GE2025 Moja ya impacts za CHADEMA kutoshiriki Uchaguzi zaanza kuonekana sasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Usidanganyike na nguvu za dola wanazotumia CCM. Kulikua na dola ya Urumi ilikua na nguvu kubwa sasa hivi tunaisoma kama historia kwenye vitabu.
Na ilichukua miaka mingapi kuangushwa? Na nani aliwaangusha? Kulikuwepo na KANU, UNIP na wengine lakini wote ama hawapo wanachechemea.

Ni lazima iko siku CCM itaondoka lakini sio lazima kuwa itaondoshwa na Chadema. Chadema ya sasa haitaweza kazi hiyo labda ikijipanga upya kabla ya 2030. Na anaeweza kuipanga upya anafahamika. Sio huyu aliye rumande au msaidizi wake.

Amandla.
 
Vyama hivyo rafiki ni kama mnyama fulani,anayedhani mkono wa binadamu anayetembea unaweza kudondoka wakaufaidi kwa kuula,, wakati kumbe sivyo, ngoja tuone mwisho wake.
 
Dhambi nyingine ya Chadema ni kuwa kutokuwa na upinzani imara kunatoa nafasi kwa CCM kuendesha uchaguzi wa haki na uwazi kuliko walivyo wahi kufanya kwa sababu hawana hofu ya kushindwa. Chadema itawasaidia kwenye hilo kwa kuendesha kampeni chafu dhidi ya wagombea wa Chaumma na ACT-WAZALENDO. Itakuwa yale yale ya bora tukose wote. Wakifanya hivyo hawatakuwa tofauti na wakina Bulaya na Msigwa.

Amandla...
 
Unataka washiriki uchaguzi na sio kushinda uchaguzi
 
NO REFORMS NO ELECTION, Watanzania wanajua vyama vingine nje ya CHADEMA ni Mali ya CCM hivyo uchaguzi bila CHADEMA tafsiri yake ni kwamba CCM inasimama peke yake kwenye uchaguzi na kujipigia kura.NO REFORMS NO ELECTION Hesabu zetu tunazifungia hapo.
 
Kutakuwa na low voter turnout,the country ever experienced
hakutakuwa na hiyo scenario, kwa sababu waliokuwa wabunge wa CHADEMA, wengi wanagombea ubunge na udiwani kupitia vyama vingine, ni rahisi sana watu kuisahau CDM, na sasa haizungumziwi kabisa, na maisha yanaendelea
 
Unataka washiriki uchaguzi na sio kushinda uchaguzi
Lengo la kushiriki uchaguzi sio kushinda tu bali pia kutuma ujumbe. Cornell West alipo gombea urais Marekani nia yake kubwa ilikuwa ni kuingizwa masuala yasiopewa kipaumbele na vyama katika mjadala wa kitaifa. Hata kama Chaumma haitashinda ubunge hata mmoja, kushiriki kwao kutawatangaza zaidi kwa umma na kama mchezo mchafu utafanyika watauweka wazi. Kwa kufanya hivyo watakuwa katika nafasi nzuri zaidi katika chaguzi za 2029 na 2030.

Amandla...
 
CDM hawakuzuiliwa ila walijizuia wenyewe, mbona wabunge wengi waliokuwa chadema, wanagombea kupitia vyama vingine, CDM si chama chenye kuamua mustakabali wa siasa za vyama vingi. Vyama 18 virtashiriki uchaguzi, vinatosha kuzidi
 
Hamna kitu ww kilaza tu kama wenzako 55
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…