Mohamed Said ana siasa za kulialia


Kwani ilikuwaje swali hili wakristo wakalikimbia kwenye sensa Na ilhali wao ndio wakilipigia njuga
 
Belo.
Umepatapo kujiuliza kwa nini mimi nimeweka jina langu hapa naandika bila kujificha?
Umepatapo kujiuliza swali hili?

Umepatapo pia kujiuliza kwa nini wewe unajificha?
Unaogopa.

Huko kujificha na uoga ndiyo kunakoleta ujasiri wa kukebehi, kukejeli na kutukana.

Nini kinakutisha?

Sababu ya mimi kujiweka wazi ni kutaka niaminike kwa ukweli wa kile ninachosema.
Ikiwa kuna mtu anataka kunihoji isiwe tabu kwake kunipata tukazungumza uso kwa uso.

Nimeandika mambo mazito ambayo wengine wangeogopa kusema ingawa yamesimama kwenye ukweli.

Nini ninachotaka kufanikisha?

Ninachotaka kufanikisha ni watu wajue kuwa tunalo tatizo na lazima litatuliwe hivi sasa tusije kushtuka kutaka kutafuta sulhu mambo yameshaharibika.

Ninapoandika na kueleza matatizo haya wale ambao walikuwa hawajui wanakuwa wanajua kuwa ala kumbe nchi yetu kuna hili na hili.

Nimekutana na watu wengi na wananiambia hawakuwa wanajua jambo kadha wa kadha.
Suala la 20:80 na Viongozi wa Vyuo Vikuu limewashtua wengi sana tena sana.

Huwezi kusimama kupigania haki ikiwa hao wenye kudhulumiwa hawajui kama ipo dhulma.

Inataka kwanza wajue kuwa ipo dhulma na hao wenye kudhulumu wajue pia kuwa kuna lawama na dhima juu ya vichwa vyao na jamii wanawataka wakomeshe hiyo dhulma.

Dhulma ikishawekwa wazi na jamii wakaijua kawaida ni kuwa watataka ikomeshwe kwani hakuna asiyejua kuwa dhulma ikiachiwa iendelee huangamiza.

Jamii ikisimama pamoja kuondoa dhulma hapana shaka itaondoka.

Hii ndiyo sababu mimi hapa nakwepa mabishano yasiyo na tija nimejikita katika kusomesha na kuelimisha ili watu wajue kile ambacho walikuwa hawakijui.

Mambo haya yanataka subra kwani si kazi nyepesi.

Sasa Bwana Belo ikiwa wewe hili jambo la ''ratio,'' ni muhimu sana kwako ninakuwekea rejea usome utajua na rejea hizi zote zipo katika kitabu cha Abdul Sykes (1998):
  1. August H. Nimtz Jr, Islam and Politics in East Africa, University of Miannapolis, 1980, p.11.
  2. Family Mirror, Second Issue, November, 1994, p. 6.
  3. Ali A. Mazrui, ‘African Islam and Competitive Religion: Between Revivalism and Expansion,'' in Third World Quarterly Vol. 10. No. 2 April, 1988, pp. 499-518.
  4. Africa South of The Sahara, Europa Publication, London, No. 20, 1991, p. 1027.
 
Wapigania uhuru walishakufa, sasa hivi tunapigania umoja na uchumi. Historia zinazoturudisha nyuma kutugawa na kutuchochea hazina nafasi nyakati hizi
 
Wapigania uhuru walishakufa, sasa hivi tunapigania umoja na uchumi. Historia zinazoturudisha nyuma kutugawa na kutuchochea hazina nafasi nyakati hizi
Lupweko,
Umoja hutoweza kuupata penye dhulma.
Dhulma ndiyo hugawa umma ukawa mapande mawili yaliyohasimiana.

Haki hujenga mapenzi na kuwaleta watu pamoja.
 
Lupweko,
Umoja hutoweza kuupata penye dhulma.
Hayo ni mawazo yako. Mimi maeneo mengi tu nimeishi na kufanya kazi na watu wa makabila na dini tofauti, wala hawana hisia za kudhulumiwa kitabaka. Sana sana watu wanapambana na kupata uchumi
 
Lupweko,
Umoja hutoweza kuupata penye dhulma.
Dhulma ndiyo hugawa umma ukawa mapande mawili yaliyohasimiana.

