Mohammed Shabiby: Namna ya kupunguza bei za mafuta kwa 50% ya bei za sasa

Mohammed Shabiby: Namna ya kupunguza bei za mafuta kwa 50% ya bei za sasa

We ndo mpuuzi kiazi mviringo maana uanjua kila kitu jpm ndo ameazisha
Mfumo umeanza 2011
Na wakati unaanza watu wengi waliandika na kufanya research ya kuonyesha madhara yake. Ila huenda kulikua na maslahi Kama alivyosema shabiby
Screenshot_20220407-145107_1.jpg
Screenshot_20220407-145219_1.jpg
 
Tatizo biashara ya mafuta inashikiliwa na wanasiasa walafi ambao ndio wanaotoa maamuzi kwa maslahi yao binafsi. Kuna haja ya kufanya mapinduzi ya kuokoa nchi kutoka mikononi manyang'au yalinayohodhi madaraka
Ndio tatizi lililopo hili,kila sekta hawa watu wamejiingiza na ndio maana vyombo vingine vya mamlkaka havina nguvu juu ya usimamiaji wa sera na sheria zake, utasikia aah hapa kuna mkono wa mkubwa hivyo ni ngumu kulisimamia.
 
Shabiby atoa mwarobaini kupanda bei mafuta​

MBUNGE wa Gairo Mohammed Shabib ameitaka Serikali kuruhusu kampuni binafsi kuagiza mafuta wenyewe bila kutumia uagizaji wa pamoja.

Shabiby ametoa ushauri huo leo Jumatano tarehe 6 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema mfumo wa uagizaji wa pamoja unafanya kutokuwepo kwa ushindani wa bei na hivyo bei inapopanda kwenye soko ambalo mafuta yanaagizwa kunakuwa hakuna mbadala.

“Leo hii mkiruhusu kampuni binafsi ziagize mafuta na kama mtu anaona kuna unafuu kwenye uagizaji wa pamoja afanye hivyo na kama ataona haina unafuu alete yeye,” amesema.

Ameongeza kuwa zimekuwa zikitolewa hoja za upotoshaji kwamba uagizaji wa mtu mmoja mmoja unasabisha ukwepaji wa ushuru.

“Meli zote zinashusha kwenye mita wanakwepaje ushuru? Hii kazi waachieni TRA utasikia TRA wanakula dili lakini ukiangalia tangu huu mfumo wa uagizaji wa pamoja mita imekufa mara nyingi kuliko kipindi cha uagizaji binafsi,” amesema.

“Naombeni sana turuhusu hayo na bei ya mafuta itashuka kuliko tulivyotarajia na wala tusidanganyane watu kwamba Serikali inaweza kutoa kodi kwenye mafuta, haiwezekani kodi ndiyo inayolipa mishahara na kununua madawa,” amesema Shabiby.
View attachment 2178669

Huyu ana Kundi lake…Katumwa na wafanyabiashara wenzake…Kwanza watuambie Mafuta ya Kula Wakati wanaagiza mbona Yakikuwa juu?
Mfano Zamani Dawa za Corono ziliagizwa na WHO kutoka Makampuni ya madawa na Ilisaidia Ktk udhibiti.
Sasa waneona watafute nafasi ya Kupiga wamemtuma tuu huyu…
Wafanyabiashara bana![emoji30]
Sukari wantuoiga,Mafuta ya Kula wanatupiga tangu zamani…
Sasa wanataka kuhamia kwa Petroleum [emoji23][emoji3]
 
Ila we jamaa comment zote hizo juu umeiona hiyo? Utakua una shida,
Tushawajua chuki zenu kwa January Makamba Ni dini yake, na sio msukuma mwenzenu, kingine mmemaindi fisadi Kalemani kutolewa Nishati
 
Utaratibu wa Bulk Procurement ni mbovu ni hakuna mfano na wala sio mwarobaini wa ukwepaji kodi tena ktk nchi hii swala la ukwepaji kodi kwa watu wakubwa haina dawa kwa sababu ccm inawajitaji mno wakati wa uchaguzi.

Kama soko la uagizwaji ukiachwa uwe liberalized unaweza ukasaidia sana kwani mafuta haya tunayotumia sana sana yanatoka uarabuni ambako bei yao waga iko juu ukilinganisha na nchi kama Russia ambao sasa hivi kwa sababu za vikwazo wanatoa "Discount" kubwa sana ya 20% ya bei ya sokoni.

Hivyo kama tungekuwa na waagizaji kutoka Russia sasa hivi bei isingekuwa juu kama ilivyo sasa. Ila kwa kuwa kuna watu wananufaika na utaratibu huu wa sasa bila shaka watapinga kwa sababu itawafanya wapoteze maslahi yao.
 
Shabiby kuna kitu hajakisema vizuri kuhusu uagizaji wa mafuta wa mtu mmoja mmoja, ubora wa mafuta unakuwa substandard sana, wengi wanafanya mix za uhuni, wanaleta mafuta with low Octane rating, alafu wanatuulia gari zetu.

