Mohammed Shabiby: Namna ya kupunguza bei za mafuta kwa 50% ya bei za sasa

Mohammed Shabiby: Namna ya kupunguza bei za mafuta kwa 50% ya bei za sasa

Shabiby atoa mwarobaini kupanda bei mafuta​

MBUNGE wa Gairo Mohammed Shabib ameitaka Serikali kuruhusu kampuni binafsi kuagiza mafuta wenyewe bila kutumia uagizaji wa pamoja.

Shabiby ametoa ushauri huo leo Jumatano tarehe 6 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema mfumo wa uagizaji wa pamoja unafanya kutokuwepo kwa ushindani wa bei na hivyo bei inapopanda kwenye soko ambalo mafuta yanaagizwa kunakuwa hakuna mbadala.

“Leo hii mkiruhusu kampuni binafsi ziagize mafuta na kama mtu anaona kuna unafuu kwenye uagizaji wa pamoja afanye hivyo na kama ataona haina unafuu alete yeye,” amesema.

Ameongeza kuwa zimekuwa zikitolewa hoja za upotoshaji kwamba uagizaji wa mtu mmoja mmoja unasabisha ukwepaji wa ushuru.

“Meli zote zinashusha kwenye mita wanakwepaje ushuru? Hii kazi waachieni TRA utasikia TRA wanakula dili lakini ukiangalia tangu huu mfumo wa uagizaji wa pamoja mita imekufa mara nyingi kuliko kipindi cha uagizaji binafsi,” amesema.

“Naombeni sana turuhusu hayo na bei ya mafuta itashuka kuliko tulivyotarajia na wala tusidanganyane watu kwamba Serikali inaweza kutoa kodi kwenye mafuta, haiwezekani kodi ndiyo inayolipa mishahara na kununua madawa,” amesema Shabiby.
View attachment 2178669
WENYE NCHI WAMEAMUA SERIKALI YAO NDIO IAGIZE
 
Binafsi namkubali sana Mhe. Shabiby kwa ushauri anaoutoa mara kwa mara kwa Serikali. Jana ameishauri Serikali juu ya utaratibu wa uagizaji wa mafuta ili bei iwe nafuu kwa watumiaji. Ameendelea kuelezea kuwa suala la BULK import ni suala linaloleta rushwa na ukiritimba. Ni ukweli usiopingika ile kamati ya uagizaji mafuta wanaweza kushawishiwa kupokea rushwa ili watoe upendeleo kwa muagizaji atakayepewa nafasi ya kuagiza. Hili nakubaliana nao kwa asilimia mia moja. Akaendelea kushauri kuwa kuwe na utaratibu wa bulk import na pia kuwe na waagizaji binafsi ili kuwe na ushindani na kwa utaratibu huu bei ya mafuta itapungua hata kwa asilimia hamsini. Ameendelea kusema kuwa hata kodi ya Serikali itaongezeka maradufu kwa kuwa watasimamia flow meter inayoshusha mafuta. Mhe. Rais ikikupendeza napendekeza Mhe. Shabiby ateuliwe kuwa Waziri ana mawazo mazuri ya kuwasaidia Watanzania.
 
Mafuta ya kula na sukari kila mtu anaagiza mbona hali inakua mbaya kila uchwao? Pia kila mtu alipokuwa anaagiza migomo ya vituo vya mafuta ilikuwa mingi...ikiwemo vituo kusingizia havina mafuta na ilikuwa ngumu kuinforce coz wakati mwingine serikali haikuwa na data za uagizaji wao ...wanataka kuturudisha tulipotoka.
 
