Mohammed Dewji: Mchakato wa mabadiliko Simba umekamilika, aweka bilioni 20

Mohammed Dewji: Mchakato wa mabadiliko Simba umekamilika, aweka bilioni 20

Hata hizo bilioni 20 ni ndogo kwa hisa za 49%,Mkitaka kulijua hilo subirini mchakato wa yanga utakapo kamilika ndo utajua hujui
Hata kama ndogo huyo mwenye nyingi zaidi ya hizo yuko wapi? Mfano wewe unaishi kwa shemeji yako unalala sebleni sasa ukiambiwa utoe hata 1m tu huna
 
Hawa uto huwa hawakosi kisingizio.... Wanaamini GSM wa aweka pesa nyingi kuliko Mo. Haya mo katumia 21.4 billion kwa miaka 4. Hao gsm waseme walizot

Wamuulize GSM kwao kashatumia ngapi na ameingiza ngapi
Kwa akili yako unaamini SIMBA IMETUMIA BIL 21 KWA MIAKA MINNE?? Umewahi kuona financial statements za SIMBA??
 
Hata kama ndogo huyo mwenye nyingi zaidi ya hizo yuko wapi? Mfano wewe unaishi kwa shemeji yako unalala sebleni sasa ukiambiwa utoe hata 1m tu huna
Hahaha, subiri uwekezaji wa timu ya wananchi mkuu ndo utajionea
 
Jiongezeni nyie Mbumbumbu,kama katumia 21Bl kwa miaka 4,je hizo 20Bl atatumia kwa miaka mingapi,then baada ya hapo itakuwaje. Na pia mbona hatoi Balance Sheet kwa hizo 21Bl jinsi zilivyotumika ikiwemo faida na hasara plus madeni.
Hayo yote yanakuhusu nini ewe kapuku mwenzangu? Washabiki tunataka makombe tu
 
Hesabu Nyepesi.. Hisa ni vipande ambavyo vina thamani sawa.

49%= 20B
51%= ?
?= (51X20)/49 = 20.8 B

Kwa hiyo thamani ya Simba Sc ni 40.8 B??????? .... Serious
Soma: Klabu ya Yanga imeingia Mkataba wa miaka 10 na Azam Media wa haki za matangazo za Klabu kupitia Yanga TV wenye thamani ya Bilioni 41.64

Thamani ya MKATABA WA KUNUNUA Simba maisha inapitwa na thamani ya Mkataba wa Yanga TV (Miaka kumi)
Zero brain mwingine huyu
 
Mbumbumbu fc katika ubora wenu, ebu Legeza misuli ya kichwa chako, hiyo thamani ya Bilion 20 ilikuwa ni miaka minne ijayo, now thamani imepanda na hii madhara yake sio leo mbumbumbu nyie
Miaka mi4 ijayo?
 
Klabu inajipandisha yenyewe thamani mkuu, Ushawahi kujiuliza kwann alipoichukua African lyon na pesa zake zote ila alishindwa kuipandisha thamani hiyo timu hahhahaah mbumbumbu katika ubora wenu
Ingekuwa ndio hivyo yanga msingetembeza bakuli, au thamani yenu ilikuwa haipandi? Ndio maana uwezo wa yanga ni kubeba mapinduzi cup tu
 
Ivi mikataba ya udhamini kati ya Simba na makampuni ya Mo ikoje au ndio anapitia mulemule kwenye uwekezaji
 
Mchakato wa mabadiliko Simba umekamilika- Mo - "Time ya Ushindani (FCC) imeshatupa ruhusa, hivyo mchakato wa mabadiliko ya Simba umekamilika, tumepewa vipengele vichache vya kufanyia kazi kama kutoa fedha," - Mohammed Dewji.

====

MWENYEKITI wa Bodi ya wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji "Mo Dewji' leo Ijumaa Julai 30, 2021 amekabidhi kitita cha Sh20 Bilion za uwekezaji wa Simba.

Amesema hanunui hisa asilimia 49 kwa pesa hiyo bali 43 Bilioni.

"Mpaka sasa nimeshalipa Simba zaidi ya Sh21 Bilioni, ukiachana na pesa nyingine za ziada za maandalizi ya msimu, usajili na nyinginezo ninazotoa”

"Mimi nimetoa jasho na machozi kwenye Simba, nimetoa muda mwingi kwa ajili ya Simba, nimepoteza fursa nyingi kwenye biashara zangu kwa ajili ya Simba."

"Sisi tumewekeza na hawezi kutokea mtu akatupa hela ya udhamini, sawa sawa na wenzangu, hili sitakubali. "

"Hakuna mtu mkubwa kuliko Simba, hii timu tumeikuta na tutaiacha, hata mimi nimeikuta."

Lakini kuna watu wanasema Mohammed Dewji hana pesa, leo hii nakabidhi cheki ya Sh 20 Bilioni," amesema.

Alitania kwamba kama akisema pesa hiyo Bilioni 20 tayari ameshaipa Simba na wamemalizana kwenye zile Bilioni 21. Mohammed Dewji amekabidhi kitita cha Sh 20 Bilion za uwekezaji wa Simba.

