Mohamed Said ana siasa za kulialia

Mohamed Said ana siasa za kulialia

Unashangaa hlo huku ukijisahaulisha wale wanaodai kumuimbia Yesu mpaka stend.
Na wle wafufua watu na ninyi wenzawazimu mkiamn upo we nguchiro????
Hao unaowasema angalau hawaombi pesa ya kujenga shule. Wanaeneza Injili kwa staili wanayoijua wao. Halafu mnashangaa mpo wachache Serikalini
 
Kuna kitu kinaitwa, "the standard of the reasonable man."
Hebu tufafanulie hiyo "the standard of the reasonable man" ina vigezo gani?

Wewe mwenyewe ni one of the most unreasonable individuals kwenye jukwaa hili. Unaleta hoja/arguments hizohizo zilizochoka miaka nenda miaka rudi. Huna jipya. Unajihadaa vibaya sana kwa kudai eti watu wana hamu ya kujua utaandika nini. Jinga kabisa.
 
Unaweza kutupa ratio ya Wakristu kwa Waislamu kwenye population ya Tanzania?

Wakristu wamejitahidi sana kuwekeza kwenye elimu kuanzia level ya chini na kuendelea tofauti na Waislamu ambao wameweka msisitizo kwenye elimu ya dini
Belo,
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimejadili tatizo la suala la ratio baina ya Waislam na Wakristo na nikaeleza kuwa ni suala lililogubikwa na unyeti mkubwa.

Kwa ajili hii mimi sipendi kuingia ndani ya gunia hili na kuanza kuchakura kwa kuwa tutafungua mlango wa mabishano yasiyo na maana yoyote.

Mimi nitakueleza historia ya Waislam na elimu.

Baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alitangaza kupumzika siasa na kushugulika na elimu ya Waislam.

Akawa sasa katika taasisi yake Daawat Islamiyya kama kiongozi mkuu na akamteua Schneider Abdillah Plantan kuwa katibu wake.

Hawa wote wawili walikuwa mstari wa mbele katika TAA na TANU.

Mwaka wa 1962 ikaitishwa Muslim Congress ya Kwanza mkutano uliohudhuriwa na taasisi zote za Kiislam Tanganyika.

Agenda kuu ilikuwa kujenga shule za msingi na sekondari Tanganyika nzima kuwakwamua Waislam kutokana na kunyimwa elimu na wakoloni.

East African Muslim Welfare Society (EAMWS)chini ya Aga Khan kama Patron ikakabidhiwa kazi hii Tewa Said Tewa akiwa President wa taasisi hiyo kwa upande wa Tanganyika.

Shule zikaanza kujengwa na ikaamuliwa kijengwe Chuo Kikuu na kila kitu kikakamilika.

(Congress ya Pili 1963 ilikuwa ngumu sana.

Waislam walimsomea Rais Nyerere risala iliyoshutumu serikali yake kuwa inahujumu maendeleo ya Waislam).

Jiwe la msingi la Chuo Kikuu liliwekwa na Julius Nyerere akishuhudiwa na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Tewa Said Tewa na mabalozi wa nchi za Kiislam.

Ghafla ukazushwa mgogoro kuwa kuna Waislam hawamtaki Aga Khan kama kiongozi wa EAMWS na wanataka kujitoa.

Lakini ukweli ni kuwa kulikuwa na nguvu ndani ya serikali iliyotishika na maendeleo ya ujenzi wa shule na chuo kikuu.

EAMWS ikapigwa marufuku na serikali kuwa ni taasisi haramu na serikali ikawaundia Waislam BAKWATA na mali zote za EAMWS zikakabidhiwa kwa BAKWATA.

Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akakamatwa na kufukuzwa Tanganyika.

Hii ilikuwa mwaka wa 1968 na mipango yote ya elimu ikawa imekufa.

BAKWATA ikawa sasa inafanya kazi ya kuangalia kama idara ya serikali kuhakikisha kuwa Waislam hawanyanyuki kama walivyopigania uhuru wa Tanganyika.

Ilichukua zaidi ya miaka 30 ya mihangaiko kwa Waislam kuweza kujikusanya upya na kuanza shughuli zao za kujenga shule hata hivyo wakikabiliwa na vizingiti vingi kutoka serikalini.

Historia hii ni Part Three ya kitabu cha Sykes na sehemu hii nimeipa anuani, "Conspiracy Against Islam," yaani Njama Dhidi ya Uislam.

Hiki ni kisa kirefu na kipo katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Unashangaa hlo huku ukijisahaulisha wale wanaodai kumuimbia Yesu mpaka stend.
Na wle wafufua watu na ninyi wenzawazimu mkiamn upo we nguchiro????
Abu...
Usishambulie dini ya wengine.
Huu mjadala si wa nani dini yake ya haki.