Haki hujenga mapenzi na kuwaleta watu pamoja.
Huko libya na irak, pakistan na afghanistan dhulma ilikuwa ni ya nini wakati kote huko ni Mafirauni ninyi watupu.
Mbona mnauana wenyewe
 
Ukikuwa utaacha,hzo nchi zilifika hapo zilipofka kwa chuki za makafiri
Huko libya na irak, pakistan na afghanistan dhulma ilikuwa ni ya nini wakati kote huko ni Mafirauni ninyi watupu.
Mbona mnauana wenyewe
 
Hayo ni mawazo yako. Mimi maeneo mengi tu nimeishi na kufanya kazi na watu wa makabila na dini tofauti, wala hawana hisia za kudhulumiwa kitabaka. Sana sana watu wanapambana na kupata uchumi
Lupweko,
Hilo haliwezekani kabisa kuwa pawe na dhulma kisha pawe na amani,
Soma historia ya dunia pote.

Wala haya si mawazo yangu.
Ukipenda naweza kukupa rejea kutoka kwingi duniani.

Tuanze na hapa nyumbani Afrika ya Mashariki.

Kwa nini Wakikuyu Kenya walinyanyua silaha kupitia Mau Mau dhidi ya Waingereza?

Kwa nini babu zetu walinyanyua silaha kupitia Maji Maji dhidi ya Wajerumani?

Usiseme jambo kwa matamanio ya nafsi yako.

Ziko sheria zinazoongoza dunia.

Hakuna binadamu anaekubali kudhulumiwa.

Nifahamishe hayo maeneo ulioishi kuna dhulma na watu wameikubali dhulma.

Labda hakuna dhulma katika hiyo jamii au wanaodhulumiwa hawajui kama wanadhulumiwa kwani kama anaedhulumiwa hajui kuwa anadhulumiwa hiyo dhulma haipo au ametezwa nguvu anaogopa kudai haki yake akihofia usalama wa nafsi yake.

Mimi ni mwanahistoria ningependa kusoma hii elimu mpya kutoka kwako.

Mimi si mdogo katika kusafiri dunia hii tutaelimishana.

Hilo la uchumi halitegemei chochote pawepo dhulma pawepo haki watu lazima wahangaikie maisha.

Wengi hudhani tunajua kumbe hatujui na matokeo yake ndiyo haya tunakuja na sheria ambazo hazipo katika ulimwengu kwani ukipigwa lazima utahisi maumivu na ikiwa unapigwa huhisi uchungu basi lipo tatizo kubwa kwa apigwae.

Hizi ndizo sheria za dunia na hazina wasiwasi wowote ingawa huwa kunatokea vitu vinaitwa ''syndrome,'' ambavyo vinakwenda kinyume na ''logic,'' yaani mantiki.

Hii ni elimu mpya sana ya miaka ya hivi karibuni.

Anaeteswa anamtetea anaemtesa.
Anaedhulumiwa anampenda dhalim anaemdhulumu.

Ikitokea hali kama hii wanaingia madaktari wa akili kutafuta tatizo liko wapi.

Karibu tutaeleweshana.
 
Kwa nini Wakikuyu Kenya walinyanyua silaha kupitia Mau Mau dhidi ya Waingereza?
.....
Hakuna binadamu anaekubali kudhulumiwa.
Na mimi nikuulize; kwa nini waisilamu nchini hawajanyanyua silaha dhidi ya 'dhuluma'?
 
Mzee wangu Mohamed Said,
Awali ya yote nakupongeza kwa kutupa elimu hii.Nina mambo nataka kujuzwa kidogo,

1. Unaweza kutujuza Barua hii ya Prof. Malima kwa aliekuwa rais wa wakati ule ilikuwa ikieleza nini zaidi?Nashangazwa vipi barua ya siri ivuje?

2.Natamani nijue zaidi kuhusu Mr Kenya Abdallah Hassan, ni nani hasa, nini alifanya?Na vipi harakati zake na mwisho wake ulikuwaje?

Shukran.
 
Na mimi nikuulize; kwa nini waisilamu nchini hawajanyanyua silaha dhidi ya 'dhuluma'?
Na mimi nikuulize; kwa nini waisilamu nchini hawajanyanyua silaha dhidi ya 'dhuluma'?
Lupweko,
Vita Vya Maji Maji iliwafunza wazee wetu kuwa hawawezi kunyanyua silaha dhidi ya silaha za Wajerumani wakapata ushindi.

Walipoingia Waingereza utawala wao ulikuwa wa ''kistaarabu,'' kuliko wa Wajerumani.

