Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
Belo,Hizi hoja ulizozitoa tayari zimeleta mabishano yasiyo na maana na umekubali kukabiliana nayo kama huna factor ya kuverify hayo madai yako hayana msingi na watu wataendelea kukupinga mpaka utapoleta huo ushahidi .Najua hii hoja unaikwepa makusudi kwa sababu ndio itakayopangua hiyo hoja yako kuu
Unamanisha Waislamu walinyimwa elimu kuanzia enzi ya Wakoloni na sio enzi za Nyerere?
Hoja zako nyingi unazozitoa ni za miaka ya 60s ,karibia miaka 60 iliyopita baaada ya Nyerere,wamepita Mwinyi,Mkapa,Kikwete,Magufuli na sasa tuko na Samia wewe bado unamlalamikia Nyerere hebu tuambia hao wengine walivyowahujumu waislamu kwenye elimu
Baada ya kuhujumiwa EAMWS mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu na ujenzi wa shule ukafa.
Hapa sasa kuna historia ya yale yaliyokuwa yakifanyika ndani ya Wizara ya Elimu.
Wizara hii ilikuwa mfano wa kigango na kulikuwa na mpango maalum wa kupitisha wanafunzi kuingia sekondari na vyuo vya elimu ya juu.
Waislam walikuwa hawazidi 10% na miaka yote ya utawala wa Nyerere Waziri wa Elimu ilikuwa lazima awe Mkristo.
Mawaziri 8 waliopita katika Wizara hii wote walikuwa Wakristo.
Mwaka wa 1987 Prof. Malima ndiye akajakuwa Waziri wa kwanza wa Elimu Muislam na aliyoyakuta hapo yalimshtua na akaandika barua ya siri kumweleza Rais Ali Hassan Mwinyi yale yaliyopo hapo wizarani.
Hii barua iliibiwa na kuvujishwa kwingi kwa watendaji wa serikali na kwa vyombo vya habari.
Prof. Malima alieleza mpango uliodumu kwa muda mrefu ambao ulikuwa unadumaza vijana wa Kiislam katika kupata elimu ya juu.
Katika watu walioipata taarifa hii ni Rais Mstaafu Julius Nyerere wakati ule akiwa Mwenyekiti wa CCM.
Prof. Malima akawateua Waislam 4 kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali.
Katika hawa wakurugenzi alikuwa kijana mmoja kutoka Moshi jina lake Kenya Abdallah Hassan.
Balaa lake lilikuwa kubwa sana.
Tuishe hapo tusonge mbele.
Lakini huko nyuma katika miaka ya 1970 OIC walitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania.
Serikali ilikataa kutoka kibali na chuo kikajengwa Mbale Uganda.
Katika miaka ya 80 vijana wa Warsha walijipenyeza BAKWATA kwa nia ya kuboresha elimu ya Waislam na vijana hao wakabadilisha shule za BAKWATA 4 walizozirithi kutoka EAMWS kuwa seminari.
Shule hizi zikaanza kufanya vizuri.
Serikali iliingilia kati na wale vijana wakaondolewa katika uongozi wa BAKWATA na kupigwa marufuku kutoendesha taasisi yoyote ya Kiislam Tanzania.
Hawa vijana hawakukubali kushindwa wakajenga shule inaitwa Masjid Quba.
Serikali ikakataa kuisajili lakini hawa vijana wakaendelea kusomesha bila tasjila hadi Prof. Malima alipokuwa Waziri wa Elimu alipoipa tasjila.
Yapo mengi, mengi sana haiwezekani yote kuelezwa hapa.