaini kulikuwa hakuna haja ya kutaja jina la nyerere kwenye title. ingetosha tu kuandika miaka aliyokaa jela.

najua title yako itawavutia watu "fulani" waje kwa speed and emotion kuchangia uzi wako.
Mie mwnyw kilichonileta ni Nyerere na Samia, baada ya kusoma nikaona mtoa post naye anania ovu...akamalizie kifungo cha aliyeachiwa
 
Nilivyokuwa nawaza mie askari akiwa anaenda lindo huwa wanaanzia kwenye silaha ambapo huweka Saini akithibitisha idadi ya risasi na aina ya silaha aliyochukua, na akitoka lindo ama akimaliza zamu yake hurudi kusaini tena akithibitisha kurudisha alivyochukua na kutolea maelezo kama kuna kilichotumika. Ama kipindi hicho hapakuwa na utaratibu huo hadi azunguke na silaha!?. Naona uwalakini kwenye stori ya mzee mudi[emoji2960]
 
Tumshaurini mtoa uzi asitishe stori yake maana mpaka sasa anaonekana Ana makosa mengi sana [emoji23][emoji23]
 
Ngoja nimsaidie kidgo yani hapo inaonekana hilo begi analobebaga huwa ndani anaweka nguo za kubadilisha pamoja na silaha inamana alipomaliza lindo alibqdilisha nguo zake akawwka kwenye begi pamoja na silaha ndo akasepa manzese kupiga ulabu .... lakini bado amefanya makosa mengi ya kiufundi ...
Mkuu wengine sisi ni majeshi mengi. Sheria ya silaha unaichukua armory unaenda kazini na ukitoka kazini unairudisha armory na si vinginevyo
 
Mimi nina maswali ambayo ningemuuliza , ambayo haya maswali nahisi kama hakuwa na majibu mazuri, hakuna taahira yeyote angeweza kumuachia huru, hata kama hana hatia.

1.) Kutoka Lugalo kwenda Manzese inabidi upite Mwenge kwanza ambako ni nyumbani kwake, kwanini hakuacha mizigo yake hapo Mwenge ndio aende Manzese akapate starehe?

2.) Kwa akili za kawaida za kibinadamu, unaweza ukaacha begi la silaha za kijeshi na vitambulisho vyako juu ya meza ya bar na kwenda msalani bila kukabidhi hata kaunta? Ukizingatia bar wanaingia watu wa kila aina?

3.) Muda wa kupoteza begi lake hadi ripoti ya ujambazi kufika polisi ilikuwa ni masaa mangapi? Yaani mtu ambae hajui ndani ya begi lako kuna nini aibe begi, awe anajua jinsi ya kutumia hiyo silaha, awe alishapanga tukio la ujambazi, maana tukio kama hilo hukurupuki tu, inatakiwa angalau siku 1 kabla uwe umepanga, aweze kutekeleza wizi na mauaji, polisi wafike wachukue ushahidi , hayo yote wamewezaje kutokea ndani ya muda mfupi hivyo? Halafu baadae wewe ndio unaenda kuripoti? How?!
Huyu mzee anahusika,kwenye majeshi kuna majambazi wengi tu
 
Duuh!! Ikiwa mpaka kwenye rufaa hakuchomoka hapo ni dhahiri anahusika sema tu anajitoa ili kutafuta huruma ya watu hasa baada ya kurejea uraiani huku akiwa hana mbele wala nyuma.
 
“Kiukweli ilifika wakati nikaona sina uwezo wa kufanya chochote nimuachie Mungu, nijiweke karibu zaidi naye anijalie afya njema wakati wote nikiwa pale gerezani na hata akiamua kunichukua, niwe katika mazingira mazuri. Nilikuwa nasali na kitu msichojua kule watu wanasali mno yaani uwepo wa Mungu upo kwa kiasi kikubwa,” alisema. Je nini kilitokea wakati akiwa gerezani kusubiri hukumu yake ya kunyongwa?
Ni kweli kwamba Mungu wetu tunamkumbuka mno wakati wa Mateso tu, mwanadamu anapofikia hatua hawezi kabisa kufanya jambo kwa uwezo wa kibinadamu ndipo anapomkumbuka Mola wake aliye juu.

Laiti tungalijua kumtafuta Muumba wetu hata siku tulizo na nguvu, furaha, pesa na afya basi Mwenyezi wetu angefurahi zaidi na zaidi.