Waingereza walijifunza kutoka kwa yale yaliyowafika Wajerumani kutoka kwa babu zetu kwa hiyo wao walianzisha, ''Indirect Rule,'' na hii iliwasaidia sana katika kuitawala Tanganyika.

1929 wazee wetu wakaasisi African Association na hii ndiyo ikaja kuzaa TANU.
Hapakuwa na haja ya kunyanyua silaha uhuru ukapatikana kwa amani bila ya kumwaga damu.

Lakini uhuru ukaja na changamoto ambazo waasisi wa harakati hizi za kuwaleta watu pamoja kujenga umoja na kudai haki hawakutegemea zitatokea.

Dunia hii ya leo ukiwa na madai yoyote njia inayokubalika ni mazungumzo si kunyanyua silaha kwani matumizi ya nguvu hasara yake ni kubwa kuliko hayo manufaa yanayotafutwa.

Mifano Afrika ipo mingi.

Nchi nyingi zilizonyanyua silaha mwishowe ziliishia katika mazungumzo yaani, ''dialogue,'' na kuulizana kwa nini hatukuzungumza tokea mwanzo tulipoliona tatizo?
 
Makao...
Barua ya Prof. Malima ilieleza dhulma iliyokuwa ikifanyika katika Wizara ya Elimu.

Unashangaa barua ya siri wizarani kuvuja?

Yapo makubwa yalikuwa yakifanyika katika ofisi kubwa kuliko ya Prof. Malima.

Kenya Abdalah Hassan aliweka uadilifu yale yaliyokuwa yakifanyika wakati ''wenyewe'' wameshika nafasi hayakuwezekana kufanyika tena.

Kenya aliendelea na kazi hadi akastaafu.

Ingia hapo chini soma:


 

Sijui neno ubishi kwa tafsiri yako linamaana gani lakini maswali niliyouliza yalihitaji ufafanuzi unajisifu unasomesha huku unatumia maneno ya kejeli? Nimeuliza ww unatumia utaalamu gani kutambua dini za watu!?
 
Sijui neno ubishi kwa tafsiri yako linamaana gani lakini maswali niliyouliza yalihitaji ufafanuzi unajisifu unasomesha huku unatumia maneno ya kejeli? Nimeuliza ww unatumia utaalamu gani kutambua dini za watu!?
The Phy...
Umeuliza swali na nimekujibu swali na kukupa nyongeza ambayo naamini hukuitegemea na hii imewashtua wengi viongozi katika vyuo vikuu.

Unaniuliza imani za hawa ambazo majina na picha zao ziko hapo kuwa nawatambuaje?
Sasa hapa anaefanya mzaha, kejeli na kebehi nani, mimi au wewe?

Pima kina cha maji.

Huoni jinsi ukumbi ulivyokuwa kimya kwa hii nyongeza niliyokutunuku wewe ili ujue ukweli na kile ambacho Waislam tunakieleza?

Unadhani mimi niko hapa kutaniana na wewe?
Wenzako wengi wako kimya.

Jiulize kwa nini?

Unapodhihiri ukweli uongo ni wenye kutoweka.
Kaa kimya subiri serikali itoe jibu iwe leo au hata baada ya miaka 100.
 
Hiki kigezo unachotumia kubainisha dini za watu hakina uhalisia kwani wewe unaamini kwamba kila Mohamed lazima awe muisilamu au jina ndio linaamua dini ya mtu!? Mbona tuna watanzania wengi tu wanatumia majina yanayonasibishwa na imani fulani wakati sio!? Kwa nini utumie kigezo cha kudhaniwa kuhalalisha madai?
Unadhani kwa nini Nyerere alisema mkitaka kujua mko wangapi mkahesabiane huko mnakoabudu!?
 
The Phy...
Nimefurahi kufanya mjadala na wewe.
 
Udini umempofusha Karani mstaafu wa Bandari ya Tanga Mzee MS. Wenzake wapo dynamic wanasaka hela, yeye yupo static na hoja zake za udini.
Hivi kumbe alikuwa karani wa bandari? Pamoja na masters yake ya UK?
 
Mzee kilizi huwezii shindana na nguvua ukristo sio Tanzania wala duniani utaishia kulialia tu humu jf na tu vitabu vyako uchwara ambavyo haviwezi tumika popote..unatakufa kwa mawazo na stress hii vita na ngumu kwako..huwezi badili historia iliyokuwepo..kwa kulazimisha illusion zako..

Huu muda tumia kulea wajukuu na kuandaa mwisho mwema.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…