Shabiby ana point, ila waagizaji binafsi wengi sio waaminifu, wanaleta mafuta with low quality, alafu wanahonga watu wa vipimo, mafuta yanapita alafu yanaua engine zetu

Takukuru iliundwa ya nini, si ifutwe tu tuelewe moja.

Kwa nini tuogope kitu kinachoweza kutupa unafuu kwa kuogopa rushwa wakati kuna vyombo vinavyotumia kodi zetu kushughulikia hilo tatizo.
 
Shabiby atoa mwarobaini kupanda bei mafuta​

MBUNGE wa Gairo Mohammed Shabib ameitaka Serikali kuruhusu kampuni binafsi kuagiza mafuta wenyewe bila kutumia uagizaji wa pamoja.

Shabiby ametoa ushauri huo leo Jumatano tarehe 6 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema mfumo wa uagizaji wa pamoja unafanya kutokuwepo kwa ushindani wa bei na hivyo bei inapopanda kwenye soko ambalo mafuta yanaagizwa kunakuwa hakuna mbadala.

“Leo hii mkiruhusu kampuni binafsi ziagize mafuta na kama mtu anaona kuna unafuu kwenye uagizaji wa pamoja afanye hivyo na kama ataona haina unafuu alete yeye,” amesema.

Ameongeza kuwa zimekuwa zikitolewa hoja za upotoshaji kwamba uagizaji wa mtu mmoja mmoja unasabisha ukwepaji wa ushuru.

“Meli zote zinashusha kwenye mita wanakwepaje ushuru? Hii kazi waachieni TRA utasikia TRA wanakula dili lakini ukiangalia tangu huu mfumo wa uagizaji wa pamoja mita imekufa mara nyingi kuliko kipindi cha uagizaji binafsi,” amesema.

“Naombeni sana turuhusu hayo na bei ya mafuta itashuka kuliko tulivyotarajia na wala tusidanganyane watu kwamba Serikali inaweza kutoa kodi kwenye mafuta, haiwezekani kodi ndiyo inayolipa mishahara na kununua madawa,” amesema Shabiby.
View attachment 2178669
Huyu ni mwongo!Wakiagiza huwezi kuwapangia bei! Wafanyabiashara watakula njama za kupandisha sana bei kuliko kawaida kwa kisingizio cha vita!
 
😀😀😀😀 nimecheka kinoma .
🇺🇸🇺🇸 akikusikia umenunua wese LA 🇷🇺🇷🇺. Nakwambia utakipata cha mtema kuni. Yaani
utakula kilichomshinda njiwa .
Lakini cha ajabu yeye US ananunua mpaka muda huu hukohuko RUSSIA😂😂😂😂😂😂😂.
wanasema Baba akikomba mboga haimaanishi na watoto nao wakombe.
Nani amekwambia US bado ananunua mafuta toka Russia, acheni kupotosha watu wengi wasiojua maswala ya kimataifa au kama ni effects ya vitu vingine vya kuvuta pia nakushauri uachane nazo.
 
Shabiby kuna kitu hajakisema vizuri kuhusu uagizaji wa mafuta wa mtu mmoja mmoja, ubora wa mafuta unakuwa substandard sana, wengi wanafanya mix za uhuni, wanaleta mafuta with low Octane rating, alafu wanatuulia gari zetu.

Shabiby ana point, ila waagizaji binafsi wengi sio waaminifu, wanaleta mafuta with low quality, alafu wanahonga watu wa vipimo, mafuta yanapita alafu yanaua engine zetu

Serikali inatakiwa kuimarisha taasisi zinazosimamia viwango tuu inatosha . Hakuna mfanyabiashara ataleta mafuta aje kupata hasara nakuhakikishia hilo.
 
Mkuu sio kweli hili,Botswana bei ya mafuta bado ni under 12P!na ni land locked country, ni mipango thabiti ya viongozi wao, moja ya vitu ambavyo ningependa kuuliza ni why awamu ya kwanza haikuweka utaratibu wa to keep on check ongezeko letu la watu?,President Samia ametuambia kuwa may be tutafikia ongezeko la kiuchumi la 5% soon, hii ni Safi ila tunaongezeka kwa 3%to4%!hii ni craze, tulitakiwa tuwe chini ya 1%ili ongezeko la uchumi tuweze kuliona.
Mkuu, ukiangalia idadi ya watoto chini ya miaka mitano huko mitaani unagundua kuwa watu wameacha kazi iendelee.... wamechagua kazi nyingine ya kuijaza Dunia. 😉
Tunatwanga maji kwenye kinu tu!😛
 
Mkuu, ukiangalia idadi ya watoto chini ya miaka mitano huko mitaani unagundua kuwa watu wameacha kazi iendelee.... wamechagua kazi nyingine ya kuijaza Dunia. 😉
Tunatwanga maji kwenye kinu tu!😛
Na hii inasikitisha mno,nchi tunazaliana mno na hili linaongeza umasikini kwenye family zetu
 
Back
Top Bottom