Hata hivyo, Mungu anasema " Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Haya maandiko tuyasoma katika Yeremia 33:3
Vilevile Mfalme Daudi katika tenzi zake ( Zaburi) anatuambia hivi " Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Zaburi 46:1

Pole ndugu yetu, laiti ungalimpokea Muumba wako enzi za ujana wako basi haya yote ya kupiga ulabu hadi kusahau majukumu yako na vifaa vya dola yasingekukuta.

Mimi naona amehusika na tukio kwa namna ya kuazimisha au kukodisha silaha.

Yaani nipange uhalifu ila silaha niisubiri Manzese kwa mwanajeshi anayetoka Lugalo aje kuacha begi lenye silaha mezani?

Tungekua tunadocument kesi mwanzo mwisho ili tunamsikiliza yeye na tunaangalia facts za mahakama.
 
Mimi nina maswali ambayo ningemuuliza , ambayo haya maswali nahisi kama hakuwa na majibu mazuri, hakuna taahira yeyote angeweza kumuachia huru, hata kama hana hatia.

1.) Kutoka Lugalo kwenda Manzese inabidi upite Mwenge kwanza ambako ni nyumbani kwake, kwanini hakuacha mizigo yake hapo Mwenge ndio aende Manzese akapate starehe?

ILIKUWA NI DHARURA YA HARAKA NA GHAFLA SANA.

2.) Kwa akili za kawaida za kibinadamu, unaweza ukaacha begi la silaha za kijeshi na vitambulisho vyako juu ya meza ya bar na kwenda msalani bila kukabidhi hata kaunta? Ukizingatia bar wanaingia watu wa kila aina?
HII NI OVERSIGHT--UNINTENTIONAL FAILURE OR MISTAKE KWA SABABU YA MAZOEA YAKE MABAYA. SAWA NA WALE WAJEDA WA UBALOZI WA UFARANSA ^GAIDI^ HAMZA ALIWAPOKONYA SILAHA.

3.) Muda wa kupoteza begi lake hadi ripoti ya ujambazi kufika polisi ilikuwa ni masaa mangapi? Yaani mtu ambae hajui ndani ya begi lako kuna nini aibe begi, awe anajua jinsi ya kutumia hiyo silaha, awe alishapanga tukio la ujambazi, maana tukio kama hilo hukurupuki tu, inatakiwa angalau siku 1 kabla uwe umepanga, aweze kutekeleza wizi na mauaji, polisi wafike wachukue ushahidi , hayo yote wamewezaje kutokea ndani ya muda mfupi hivyo? Halafu baadae wewe ndio unaenda kuripoti? How?!

ALIKUWA AMELEWA SANA HALI ILIYOMCHANGANYA ASIAMINI BEGI AMEIBIWA KWELI AMA ALIIACHA HOME, HAKUJA NAYO.
 
Pamoja na imani yake kuongezeka Mohamed alikuwa amekata tamaa ya kuishi, hivyo wakati wote akiwa gerezani hakutaka kujifunza ujuzi wowote akiamini hatoweza kuutumia kwa sababu kilicho mbele yake ni kunyongwa hadi kufa.

Hilo likamfanya ajikite kwenye shughuli anazopangiwa kila siku, lakini si kutafuta ujuzi ambao ungemfanya kubobea kwenye eneo fulani kama ambavyo wafungwa wengine hufanya mfano ujenzi, ufundi seremala, shughuli za kiwandani.

Anasema wakiwa gerezani walikuwa wanapata wasaa wa kusikiliza redio na televisheni, hivyo walikuwa wakifahamu masuala mbalimbali yalikuwa yakiendelea ndani na nje ya nchi.

Kifungo chake hakikuishia Ukonga, kwani katika kipindi cha miaka 30 baada ya kuhukumiwa alihamishwa kwenye magereza kadhaa ikiwemo la Dodoma, Tanga alikokaa miaka 22 na hatimaye akarejea tena Ukonga.

Siku moja katika kusikiliza habari kwenye redio wakapata taarifa kuwa adhabu ya kunyongwa imefutwa na Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizosaini makubaliano ya kuzuia adhabu hiyo.

“Ilikuwa habari njema kwa tuliokuwa na adhabu ya kunyongwa nakumbuka ilikuwa wakati wa Rais Benjamin Mkapa, hilo jambo siwezi kusahau tulishukuru na kumuombea dua kwa Mungu ampe afya njema maana ametunusuru kwenye kifo, lakini bado tukawa na wasiwasi kwamba akija Rais mwingine itakuwaje.