Binafsi namkubali sana Mhe. Shabiby kwa ushauri anaoutoa mara kwa mara kwa Serikali. Jana ameishauri Serikali juu ya utaratibu wa uagizaji wa mafuta ili bei iwe nafuu kwa watumiaji. Ameendelea kuelezea kuwa suala la BULK import ni suala linaloleta rushwa na ukiritimba. Ni ukweli usiopingika ile kamati ya uagizaji mafuta wanaweza kushawishiwa kupokea rushwa ili watoe upendeleo kwa muagizaji atakayepewa nafasi ya kuagiza. Hili nakubaliana nao kwa asilimia mia moja. Akaendelea kushauri kuwa kuwe na utaratibu wa bulk import na pia kuwe na waagizaji binafsi ili kuwe na ushindani na kwa utaratibu huu bei ya mafuta itapungua hata kwa asilimia hamsini. Ameendelea kusema kuwa hata kodi ya Serikali itaongezeka maradufu kwa kuwa watasimamia flow meter inayoshusha mafuta. Mhe. Rais ikikupendeza napendekeza Mhe. Shabiby ateuliwe kuwa Waziri ana mawazo mazuri ya kuwasaidia Watanzania.
Inahitaji mjadala kuhusu hilo
 
Biskuti TU zinaagizwa nje lakn Bei hazishuki sembuse mafuta Tena bidhaa hitajika
 
Nakubaliana na wewe, huyu Shabiby nami nimemfuatilia sana hotuba zake bungeni yuko very creative na kwa kuwa ni mfanyabiashara ana Uelewa mkubwa. Halafu huyu jamaa yeye huwa anachangia kwenye eneo analolielewa vizuri, kiukweli angefaa sana kuwa waziri kwenye eneo hili. Pili baada ya Kusikiliza michango yake nikajiuliza kwa nini na sisi tusinunue mafuta kwa Rubo kama India ili tupate punguzo kubwa?? Yaani huu mgogoro Kuna mataifa yatanufaika sana kwa kununua mafuta kwa bei poa na kuwa na reserve ya kutosha.
 
Maana yake nini kutuwekea hii?

Je, unaleta orodha ya nchi hizi 16 dunia nzima na bei za mafuta ya petrol ku justify inachokifanya serikali ya Tanzania kuwasababishia ugumu wa maisha ya wananchi wake wa kawaida?

Ok. Hata hivyo;

Ulipaswa kwenda mbali zaidi kwa kulinganisha na viwango vya uchumi vya nchi hizi..

Kisha useme na hatua inayochukua kila moja ya nchi hizo kukabiliana na upandaji wa nishati ya mafuta ya petrol ili kuleta unafuu wa maisha..

Mwisho umalizie na hatua ambazo serikali yako ya Tanzania inazo chukua ku - comprehend hii hali mbaya ya kiuchumi..
 
Nakubaliana na wewe, huyu Shabiby nami nimemfuatilia sana hotuba zake bungeni yuko very creative na kwa kuwa ni mfanyabiashara ana Uelewa mkubwa. Halafu huyu jamaa yeye huwa anachangia kwenye eneo analolielewa vizuri, kiukweli angefaa sana kuwa waziri kwenye eneo hili. Pili baada ya Kusikiliza michango yake nikajiuliza kwa nini na sisi tusinunue mafuta kwa Rubo kama India ili tupate punguzo kubwa?? Yaani huu mgogoro Kuna mataifa yatanufaika sana kwa kununua mafuta kwa bei poa na kuwa na reserve ya kutosha.
Kwamba Ahmed Shabiby anaweza kuwa waziri mzuri sana kwenye sekta ya nishati kwa sababu ya michango yake bungeni..?

No way!.... Hizi ni fikra za KUJIDANGANYA na inaelekea wengi hamjui kiini cha tatizo la nchi hii kilipo..!

Tatizo la uongozi wa nchi hii haliko kwenye uzuri au ubaya wa mtu as a person..

Tatizo la nchi hizi liko kwenye mfumo wetu wa kisiasa na kiutawala..

Tukiwa na tatizo ktk eneo hili, hata tuwe na watu wazuri na wasomi wa kiwango cha Havard or Oxford universities na tukawapa uongozi ktk sekta muhimu zote za nchi hii..

Lakini so long as hawa viongozi watakuwa wametokana na watatekeleza majukumu yao ndani ya mfumo wa kisiasa na kiutawala wa dizaini hii, basi watakuwa wa hovyo na wajinga kama hawajawahi kwenda shule yoyote vile..!!