View attachment 1873903

=========

Ni wakati sasa wa Simba kugomea Bilioni 20 za Mo na kutaka Thamani ya Klabu iongezwe au kama kuna mwenye Mzigo zaidi Aje.

Anaonekana wzi anagomea wadhamini wengine, kiuhalisia thamani ya simba imepanda. Kama Yanga TV tu ni zaidi ya hizo Bilioni 20 tena kwa miaka kumi vipi kuhusu Brand ya Simba?

Kwa maelezo yake Bil 21 ametumia kwa miaka 4 , mbona hasemi faida aliyopata? . Kama ametumia kwa miaka 4 bil 21 , maana yake hizi 20 zitaisha baada ya Miaka 4 tena!.. Then whats next ataendelea kutoa hisani ya fedha zake? au ataanza kula matunda ya uwekezaji wake?

Anasema ahanunui hisa kwa 20B bali ni 43B, Ipo kwenye mkataba?. Je hizo alizokuwa anatoa kumbe alikuwa anazihesabu. Je zijazo atatoa au atawaambia watumie hizo 20B alizowapa?

Kwa nini Valuation ya Hisa imefanywa kiholela, Na kwa nini hakuna wawekezaji wengine waliojitokeza kupambana kwenye kupata hiyo Dili ya uwekezaji?

Ni strategy za kibiashara ambazo zitaiwezesha Simba kujiendesha na kutengeneza faida toka hizo B20 SABABU hata Mo mwenyewe anaonekana KUPOTEZA PESA katika huo udhamini kwa madai yake.

Kumbuka huu ni mchakato wa Mabadiliko ya uendeshaji wa timu, siyo mchakato wa kumpa Mo Timu. Hii Press ni ya kibabe sana. Inaonekana Simba OG ni kama wamenyongea na wanaendeshwa tu.

KWENYE MAJUKWAA NA USHABIKI SIMBA ISHANGILIE USHINDI KUWAJIBU YANGA KWA HILI
KIBIASHARA NA KIMKAKATI SIMBA IMEPIGWA KWEUPE.

Ifikirie Mwaka 2035 Bado familia ya Mo itakuwa inaimiliki hii klabu kwa 49% hata kama Mo atakuwa hayupo hai. Hizo 20B zitakuwa zimeyeyuka kitambo sana. Naiona Simba na Mo Family wakiburuzana kortini baadaye.
Itakuwa kesi ya: Tuachieni Timu yetu Vs Turudishieni Pesa zetu 49%
Hivi unaelewa nini maana ya pesa? Muda mwingine ni bora kunyamaza, tafuta uelewa kidogo, emu uliza watu wanaojua business haswa, msikurupuke ndugu mtakuja kupata aibu kama ,umepata uelewa juu ya mkataba wa yanga na Adam? Kijana soma utapata aibu kama hizi hadi lini,!! Jaribu kuuliza usiwe mjuaji
 
Yaani MO kaokota dodo Simba, Kwasasa Kama kaweka 20b Ina maana waki iingia mkataba na Azam au mdhamini yoyote ana haki ya kugawana kinacho ingia na Klabu ya Simba.

Ndio maana aligomea mkataba wa Azam ili avute muda kwakua alikua hajaweka mzigo 20 b ingekua ngumu yeye kugawana faida ya udhamin wa Azam na Klabu ya Simba.

Maana wenye akili wange piga kelele.
Yeye anachomiliki Ni 49% ya share, Atakachokipata Ni dividend ya hizo hisa. Hatakama Azam watatoa 100billion kwa kupata dili ya Simba tv haimanishi mo ndo anapewa 49% yahio pesa. Mambo yahisa namgawanyo wa dividend nimagum kias kma hunakichwa kizuri chahesabu.

Mkuu mim nimaskin kma ningekua nahela nisingebaki nyuma kwenye ununuzi wahisa za club ya Simba, Kuna kila dalili kwa uwepo wa moo kwenye club nakuwekeza hizo 20 billion huku akiwa yeye ndio major shareholder itaipaisha demand ya share zake nakuifanya thamani yake kua kubwa zaid. Hawajamaa wanaenda kufanya mapinduzi kakubwa
 
MO amewahi kuziweka bilioni 20 mapema kwasababu tulikuwa na mpango wa kuchukua Bilion 20 za Azam tuje kuinunua simba kwanza, bahati yake kawahi kabla

Tazama huyu Bogus yani ni Kiazi Mviringo kabisa 😂😂😂😂
Hivi Nugaz ndiyo kawaambia hizo 41B mutapewa zote kwa pamoja?

Lile Genge la Jangwani sio siri ni la kupelekwa Mirembe lote tukianza na Bumbuli 😂😂😂
 
Tazama huyu Bogus yani ni Kiazi Mviringo kabisa 😂😂😂😂
Hivi Nugaz ndiyo kawaambia hizo 41B mutapewa zote kwa pamoja?

Lile Genge la Jangwani sio siri ni la kupelekwa Mirembe lote tukianza na Bumbuli 😂😂😂
Just sell media right for more than 40 billions in 10 years only

But Mbumbumbu sale their whole club in life time for 20 billions! That's joke
 
Back
Top Bottom