“Basi niliendelea kukaa gerezani hadi mwaka 2005 ndipo nilipopewa taarifa rasmi kuwa adhabu imebadilishwa, imetoka kwenye kunyongwa hadi kifungo cha maisha, ilinipa matumaini kiasi fulani, lakini bado huwezi kufurahia kwa kuwa upo gerezani sehemu ambayo hauna uhuru,” anaeleza.

Hata hivyo, ile hofu ya kunyongwa ikawa imeondoka, akaielekeza akili yake kuamini kuwa maisha yake yote yatakuwa gerezani hivyo akalazimika kukubaliana na maisha ya gerezani na kufanya kila kinachotakiwa kufanyika.

“Kabla ya kuingia jeshini nilikuwa mchezaji na sisi ndio tulianzisha timu ya Simba B, nilipokuwa gerezani nikarudi kucheza mpira na kule tukawa na timu kabisa Simba na Yanga, tukawa tunajipa burudani kwa mtindo huo kujipotezea mawazo.

“Haikushia kucheza tu, tulikuwa mashabiki kindaki ndaki mpira ukichezwa huku uraiani na sie kule tunakuwa na presha kama ilivyo huku, kwa kifupi tulikuwa mashabiki hasa na wakati mwingine tulikuwa tunaandika barua kwenye klabu zetu na walikuwa wanatuletea misaada,” anasema.

Mwishoni mwa mwaka jana, alipata taarifa huenda akawa kwenye orodha ya wafungwa watakaosamehewa baada ya kutumikia kifungo chake kwa muda mrefu, habari hiyo aliifurahia lakini ilimpa mawazo.

Anasema hofu yake kubwa ilikuwa kuanza maisha ya uraiani, hakujua wapi aanzie na watu wake wa karibu wengi wameshafariki dunia, hivyo alijua anakwenda kukumbana na upweke na mahangaiko.

Hata hivyo, alijipa moyo na kujifariji ni bora maisha ya upweke akiwa huru kuliko kuendelea kukaa gerezani, hivyo kwa mara nyingine akamuomba Mungu amuonyeshe njia ya kuweza kuishi maisha mapya.

Maisha mapya uraiani

Desemba 9, 2021 siku ambayo Tanzania iliadhimisha miaka 60 ya Uhuru, Mohamed ni miongoni mwa waliofurahia siku hiyo kupita kiasi.

Ni siku ambayo alitoa mguu wake nje ya geti la Ukonga akiwa huru ikiwa ni baada ya kupita miaka 40 tangu awe katika hali hiyo.

Mohamed anasema mabadiliko aliyoyaona nje akatambua kuwa hawezi kufika popote kutokana na ugeni aliokuwa nao, hivyo akampigia simu rafiki yake ambaye alikuwa na namba zake.

“Alikuja kunifuata pale nikaenda kwake nikiwa najipanga kuwatafuta ndugu zangu au watu niliokuwa na uhusiano nao, maana nilivyotoka gerezani nimekuta wengi wamefariki dunia na hata maisha yamebadilika.

“Baba, mama, dada, kaka wote wamefariki, nyumba yetu iliyokuwa Temeke nimekuta ilishauzwa sijafanikiwa kukutana na ndugu yeyote. Hadi sasa naishi kwa msaada wa mtu ambaye kwa sasa namchukulia kama ndugu yangu,” anasema.

Kulingana na Mohamed, wakati anakamatwa alikuwa na watoto wawili, lakini kufungwa kwake kulimfanya apotezane nao na baadaye alipata taarifa za mtoto mmoja.

Anasema, “Najihesabu sina mtoto, nilikuwa na watoto wawili, wa kiume alikuwa na miaka miwili kama sio mitatu wakati nakumbwa na madhira haya na wa kike alikuwa na mwezi mmoja.

“Watoto hawa kila mmoja alikuwa na mama yake, basi kufungwa kwangu kukafanya nipotezane nao ila huyu wa kike nilisikia yeye na mama yake aitwaye Asha Kipini walishafariki. Sina uhakika wa taarifa hizo kama yupo hai wanitafute walikuwa wanaishi Mwananyamala”.

Kama ilivyo kwa mtu mwingine ambaye hakuwepo nchini kwa muda mrefu, hamu kubwa ya mzee huyu ni kufika maeneo aliyokuwa akizunguka miaka hiyo ila changamoto anayokutana nayo ni mabadiliko makubwa yaliyotokea katika jiji la Dar es Salaam ndani ya miaka 40.

