GE2025 Moja ya impacts za CHADEMA kutoshiriki Uchaguzi zaanza kuonekana sasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
NO REFORMS NO ELECTION, Watanzania wanajua vyama vingine nje ya CHADEMA ni Mali ya CCM hivyo uchaguzi bila CHADEMA tafsiri yake ni kwamba CCM inasimama peke yake kwenye uchaguzi na kujipigia kura.NO REFORMS NO ELECTION Hesabu zetu tunazifungia hapo.
kumbe malengo ya NENR yametimia
 
Jibu rahisi ni kutoshiriki uchaguzi wapite tu kama walivyopanga sisi tuendelee na maisha yetu.
 
Huwezi kusimamisha gari ukiwa ndani yake. Acha wasusie Chama kitaendeeshwa na michango ya hiyari ya wanachama/wananchi.
 
Wewe mwenyew kilaza tu kama huyo bumunda mwenzako
😀😀any way CDM umeipenda mwenyewe the geneous, acha si vilaza tuendele kuona mnavyoteseka kisaikolojia, but u need to see a psychiatrist, utapona tu
 
Kuchukua fomu sio kushinda ubunge. Wanachukua 50 Lakini atapitishwa mmoja. Kwenye msafara wa mamba lazima kenge wawepo

Hao wanachukua fomu, wanatumia Haki Yao kwa mujibu wa Katiba. Hata CHADEMA kilikuwa na Haki yake kwa mujibu wa Katiba kuingia kwenye uchaguzi.

Lakini pia CCM itatengeneza mapato makubwa sana kutokana na uuzaji wa fomu. Hii nayo ni project nzuri kwa chama chenye wafuasi wengi. Sisi tuendelee kushinda kwenye keyboard, wengine wanasonga hivyo!
 
Mpaka sasa hivi kuanzia 2020 Bunge lote ni la CCM.Kwani CHADEMA wana kosa gani kukataa kushiriki upuuzi wa kupotezeana muda na maumivu juu?
 
Chadema wao ndiyo waliamua hivyo na wako tayari kwa matokeo yoyote. Mtu yeyote kama anaona maamuzi hayo si mazuri ni ruksa kuhamia chama kingine.
No reforms no election
 
😀😀any way CDM umeipenda mwenyewe the geneous, acha si vilaza tuendele kuona mnavyoteseka kisaikolojia, but u need to see a psychiatrist, utapona tu
Sasa wew mtu anatoa hoja kuwa CHADEMA ishiriki uchaguzi usio huru na uwazi then anatoa sababu eti kuwa wakishiriki wanajiitengenezea platform ya kushinda miaka mitano ijayo na na kupata umarrufu kwa watu ,
Kitu ambacho hakina sense yoyote mwanaichi gani huyo hajawahi kusikia uwepo wa chadema kwanza mpka ianze kutafuta umaarufu Lissu katawanya panya wengi sana pale wapiga dili
 
Sikiliza, ni bora Chadema isiwepo kabisa kuliko kushiriki kitu cha maigizo.

Unashiriki ili iwe nini wakati unajua hata ukishinda huwezi kutangazwa?

Kushiriki ili kupewa hisani ya wabunge wachache ni ujuha, ni kujali maslahi binafsi kuliko ya nchi.

Kuwa na demokrasia danganya toto ni upuuzi.

Ni aidha tuwe na mfumo kamili wa vyama vingi ama turudi chama kimoja.

Tunatumia pesa nyingi mno kuandaa uchaguzi wa maigizo, kama hatutaki vyama vingi, kwa nini tusiwe kama china?

Futa vyama vingi pesa za kulipa tume ya uchaguzi na gharama zote ziende kwenye maendeleo.
 
Uchambuzi murua kabisa!
 
ok, nimekuelewa, ni vyema kutoshiriki labda 2030 kama reform zitafanyika, otherwise hakuna haja ya kushiriki dhambi, viachiwe hivyo vyama 18 viendelee
 
Hamna kitu ww kilaza tu kama wenzako 55
Wewe sio wa kwanza kuniita kilaza. Kuwaingiza G-55 kwenye hilo ni kuwaonea. Kwa vile wewe sio kilaza kama mimi, nielimishe No Election ina maanisha nini na itafanikishwa vipi.

Amandla...
 
Acha ujinga mzee, chadema walishaelezea maama ya NRNE

Wagombea wao kuenguliwa hovyo bila sababu ya msingi, wizi wa kura, mawakala wao kuzuiwa kungia kwa muda kwenye vyumba vya kupigia kura

Kanuni za maadili zilizotungwa kwenye uchaguzi huu si rafiki kwa Upinzani

Ndo maana wanadai reforms ili kuwe na fair election

Kuunganisha nguvu bila uchaguzi huru hakuna maana yoyote, wagombea wenu wataenguliwa mawakala wenu watazuiwa ili watu waingize kura feki, wanachama wenu watauawa kwa kudai haki Yao ambayo ni kura


Ila kwa wajinga kama nyinyi hamuelewi ni kuilaumu chadema kama fala
 
Nimesema wapi Chadema ishiriki kwenye uchaguzi? Chadema mpaka sasa hivi haiwezi kushiriki bila kusaini masharti ambayo kila mmoja anajua yana kasoro kibao. CHADEMA ikisaini itaonekana kuwa ni wanafik na ikishiriki kwenye uchaguzi bila reforms ( wenye nchi wamesema Katiba mpya ni ajenda ya 2026 mpaka 2030) kufanyika unafik wao utazidi kuthibitishwa. Naamini kwenye hili busara zitawaongoza na hawatashiriki.

Niliozungumzia ushiriki wao ni Chaumma. Chaumma ya sasa imekuwa na muda mfupi sana wa kujijenga kwa wananchi. Kinachowabeba ni sifa za watu na sio chama. Chaumma watatumia vyema muda wa kampeni na baada ya kampeni kujijenga zaidi. Itakapofika 2029 watakuwa katika nafasi nzuri zaidi hasa kama Chadema wataendelea kukaza shingo. Pengo la Chadema litazibwa na Chaumma na ACT-WAZALENDO.

Tafadhali jitahidi kuandika kwa ufasaha zaidi ili sisi vilaza tuweze kukuelewa. Ungeandika upya paragraph yako ya mwisho ili iwe rahisi kwa vilaza kukuelewa. Samahani lakini.

Fundi Mchundo Kilaza

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…