Nitakupa mfano latest na mzuri kabisa wa IGP huyu aliyepo ndugu Simon Sirro..

Huyu bwana kabla hajawa IGP akiwa polisi wa kawaida tu ngazi za chini huko, tulikuwa tunamuona mtu mzuri sana hata kusema akipewa u - IGP, basi TANPOL litakuwa jeshi bora sana hapa TZ..!

Mungu siyo Athumani bwana. Ni IGP sasa lakini kawa ni defection ya hali ya juu. Mpaka sasa mnadai na kumtaka ajiuzulu kwa sababu ameshindwa kazi ya u - IGP..!

Lakini tatizo siyo yeye as a person na usomi wake. Tatizo ni mfumo wa kisiasa na kiutawala tulionao. Mfumo wetu unapelekeshwa na viongozi na siyo viongozi waongozwe na wafuate mfumo unavyowataka wawe..!!
 
Wanataka watuletee mafuta yasiyo na quality. zaidi zaidi watalketa mafuta mabovu waliyonunua vichochoroni na kutuuzia kwa bei ya soko.
 
Atuambie kwa nini serikali iliamua huo utaratibu wa bulk procurement? Sababu hizo haziko leo hii?

Umeacha jambo muhimu ambalo Mh Shabibu aliliongelea. Kulikuwa na kampuni ya India Alliance ambayo kwa mujibu wa huyu Mh ndio wenye refinary kubwa duniani. Hii kampuni ilitaka kuleta mafuta na kwa kuanzia ikayanunua makapuni ya mafuta mawili hapa nchini GAPCO na jingine. Hii tayari ni kuua ushindani wa soko ili ufanye monopoly na unaweza kuyumbisha serikali ukitaka kwenye suala la mafuta.

Tuseme ukweli hivi mfanyabiashara gani bepari anaweza kuwahurumia wananchi walaji wa mwisho kwa kupunguza bei eti kuwaonea huruma? Hayuko wa aina hiyo. Leo mfanyabiashara wa mafuta akaenda deep sea akakuta hizo meli anazosema Mh Shabibu ziko huko zinasubiria wateja. Akiuziwa lita moja ya Petrol kwa 200/- bado atakuja kuiza 2,855/-. Punguzo la 6/- insiginifacant.

Huyu Mh aseme alikuwa na maslahi yake aliyopokwa kwenye hiyo bulk procurement basi. Suala la flow meter kuharibika ni uzembe tu. Kuwaachia waagiza mafuta wa agize kiholela itakayoumia ni serikali kwenye kodi na Wananchi. Hii ya kusema italeta unafuu haina mashiko hata kidogo, zaidi ya kunufaisha wafanyabiashara wakina Mh shabibu na kuwaumiza wananchi na serikali itakosa kodi kwa kuongeza mwanya wa upigaji na kuwa pengo la upigaji na ukwepaji kodi.
 
Nchi kama rwanda inapitishia mafuta yake kwetu,
Lakini mbona bei yao rahisi kuliko sie?
 
Huyu ni mwongo!Wakiagiza huwezi kuwapangia bei! Wafanyabiashara watakula njama za kupandisha sana bei kuliko kawaida kwa kisingizio cha vita!
Kwa hiyo tusifanye chochote au? na hao wanaoagiza ambao hawazidi watano huoni ndio rahisi kuweka njama za kutupandishia bei? na tuna vyombo vya serikali vinatakiwa kuangalia upuuzi wa price rigging kitu ambacho ni illegal, as of now wananchi are paying the price kutokana na policy mbaya na vyombo vyetu dhaifu vya kusimamia biashara ya mafuta ambavyo vimejaa rushwa tupu na watu wasio na akili, tuanze na kubadilisha policy kwanza na kuondoa monopoly na kuimarisha usimamizi wa hii biashara iwe fair kwa wote
 
Atuambie kwa nini serikali iliamua huo utaratibu wa bulk procurement? Sababu hizo haziko leo hii?

