Ujinga unatutafuna sisi waluguru na utaendelea kututafuna.....kuna mtu alisema mluguru ukimpa kofia ya fisiem au kanga halafu ukamwambia anywe sumu ili uone kama inaua anakunywa........(mtu akikunyima elimu kakunyima vitu vingi sana .....hawa watu wawapendi ndugu zetu waelimike kwa sababu wakielimika hawawachagui)........pole zenu njooni huku kasikazini kuna unafuu...
Cha ajabu huenda una degree ila upeo wako uko chini sana hebu niambie barabara ina uhusiano gani na kujituma kwa wananchi.Wapeni wananchi yale mliyowaahidi MUNGU anawaona mlivyo wanafiki
Wilaya kama hizi ni nyingi sana. Na, binafsi wala siwashangai Wananchi hao kwa kuipigia kura CCM; maana ndiyo ufahamu wao umeishia hapo.
Lakini, si wakati wote ufumbuzi wa matatizo yetu ni kuchagua Upinzani; Vyama vya Upinzani havipati Wanachama toka Germany, Viongozi wao na Wanachama wanatoka miongoni mwetu sisi hawa hawa. Halmashauri Manispaa ya Musoma ilikuwa ya CHADEMA, nini cha maana sana kilichofanyika kule? UKAWA watasingizia waliibiwa kura.
Ishu ni kwamba je kuna maendeleo? Upeo mpana peke yake hautoshi. Hata utumbo upo utumbo mpana
Maendeleo ya aina gani na yaletwe na nani? Mf.barabara au hospital au maji nani anatakiwa awpelekee wananchi kama sio nyie mnao kusanya kodi msikwepe wajibu wenu hivyo nilivyo vitaja hapo juu sio kazi ya mbunge
Ujinga unatutafuna sisi waluguru na utaendelea kututafuna[/QUO
Naumia sana kwa ukweli huu! Mimi natoka kwa WACHIRO na WAPONDA! basi siendelei sana
Watu wa morogoro mjini,vijijini,kilosa,mvomero na gairo wote ------- sana.
Wanadanganywa kama ------- vile
Wilaya hii makao makuu yake yapo moro mjini kwa kuwa watendaji wengi wa wilaya hii wanakwepa maisha ya dhiki yasiyo stahili kuishi binadamu ndani ya wilaya.
ELIMU:
-Wilaya ya Morogoro hakuna hata shule moja ya Advance level (kidato cha tano na sita).
-Shule za msingi zilizopo ni duni chakavu tena zilizochoka.
-Hakuna walimu wa kutosha. Kuna shule kama shile ya msingi kitengu, lumba chini na lumba juu kuna mwalimu mmoja mmoja kila shule.
Mbunge ni wa ccm.
AFYA:
Wilaya hii hakuna hospital yenye hadhi ya kuwa hospital ya wilaya. Kuna kituo cha afya cha tawa eti ndo wanataka kuifanya hospital ya wilaya. Kiukweli haina hadhi, kama ingekuwa Dar hii ingekuwa zahanati.
Mbunge ni wa ccm.
BARABARA:
Unaweza ukafikiri kama nafanya uchochezi au masihara ila ukweli ni kwamba HAKUNA HATA MITA MOJA ya kipande cha lami. Barabara huku kwetu ni za vumbi zilizojaa makorongo zinazohatarisha safari.
Mbunge ni wa ccm.
UONEVU:
wananchi wanaonewa kwa kulipishwa michango na faini zisizo na tija. Kuna mpango wa kila kata kuchangia shilingi elfu moja kulipia vyanzo vya maji mpango huu unaratibiwa na shirika na CARE INTERNATIONAL. Wakati mito Mungu mwenyewe ndiyo kaiumba na ipo tu siku zote toka utotoni kwa bibi na babu zetu na tulikuwa tunatumia bure.
Mbunge ni wa CCM.
Lakini pamoja na yote hayo wananchi wameridhika na ccm huwaambii kitu juu ya CCM yao.
Huku mgombea akishapitishwa na CCM basi yeye ndiye mshindi kwa asilimia 90. Haijawahi pata kiongozi wa upinzani ingawa mwaka 2005 - 2010 tulikuwa na diwani mmoja tu wa chadema kata ya kibungo juu.
Wananchi tumeamua kujisemea wenyewebkwa kuwa masikini wachache na wajinga wachache wanatuumiza sisi kwa kuendelea kuichagua ccm.
Wanakera sana watu wa morogoro yaani hawajiamini wao kwa wao. Usishangae wakimuona mwarabu hata mtoto wanamwakia. Ni mkoa wangu ila kuna baadhi ya maeneo wananichukiza sana. Bora kilombero iwe mkoa tuhamie mkoa mpya wa kilombero maana kule wameamka
Mimi natoka ukoo wa wamangala, ni ukoo mdogo masikini miongoni mwa koo za kiluguru
Ona! Wa ukae longa! Tatizo nzala, nzala!