Morocco ilijitoa Afrika ikajiomba kujiunga Ulaya ila wazungu wakaikataa. Hii inatufundisha nini?

Ningekuwa na Mamlaka ningeiomba Marekani iichukuwe Tanzania liwe jimbo la 53 la Marekani na Watanzania wote automatically wanakuwa Wamarekani.

Morocco walikuwa sahihi, ila ukiwa kichwa maji huwezi kuliona hilo.
Gwajima aliahidi kubadilishana vijana waende Birmingham Alabama.!
 
Unashindwa hata ku Google kitu kidogo upate uelewa.
 
Mwenye kukosa akili ni yupi mkuu kati ya mimi na morroco

Morocco aliyejiondoa africa kujiunga ulaya wakamtosa
Kumbe naongea na mtu ambae huna akili. Haya endelea na ujinga wako
 
Yaan mashindano ya kabumbu ya dunia yamekuchanganya mno
 
Huu ni uongo. Moroco ni mwanachama mwanzilishi wa OAU, ambapo ilijiunga May 25, 1963.

Moroco alijitoa OAU mwaka 1984 kupinga Chama cha POLISARIO cha Sahara Magharibi kupewa kiti OAU kama mwakilishi wa Western Sahara, sehemu ambayo Moroco inasema ni jimbo lake.

Moroco alirudi AU (Zamani OAU) mwaka 2016 kama mwanachama baada ya kampeni ndefu ya kutaka utambulisho wa POLISARIO ufutwe. Utakumbuka hata Tanzania ilikuwa ikiitambua POLISARIO na hata mfalme wao kuja hapa Tanzania wakati wa Magufuli akatujengea Msikiti pale Kinondoni na ahadi ya Uwanja Dodoma ni sehemu ya kampeni za kuitokomeza POLISARIO.

So siyo kweli Moroco walijitoa sababu walijiona wazungu. Moroco ina native wengi ambao ni Berbers kuliko Waarab na hao ni wenyeji wa Moroco kama Wagogo walivyo wenyeji wa Tanganyika
 
Uongo wa nn makuu ethiopia ni karibu kwa kila nchi kwa kuwa ipo katikati
Tulia wewe standard 4 geography failure, Morocco ipo mbali sana na Ethiopia tena sanaaaa. Na kwa sababu yako ya katikati bora ungesema Central African republic au Congo DRC
 
Tuanze na:
Source # 1
Source # 2
Haya ni makitu gani wakuu naona karibu kila uzi
 
Tuanze na:
Source # 1
Source # 2
Haya ni makitu gani wakuu naona karibu kila uzi
Nadhani ni chanzo cha habari ila sasa huyu mwandishi hajaleta chanzo kaleta umbeya.
 
Ikawaje wakaenda kuomba kujiunga ulaya
 
Nadhani ni chanzo cha habari ila sasa huyu mwandishi hajaleta chanzo kaleta umbeya.
Nilitarajia hivyo vitu nitaona kadri ninavyosoma lkn hola.
Na wengi wanaanza hivyo lakini matumizi yake ni zero
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…