Umeacha jambo muhimu ambalo Mh Shabibu aliliongelea. Kulikuwa na kampuni ya India Alliance ambayo kwa mujibu wa huyu Mh ndio wenye refinary kubwa duniani. Hii kampuni ilitaka kuleta mafuta na kwa kuanzia ikayanunua makapuni ya mafuta mawili hapa nchini GAPCO na jingine. Hii tayari ni kuua ushindani wa soko ili ufanye monopoly na unaweza kuyumbisha serikali ukitaka kwenye suala la mafuta.

Tuseme ukweli hivi mfanyabiashara gani bepari anaweza kuwahurumia wananchi walaji wa mwisho kwa kupunguza bei eti kuwaonea huruma? Hayuko wa aina hiyo. Leo mfanyabiashara wa mafuta akaenda deep sea akakuta hizo meli anazosema Mh Shabibu ziko huko zinasubiria wateja. Akiuziwa lita moja ya Petrol kwa 200/- bado atakuja kuiza 2,855/-. Punguzo la 6/- insiginifacant.

Huyu Mh aseme alikuwa na maslahi yake aliyopokwa kwenye hiyo bulk procurement basi. Suala la flow meter kuharibika ni uzembe tu. Kuwaachia waagiza mafuta wa agize kiholela itakayoumia ni serikali kwenye kodi na Wananchi. Hii ya kusema italeta unafuu haina mashiko hata kidogo, zaidi ya kunufaisha wafanyabiashara wakina Mh shabibu na kuwaumiza wananchi na serikali itakosa kodi kwa kuongeza mwanya wa upigaji na kuwa pengo la upigaji na ukwepaji kodi.
Kwa hiyo tusifanye kitu au tufanye nini?
 
Kwa hiyo tusifanye kitu au tufanye nini?

Serikali ijiridhishe je, zile sababu za kuacha utaratibu wa zamani wa uagizaji mafuta kiholela kwa kila mfanyabiashara kivyake hazina umuhimu tena hii leo? Ikiona kuna umuhimu wa kuendelea na huu wa sasa wa bulk procurement basi mapungufu yaliyo jitokeza yarekebishwe.

Kama kuna jambo ambalo wafanyabiashara binafsi wanaweza kufanya lililo katika utaratibu wa kisheria wa ununuzi wa mafuta ambalo litafanya bei ishuke serikali haishindwi kulifanya. Hiyo flow meter kuharibika mara kwa mara kama serikaili ina utashi wa kweli hilo haliwezi kujitokeza. Serikali itoe ruzuku kama njia nyingine za kupunguza bei ya mafuta zimeshindikana. Serikali iachane na kuanzisha miradi mipya ya kimaendeleo mwaka wa fedha 22/23 ambayo inaigharimia yenyewe 100%, ili iweze kutoa ruzuku kunako hitajika mpaka hali hii ya mtikisiko wa kiuchumi itakapotengemaa.

Serikali isidanganyike ikaruhusu wafanyabiashara binafsi kwenda kununua mafuta ya hizo meli za Urusi zinazo semekana ziko huko deepsea. Hii itakuwa ni kuiweka hali ya nchi yetu ya ulinzi na kiusalama kuwa hatarini. NATO hawawezi kuvumila kuona vikwazo vya kiuchumi ilivoiwekea Urusi vikihujumiwa.

Wafanyabiashara wa mafuta tamaa zao za kujitajirisha zisije zikawaingiza matatani wafanyabiashara wengine kushikiwaliwa mali zao, kuwekewa vikwazo kwa wanasiasa wengine nchini nk. Tumeshuhudia kilicho wapata oligaki wa Urusi.
 
Bulk procurement faida yake ninayoiona ni control ya kodi.

Ila faida ya kuacha watu waagize wenyewe ni ushindani wa bei hapa ananufaika mlaji wa mwisho.

Sasa ni jambo la kuchagua kati ya hayo mawili.

Kodi kwa serikali au faida ya soko huria.
Control ipi ikiwa mita zinaharibiwa makusidi kuliko hapo awali?

Pili Kodi inalipwa kwenye vituo vya mafuta na consumers au huwa hudai risiti ukienda kununua?
 
