JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
IGP Camillus Wambura ametoa maagizo hayo kutokana na watu wawili kuuawa kwa silaha za moto na wawili kujeruhiwa wakati Polisi wakizuia vurugu Kijiji cha Ikwambi Kata ya Mofu, Wilaya ya Kilombero, Oktoba 23, 2022.
IGP Wambura amesema “Nimeunda Tume Huru kuchunguza vurugu zinazotokea, lengo kujua nguvu iliyotumika kama kudhibiti ilikuwa inaendana na uhalisia, askari wote waliohusika wakae kando na ikibainika kuna uzembe au mapungufu hatua za kisheria zitachukuliwa.”
Awali, ilidaiwa baadhi ya wananchi walichoma moto ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Mofu ikielezwa hawaridhishwi na maamuzi yanayotolewa na viongozi wakati wa utatuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji.
Pia soma: Morogoro: Wananchi wachoma ofisi ya kijiji Kilombero, wawili wauawa