“Sijui kama Matunda Bar bado ipo, ila natamani siku moja niende Manzese nikaone yale mazingira, mambo mengi yamebadilika. Yaani hata nikitembea barabarani najiona niko tofauti na watu wengine, najaribu kujitahidi kuzoea mazingira ya nje. Niliacha simu za mezani, sasa nimekuta simu za mkononi, basi nashangaa vitu vingi kwangu ni vipya.

“Changamoto kubwa ni shughuli ya kufanya, katika umri huu siwezi kufanya kazi ngumu naomba kama kuna uwezekano wafadhili wanisaidie nipate eneo nifanye biashara ndogo ndogo, ili niweze kupunguza makali ya maisha, nimeona huwezi kuishi kwenye jiji hili ukiwa huna shughuli ya kufanya,” anasema.

Kwa atakayeguswa kumsaidia Mohamed Said anapatikana kwa 0654718896
 
ILIKUWA NI DHARURA YA HARAKA NA GHAFLA SANA.

HII NI OVERSIGHT--UNINTENTIONAL FAILURE OR MISTAKE KWA SABABU YA MAZOEA YAKE MABAYA. SAWA NA WALE WAJEDA WA UBALOZI WA UFARANSA ^GAIDI^ HAMZA ALIWAPOKONYA SILAHA.

ALIKUWA AMELEWA SANA HALI ILIYOMCHANGANYA ASIAMINI BEGI AMEIBIWA KWELI AMA ALIIACHA HOME, HAKUJA NAYO.
Majibu dhaifu mno...
 
Hilo lilitokana na vitambulisho vyake kukutwa pamoja na silaha iliyotumika kwenye tukio la wizi wa gari na mauaji.

Nini kiliporwa, nani aliuwa, na maeneo gani haya matukio yalitokea....
Isije kuwa polisi waliaanza ushenzi wao tokea miaka ileee.....
 
Pamoja na imani yake kuongezeka Mohamed alikuwa amekata tamaa ya kuishi, hivyo wakati wote akiwa gerezani hakutaka kujifunza ujuzi wowote akiamini hatoweza kuutumia kwa sababu kilicho mbele yake ni kunyongwa hadi kufa.

Hilo likamfanya ajikite kwenye shughuli anazopangiwa kila siku, lakini si kutafuta ujuzi ambao ungemfanya kubobea kwenye eneo fulani kama ambavyo wafungwa wengine hufanya mfano ujenzi, ufundi seremala, shughuli za kiwandani.

Anasema wakiwa gerezani walikuwa wanapata wasaa wa kusikiliza redio na televisheni, hivyo walikuwa wakifahamu masuala mbalimbali yalikuwa yakiendelea ndani na nje ya nchi.

Kifungo chake hakikuishia Ukonga, kwani katika kipindi cha miaka 30 baada ya kuhukumiwa alihamishwa kwenye magereza kadhaa ikiwemo la Dodoma, Tanga alikokaa miaka 22 na hatimaye akarejea tena Ukonga.

Siku moja katika kusikiliza habari kwenye redio wakapata taarifa kuwa adhabu ya kunyongwa imefutwa na Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizosaini makubaliano ya kuzuia adhabu hiyo.

“Ilikuwa habari njema kwa tuliokuwa na adhabu ya kunyongwa nakumbuka ilikuwa wakati wa Rais Benjamin Mkapa, hilo jambo siwezi kusahau tulishukuru na kumuombea dua kwa Mungu ampe afya njema maana ametunusuru kwenye kifo, lakini bado tukawa na wasiwasi kwamba akija Rais mwingine itakuwaje.

“Basi niliendelea kukaa gerezani hadi mwaka 2005 ndipo nilipopewa taarifa rasmi kuwa adhabu imebadilishwa, imetoka kwenye kunyongwa hadi kifungo cha maisha, ilinipa matumaini kiasi fulani, lakini bado huwezi kufurahia kwa kuwa upo gerezani sehemu ambayo hauna uhuru,” anaeleza.

Hata hivyo, ile hofu ya kunyongwa ikawa imeondoka, akaielekeza akili yake kuamini kuwa maisha yake yote yatakuwa gerezani hivyo akalazimika kukubaliana na maisha ya gerezani na kufanya kila kinachotakiwa kufanyika.

“Kabla ya kuingia jeshini nilikuwa mchezaji na sisi ndio tulianzisha timu ya Simba B, nilipokuwa gerezani nikarudi kucheza mpira na kule tukawa na timu kabisa Simba na Yanga, tukawa tunajipa burudani kwa mtindo huo kujipotezea mawazo.

