Mohammed Shabiby: Namna ya kupunguza bei za mafuta kwa 50% ya bei za sasa

Mohammed Shabiby: Namna ya kupunguza bei za mafuta kwa 50% ya bei za sasa

Kama serikali inaakili huo ndio ushauri wa kufuata ili kushusha bei ya mafuta.
 
Matrekta ya "URSUS" yanatoka Poland. Dili lake lilisukwa tangu enzi za waziri mmoja wa kilimo anaefanana na Tyson. Nchi hii ni kama shamba la bibi, Kila awamu inakuja na upigaji wake.
Hizo trekta ni janga la dunia
 

Shabiby atoa mwarobaini kupanda bei mafuta​


MBUNGE wa Gairo Mohammed Shabib ameitaka Serikali kuruhusu kampuni binafsi kuagiza mafuta wenyewe bila kutumia uagizaji wa pamoja.

Shabiby ametoa ushauri huo leo Jumatano tarehe 6 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema mfumo wa uagizaji wa pamoja unafanya kutokuwepo kwa ushindani wa bei na hivyo bei inapopanda kwenye soko ambalo mafuta yanaagizwa kunakuwa hakuna mbadala.

“Leo hii mkiruhusu kampuni binafsi ziagize mafuta na kama mtu anaona kuna unafuu kwenye uagizaji wa pamoja afanye hivyo na kama ataona haina unafuu alete yeye,” amesema.

Ameongeza kuwa zimekuwa zikitolewa hoja za upotoshaji kwamba uagizaji wa mtu mmoja mmoja unasabisha ukwepaji wa ushuru.

“Meli zote zinashusha kwenye mita wanakwepaje ushuru? Hii kazi waachieni TRA utasikia TRA wanakula dili lakini ukiangalia tangu huu mfumo wa uagizaji wa pamoja mita imekufa mara nyingi kuliko kipindi cha uagizaji binafsi,” amesema.

“Naombeni sana turuhusu hayo na bei ya mafuta itashuka kuliko tulivyotarajia na wala tusidanganyane watu kwamba Serikali inaweza kutoa kodi kwenye mafuta, haiwezekani kodi ndiyo inayolipa mishahara na kununua madawa,” amesema Shabiby.
View attachment 2178669
tangu huu mfumo wa uagizaji wa pamoja mita imekufa mara nyingi kuliko kipindi cha uagizaji binafsi[emoji848][emoji2827]
 
Bulk procurement faida yake ninayoiona ni control ya kodi.

Ila faida ya kuacha watu waagize wenyewe ni ushindani wa bei hapa ananufaika mlaji wa mwisho.

Sasa ni jambo la kuchagua kati ya hayo mawili.

Kodi kwa serikali au faida ya soko huria.
Kinachoshindikana ku control kodi katika uagizaji huria wa mafuta ni nini? Na je huko katika bulk procurement una uhakika kodi inalipwa kwa 100% maana bei inapangwa na wachache kwahiyo nachoona mzigo anabebeshwa mtumiaji wa mwisho wachache wanatafuna karamu ya bwana.
 

Nishati na mafuta Makamba, ardhi na makazi Riziwani Kikwete, ujenzi na miundombinu mbarawa ( visiwani) jifunzeni kitu​

Kwaiyo hizo wizara wangewekwa wakristo hapo ingekuwa sawa, au wangewekwa wasukuma wenzio is okay?! Nyie mb..wa mna matatizo sana
 
Mkuu si mara zote kukosea ni uongo one can be honestly wrong. Kumbandika label ya uongo simply tu kwakuwa kamwita Ahmed kuwa Muddy is quite unfair at least kwa opinion yangu.
Hata mimi nimemshangaa sana mjumbe mwenzetu wa baraza hili notkel

After all, hata kama kuna "slight error" kwenye uandishi wa jina la mbunge mtoa maoni, mwandishi kaambatanisha na video clip ya mhusika..

Lakini cha ajabu jamaa bado akamwita mwenzake MWONGO kwa herufi kubwa!!
kababu
 
Nionyeshe hapo kwenye kushuka bei kwa 50% mimi sijapaona nadhani miwani yangu ina tatizo
Hata ikiwa chini ya 50% kidogo siyo mbaya mradi yashuke hata kwa 40% inatosha. Muhimu ushauri uangaliwe kama unafaa.
 
Ameongea point sana aisee... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
... hao wahuni watatengeneza cartel; wata-collude kuwaumiza wananchi. Sidhani kama huo ushauri una msaada wowote maana siku za nyuma ilikuwa hivyo "wakashindikana" ndipo serikali ikaja na wazo la bulk procurement kujaribu kuondoa tatizo. Asitake kuturudisha kule.
Mawazo ya serikali kutufanyia vitu kama hivyo ni wizi wa mchana.
 
Back
Top Bottom