Hapa tunaeleza dhulma dhidi ya Waislam.

Tafadhali acha kufanya hivyo utaharibu mjadala.

Mimi natukanwa lakini simjibu anaenitukana lakini najibu anaeniuliza maswali.

Hii ndiyo njia bora ya kueleza matatizo tuliyonayo.

Waliokuwa hawajui wanapata fursa ya kujifunza.
 
hata hivyo wakikabiliwa na vicinity vingi kutoka serikalini.
“Vicinity vingi kutoka serikali” ndiyo nini? Hicho kitabu uliandikiwa na ghost writer(s) kina Mlamali et al. maana inaonekana Kiingereza chako ni duni. Kwa Kiingereza chako, vicinity ni sawa na vizingiti?
 
Belo,
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimejadili tatizo la suala la ratio baina ya Waislam na Wakristo na nikaeleza kuwa ni suala lililogubikwa na unyeti mkubwa.

Kwa ajili hii mimi sipendi kuingia ndani ya gunia hili na kuanza kuchakura kwa kuwa tutafungua mlango wa mabishano yasiyo na maana yoyote.

Mimi nitakueleza historia ya Waislam na elimu.

Baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alitangaza kupumzika siasa na kushugulika na elimu ya Waislam.

Akawa sasa katika taasisi yake Daawat Islamiyya kama kiongozi mkuu na akamteua Schneider Abdillah Plantan kuwa katibu wake.

Hawa wote wawili walikuwa mstari wa mbele katika TAA na TANU.

Mwaka wa 1962 ikaitishwa Muslim Congress ya Kwanza mkutano uliohudhuriwa na taasisi zote za Kiislam Tanganyika.

Agenda kuu ilikuwa kujenga shule za msingi na sekondari Tanganyika nzima kuwakwamua Waislam kutokana na kunyimwa elimu na wakoloni.

East African Muslim Welfare Society (EAMWS)chini ya Aga Khan kama Patron ikakabidhiwa kazi hii Tewa Said Tewa akiwa President wa taasisi hiyo kwa upande wa Tanganyika.

Shule zikaanza kujengwa na ikaamuliwa kijengwe Chuo Kikuu na kila kitu kikakamilika.

(Congress ya Pili 1963 ilikuwa ngumu sana.

Waislam walimsomea Rais Nyerere risala iliyoshutumu serikali yake kuwa inahujumu maendeleo ya Waislam).

Jiwe la msingi la Chuo Kikuu liliwekwa na Julius Nyerere akishuhudiwa na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Tewa Said Tewa na mabalozi wa nchi za Kiislam.

Ghafla ukazushwa mgogoro kuwa kuna Waislam hawamtaki Aga Khan kama kiongozi wa EAMWS na wanataka kujitoa.

Lakini ukweli ni kuwa kulikuwa na nguvu ndani ya serikali iliyotishika na maendeleo ya ujenzi wa shule na chuo kikuu.

EAMWS ikapigwa marufuku na serikali kuwa ni taasisi haramu na serikali ikawaundia Waislam BAKWATA na mali zote za EAMWS zikakabidhiwa kwa BAKWATA.

Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akakamatwa na kufukuzwa Tanganyika.

Hii ilikuwa mwaka wa 1968 na mipango yote ya elimu ikawa imekufa.

BAKWATA ikawa sasa inafanya kazi ya kuangalia kama idara ya serikali kuhakikisha kuwa Waislam hawanyanyuki kama walivyopigania uhuru wa Tanganyika.

Ilichukua zaidi ya miaka 30 ya mihangaiko kwa Waislam kuweza kujikusanya upya na kuanza shughuli zao za kujenga shule hata hivyo wakikabiliwa na vicinity vingi kutoka serikalini.

Historia hii ni Part Three ya kitabu cha Sykes na sehemu hii nimeipa anuani, "Conspiracy Against Islam," yaani Njama Dhidi ya Uislam.

Hiki ni kisa kirefu na kipo katika kitabu cha Abdul Sykes.
Hizi hoja ulizozitoa tayari zimeleta mabishano yasiyo na maana na umekubali kukabiliana nayo kama huna factor ya kuverify hayo madai yako hayana msingi na watu wataendelea kukupinga mpaka utapoleta huo ushahidi .Najua hii hoja unaikwepa makusudi kwa sababu ndio itakayopangua hiyo hoja yako kuu

Unamanisha Waislamu walinyimwa elimu kuanzia enzi ya Wakoloni na sio enzi za Nyerere?

