Mohamed Said alifungwa wakati wa Nyerere, asamehewa wakati wa Rais Samia

Inafikilisha kwa kweli.. watu waliiba kibegi chake siku hiyo hiyo na wakaenda kupigia tukio siku hiyo hiyo.. jamaa inabidi amshukuru MAMA
Usiseme siku hiyo hiyo. Sema muda huo huo! Because silaha ikipotea kwa namna hivyo, immediately unakimbilia kituo cha polisi. So, like under 30 minutes sinema nzima imepangwa na wahalifu na wezi wa gari.
 
Kwamba aliporudi hata hakugundua kwamba begi halipo, hadi baadaeeee, hapo ndio nimechoka; maana yake huyu hata angeweza kurudi nyumbani bila hilo begi, akalala hadi asubuhi ndio akashtuka kaacha begi bar..
baadaeeeeee = almost 10 hours! 🙂
 
Huwa ni normal KARMA kwa wahalifu kuacha ushahidi wa namna fulani, esp. kwenye eneo la tukio. US wezi wa pesa benki walibambwa na kutiwa hatiani, five months away, kwa sababu tu ya kipisi cha plastiki cha taa ya gari, kilichopasuka wakati wa harakati za kujikusanyia na ku-load mihela.

^This lone piece of evidence matched with uncanny exactness to the original dislocation on the very truck which had also been stolen and later abandoned.^
 
Kuna uwezekano mkubwa alihusika. Kuna askari mmoja Tanga alikua lindo CRDB miaka ya 2010 akakodisha silaha usiku afu imefika asubuhi jamaa hawajarudisha na hawapatikani. Akaona isiwe tabu akakimbia akaacha lindo. Mwenzake nae alokua nae lindo akakamatwa kusaidia upelelezi
 
Napenda sana crime and investigation channel...wenzetu ni balaa
 
Huyo alistahili kufungwa aisee.. tokea lini Askari akawa mzembe kiasi hicho?
 
Muongo mkubwa huyo.
Askari umemaliza mda wako wa ulinzi hukurudisha bunduki armory, ukaenda nyumbani kwako ukiwa na silaha ya serikali, ukabadili uniform na kuvaa nguo za kiraia, bunduki ukaiweka kwenye begi ukaenda nayo bar halafu bado ukawa huna umakini na silaha hiyo!! Huo ni uongo uliyopitiliza. Jambazi mkubwa wewe
 
Labda Mohamed Said alikuwa anaitumia kupata pombe za bure bar wakamchoka
 
hiyo no 3 anafika polisi anakuta taarifa za uhalifu zishapelekwa na mhalifu katambulika tyr ndani ya mda mfupi akiwa anasaka begi huo ni usanii
Ivi katika hali ya kawaid unaweza Acha begi yenye silaha ikiwa na vitambulisho vyako ivi huyu askari maadili ya jeshi anayqjua kweli? Kuna makosa mengi sana ya kiufundi amefanya
 
Ngoja nimsaidie kidgo yani hapo inaonekana hilo begi analobebaga huwa ndani anaweka nguo za kubadilisha pamoja na silaha inamana alipomaliza lindo alibqdilisha nguo zake akawwka kwenye begi pamoja na silaha ndo akasepa manzese kupiga ulabu .... lakini bado amefanya makosa mengi ya kiufundi ...
 
msimshangae sana huyo afande mbona wapo wazembe kama yeye adi leo hii,

nikiwa nasoma shule flani inayomilikiwa na jeshi la wananchi (JWTZ) nikiwa ni scout na ni kijana mtukutu, nlikua naelewana sana na askar wengi waliokua wanakuja kulinda pale shuleni, ilifikia hatua muda wa prepo(kujisomea usiku) mimi natumwa mtaan kununua ngada , pia kuna kupindi SIKU AMBAZO KUNA MECHI ZA MPIRA JAMAA WANANIACHIA SILAHA 3 AU NNE NAKAA NAZO VICHAKANI HADI MUDA WANARUDI. MIM NDIO NAENDA KULALA.(just imagine watanzania wenzangu! what kind of stupidity is this! faken!
 
Sheria za kazi zinasemaje? Maana kama kila mtu anaondoka na vitendea kazi akitoka ofisini, halafu vikaishia kupotea, nini kinaweza kutokea? Popote duniani, kazi zina taratibu na sheria zake. Ukivunja taratibu hizo pia kuna gharama zake. Pole sana kwake
Kumbe Manzese uhuni ulianza siku nyingi
 
Huwezi kubeba silaha kienyeji ukaipoteza, especially kama wewe ni askari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…