The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Nchi gani kubwa hizo zinazopata taabu na suala la mafuta?Huu ushauri ni mzuri lkn suala la mafuta hata nchi kubwa zinapata taabu je nao wanauziwa na bandari yetu au
Na nini hasa maana ya "nchi kubwa" na "nchi ndogo?" na uhusiano wake na hiki tunachojadili hapa?
Kuna nchi kama Luxembourg, Israel, Quatar, Austria nk ni nchi dogo sana lakini ni nchi zenye chumi imara na nchi zenye maisha nafuu sana kwa wananchi wao..!
Na kwa taarifa yako mambo haya hayako hivyo unavyofikiri..
Haya mambo ya uendeshaji wa uchumi wa nchi kwa manufaa nafuu ya maisha kwa wananchi ni suala la SERA na MIPANGO BORA..
Huwezi kuwa na mipango na sera bora bila kuwa na MFUMO BORA wa UTAWALA unaozalisha VIONGOZI BORA wenye kutumia bongo zao vizuri na wasio WABINAFSI (Selfish)..
Tatizo la nchi yetu ya Tanzania wala hata haliko huko unakofikiri wewe..
Tatizo liko kwenye ubinafsi wa viongozi wetu. Na viongozi hawa hutumia matatizo kama haya kujinufaisha kisiasa kwa gharama ya wananchi..!!