Hi all,
Chadema imefanikiwa sana katika mkakati wake iliouleta wa NRNE, tayari msamiati huu umewafikia walengwa. Kwa mtu smart na anayefuatilia vizuri siasa za Bongo anaweza kukupa ukweli huu, tatizo wengi tunaangalia matokeo ya uchaguzi wenye kulalamikiwa. Impact ya NRNE tutaiona kwenye foleni za siku ya kupiga kura, wangapi watajitokeza, habari ya simple majority tuiweke kando. Nadhani wengi tutakumbuka uchaguzi serikali za mitaa ulikuwaje.
Umuhimu wa Chadema kwenye uchaguzi huu ni mkubwa maana nchi inashindanisha Wagombea bora kwa sera na hoja zenye mashiko, CCM wanapata changamoto Chadema akiwepo, na CCM wanalijua hili vizuri. Baada ya CDM kuondokewa na wanachama kwenda Chauma, ni kama nyoka anavyojivua gamba. Leo CDM wakirudi kwenye Uchaguzi ( baada ya NRNE kufanyiwa kazi), watakuwa Wazuri na hatari kwa CCM kuliko kabla na vijana wengi wataingia CDM wenye Bongo kali kwa kuwa kutakuwa na fursa/nafasi huru kuliko CCM. Rejeo la CDM kwenye uchaguzi na ulingo wa siasa ktk mazingira yaliyorekebishwa utaifanya CDM kuwa ktk mstari sahihi.