“Haikushia kucheza tu, tulikuwa mashabiki kindaki ndaki mpira ukichezwa huku uraiani na sie kule tunakuwa na presha kama ilivyo huku, kwa kifupi tulikuwa mashabiki hasa na wakati mwingine tulikuwa tunaandika barua kwenye klabu zetu na walikuwa wanatuletea misaada,” anasema.

Mwishoni mwa mwaka jana, alipata taarifa huenda akawa kwenye orodha ya wafungwa watakaosamehewa baada ya kutumikia kifungo chake kwa muda mrefu, habari hiyo aliifurahia lakini ilimpa mawazo.

Anasema hofu yake kubwa ilikuwa kuanza maisha ya uraiani, hakujua wapi aanzie na watu wake wa karibu wengi wameshafariki dunia, hivyo alijua anakwenda kukumbana na upweke na mahangaiko.

Hata hivyo, alijipa moyo na kujifariji ni bora maisha ya upweke akiwa huru kuliko kuendelea kukaa gerezani, hivyo kwa mara nyingine akamuomba Mungu amuonyeshe njia ya kuweza kuishi maisha mapya.

Maisha mapya uraiani

Desemba 9, 2021 siku ambayo Tanzania iliadhimisha miaka 60 ya Uhuru, Mohamed ni miongoni mwa waliofurahia siku hiyo kupita kiasi.

Ni siku ambayo alitoa mguu wake nje ya geti la Ukonga akiwa huru ikiwa ni baada ya kupita miaka 40 tangu awe katika hali hiyo.

Mohamed anasema mabadiliko aliyoyaona nje akatambua kuwa hawezi kufika popote kutokana na ugeni aliokuwa nao, hivyo akampigia simu rafiki yake ambaye alikuwa na namba zake.

“Alikuja kunifuata pale nikaenda kwake nikiwa najipanga kuwatafuta ndugu zangu au watu niliokuwa na uhusiano nao, maana nilivyotoka gerezani nimekuta wengi wamefariki dunia na hata maisha yamebadilika.

“Baba, mama, dada, kaka wote wamefariki, nyumba yetu iliyokuwa Temeke nimekuta ilishauzwa sijafanikiwa kukutana na ndugu yeyote. Hadi sasa naishi kwa msaada wa mtu ambaye kwa sasa namchukulia kama ndugu yangu,” anasema.

Kulingana na Mohamed, wakati anakamatwa alikuwa na watoto wawili, lakini kufungwa kwake kulimfanya apotezane nao na baadaye alipata taarifa za mtoto mmoja.

Anasema, “Najihesabu sina mtoto, nilikuwa na watoto wawili, wa kiume alikuwa na miaka miwili kama sio mitatu wakati nakumbwa na madhira haya na wa kike alikuwa na mwezi mmoja.

“Watoto hawa kila mmoja alikuwa na mama yake, basi kufungwa kwangu kukafanya nipotezane nao ila huyu wa kike nilisikia yeye na mama yake aitwaye Asha Kipini walishafariki. Sina uhakika wa taarifa hizo kama yupo hai wanitafute walikuwa wanaishi Mwananyamala”.

Kama ilivyo kwa mtu mwingine ambaye hakuwepo nchini kwa muda mrefu, hamu kubwa ya mzee huyu ni kufika maeneo aliyokuwa akizunguka miaka hiyo ila changamoto anayokutana nayo ni mabadiliko makubwa yaliyotokea katika jiji la Dar es Salaam ndani ya miaka 40.

“Sijui kama Matunda Bar bado ipo, ila natamani siku moja niende Manzese nikaone yale mazingira, mambo mengi yamebadilika. Yaani hata nikitembea barabarani najiona niko tofauti na watu wengine, najaribu kujitahidi kuzoea mazingira ya nje. Niliacha simu za mezani, sasa nimekuta simu za mkononi, basi nashangaa vitu vingi kwangu ni vipya.

“Changamoto kubwa ni shughuli ya kufanya, katika umri huu siwezi kufanya kazi ngumu naomba kama kuna uwezekano wafadhili wanisaidie nipate eneo nifanye biashara ndogo ndogo, ili niweze kupunguza makali ya maisha, nimeona huwezi kuishi kwenye jiji hili ukiwa huna shughuli ya kufanya,” anasema.

Kwa atakayeguswa kumsaidia Mohamed Said anapatikana kwa 0654718896
Mzee umamalizia hii stori na ID nyingine au...........
 
Back
Top Bottom