Hoja zako nyingi unazozitoa ni za miaka ya 60s ,karibia miaka 60 iliyopita baaada ya Nyerere,wamepita Mwinyi,Mkapa,Kikwete,Magufuli na sasa tuko na Samia wewe bado unamlalamikia Nyerere hebu tuambia hao wengine walivyowahujumu waislamu kwenye elimu
 
Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.

Utafiti wako uta-make sense pia ukiweka mchanganuo kama huo kwenye utawala wa Mwinyi,Mkapa , Jakaya na Samia
 
“Vicinity vingi kutoka serikali” ndiyo nini? Hicho kitabu uliandikiwa na ghost writer(s) kina Mlamali et al. maana inaonekana Kiingereza chako ni duni. Kwa Kiingereza chako, vicinity ni sawa na vizingiti?
Schmidt,
Neno nilokusudia ni "vizingiti" suggest imeweka "vicinity."

Nimesahihisha.

Kiingereza Cambridge 1970 Oral English Merit Pass.
 
Ila nachowapendea wakina sykes walikuwa wanakwenda na wakati walikuwa mbele ya muda,hata kula bata walikuwa wanakula
Mohamed Said

Ova
 
Et hawaombi pesa ,hzo kelele zao mwisho lazma waombe sadaka kwa ajili ya bwana.
Ndugu kama kuna wenye imani ya kizezeta basi ninyi.

Mana mpaka kuna wanaodai wanafufua wafu na mnawashangilia kweli ninyi ni zaid ya mazuzu
Hao unaowasema angalau hawaombi pesa ya kujenga shule. Wanaeneza Injili kwa staili wanayoijua wao. Halafu mnashangaa mpo wachache Serikalini
 
P1 Mkuu lkn yanakera sana haya
Abu...
Usishambulie dini ya wengine.
Huu mjadala si wa nani dini yake ya haki.

Hapa tunaeleza dhulma dhidi ya Waislam.

Tafadhali acha kufanya hivyo utaharibu mjadala.

Mimi natukanwa lakini simjibu anaenitukana lakini najibu anaeniuliza maswali.

Hii ndiyo njia bora ya kueleza matatizo tuliyonayo.

Waliokuwa hawajui wanapata fursa ya kujifunza.
 
Unaweza kutupa ratio ya Wakristu kwa Waislamu kwenye population ya Tanzania?

Wakristu wamejitahidi sana kuwekeza kwenye elimu kuanzia level ya chini na kuendelea tofauti na Waislamu ambao wameweka msisitizo kwenye elimu ya dini
Hakuna kitu kinaitwa wakristu au waislamu wote ni watanzania.. dini ni utapeli
 
Abu...
Usishambulie dini ya wengine.
Huu mjadala si wa nani dini yake ya haki.

Hapa tunaeleza dhulma dhidi ya Waislam.

Tafadhali acha kufanya hivyo utaharibu mjadala.

Mimi natukanwa lakini simjibu anaenitukana lakini najibu anaeniuliza maswali.

Hii ndiyo njia bora ya kueleza matatizo tuliyonayo.

Waliokuwa hawajui wanapata fursa ya kujifunza.
Mzee kwani kipimo cha mtanzania ni dini au utanzania na uafrika wake?
 
Hao unaowasema angalau hawaombi pesa ya kujenga shule. Wanaeneza Injili kwa staili wanayoijua wao. Halafu mnashangaa mpo wachache Serikalini
Kwanza unafikiri wakina sykes walikuwa wafia dini wao tena walikua na umaghsribi zaidi
Sema mzee wetu Mohamed Said anawapelrka huko zaidi

Hilo ni wazi ndiyo maana waling'ang'ania majina ya Kizungu waliyobatizwa na Wajerumani hadi la ukoo. Huyu mzee MS kazi kujipendekeza kwa Sykes, ilhali atimize ajenda zake za udini kupitia mgongo wa Sykes.
 
Et hawaombi pesa ,hzo kelele zao mwisho lazma waombe sadaka kwa ajili ya bwana.
Ndugu kama kuna wenye imani ya kizezeta basi ninyi.

Mana mpaka kuna wanaodai wanafufua wafu na mnawashangilia kweli ninyi ni zaid ya mazuzu
Wee mtembeza bakuli kwenye mabaa na kanzu lako ili mjenge madrasa tulia dawa ikuingie vizuri. Halafu muulize Maalim wako MS jee kwa Kiingereza, "vizingiti" ndiyo inaitwa "vicinity"? Miaka 30 ya mabadiliko ya kiuchumi, kielimu, kitekonlojia, kisisasa, na tawala za Marais wa imani, yeye bado kabaki na hoja zake zilezile za vitabuni za tokea enzi za kudai Uhuru.
 
Back
Top Bottom