Tatizo biashara ya mafuta inashikiliwa na wanasiasa walafi ambao ndio wanaotoa maamuzi kwa maslahi yao binafsi. Kuna haja ya kufanya mapinduzi ya kuokoa nchi kutoka mikononi manyang'au yalinayohodhi madaraka
Maskini anaweza fanya mapinduzi gani? Maskini wa akili na mali kama Mwendazake alifanya nini cha maana zaidi ya kuua uchumi?

Maskini wengine wa mali na akili wa Zambabwe walifanya nini cha maana zaidi ya kuvuruga Nchi?

Yaani umpe maskini aharibu afu na yeye aanze kuiba Ili ajitie kwenye ufukara si utakuwa ni Wehu.Maskini siku zote ni hasara tuu.
 
Serikali ijiridhishe je, zile sababu za kuacha utaratibu wa zamani wa uagizaji mafuta kiholela kwa kila mfanyabiashara kivyake hazina umuhimu tena hii leo? Ikiona kuna umuhimu wa kuendelea na huu wa sasa wa bulk procurement basi mapungufu yaliyo jitokeza yarekebishwe.

Kama kuna jambo ambalo wafanyabiashara binafsi wanaweza kufanya lililo katika utaratibu wa kisheria wa ununuzi wa mafuta ambalo litafanya bei ishuke serikali haishindwi kulifanya. Hiyo flow meter kuharibika mara kwa mara kama serikaili ina utashi wa kweli hilo haliwezi kujitokeza. Serikali itoe ruzuku kama njia nyingine za kupunguza bei ya mafuta zimeshindikana. Serikali iachane na kuanzisha miradi mipya ya kimaendeleo mwaka wa fedha 22/23 ambayo inaigharimia yenyewe 100%, ili iweze kutoa ruzuku kunako hitajika mpaka hali hii ya mtikisiko wa kiuchumi itakapotengemaa.

Serikali isidanganyike ikaruhusu wafanyabiashara binafsi kwenda kununua mafuta ya hizo meli za Urusi zinazo semekana ziko huko deepsea. Hii itakuwa ni kuiweka hali ya nchi yetu ya ulinzi na kiusalama kuwa hatarini. NATO hawawezi kuvumila kuona vikwazo vya kiuchumi ilivoiwekea Urusi vikihujumiwa.

Wafanyabiashara wa mafuta tamaa zao za kujitajirisha zisije zikawaingiza matatani wafanyabiashara wengine kushikiwaliwa mali zao, kuwekewa vikwazo kwa wanasiasa wengine nchini nk. Tumeshuhudia kilicho wapata oligaki wa Urusi.
Nimeshajibu hapo awali kwamba mara nyingi watu wenye fikra za kijamaa huwa Wana akili finyu Sana na Wanaongozwa kwa mihemko..

Kama ulimsoma Shabiby ameelezea historia ya hadi kuamua kuanzisha bulk procurement kwamba kuna wafanyabiashara walitaka kumuondoa mmja wa wafanyabiashara wenzao kwenye soko kwa sababu alikuwa anauza mafuta Kwa bei ya chini kuliko wao kwa hiyo wakafanya mgomo kwa kisingizio kwamba Bei ya kilimo waliyowekewa na Ewura haiwalipi kwa sababu ewura wali gauge bei kwa kufuata anachouza huyo mwenzao..

Sasa Ili kujilinda wakafanya walichofanyia ndio ukaja mswaada wa bulk procurement..

Point yangu inabakia pale pale,ku deal na changamoto za free market economy ni nafuu kuliko kuleta control economy.Kwa Sababu since then hakuna unafuu uliopatikana kwa wananchi zaidi ya kulinda kundi la wanufaika na bulk procurement system..

Serikali itenge bajeti kubwa ya kujenga storage facilities kwa ajili ya mafuta ya reserves Ili pindi ikitokea scenario ya wafanyabiashara ku collude na kulazimisha bei iingize mafuta yake kwenye mzunguko wakati inatatua changamoto itakayokuwa imejitokeza..
 
Back
Top Bottom