Morogoro: Mpangaji afungiwa ndani Saa 27 na Mmiliki wa nyumba kwa madai ya kukiuka Notisi ya kuhama

Pascal njoo huku umsaidie wajina wako, hii itakuwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wananchi.
 
Yan umeshindwaje kuielewa hoja yangu? Hoja ni kwamba mpangaji hawezi kufanya maamuzi ya ni lini alipe na ni kwa namna gani malipo hayo yatakuwa.
Halafu inakuwa mkuu; Yan Tatizo lilikuwa linasubiri ili lijitokeze wakati mpangaji anapotakiwa alipe kodi?? Kiustaarabu hatukatai tatizo linaweza kujitokeza; lakini Mlipaji/Mpngaji katika hali ya kawaida huenda kumwona mwenye nyumba na kujieleza na sio kumkwepa au kufanya uhuni. Kwani huyo Mpangaji hana namna au vyanzo vingine vya kupata fedha ili akalipe kodi??
Ukiona wewe mpangaji umebanwa sana kifedha ni vyema ukajinyenyekesha kwa mwenye nyumba hata kama itakubidi uweke rehani baadhi ya vitu vyako ili uendelee kujiaminisha na kusubiriwa hali iwe nzuri.
 
Mkuu; Nilisahau hapo juu kukuambia kwamba Hakuna pesa ndogo. Kodi ya nyumba ni pesa kama pesa nyingine kwenye biashara. Kama ingelikuwa ni pesa ndogo si angelipa chap' sio mpaka afungiwe ndani kama utumbo.
 
Nimemwachia Kodi ya miezi 3 hajanilipa na bill ya maji ya miezi 6 nimelipia mwenyewe. Ili mradi tu aniachie gofu na pagale langu nifugie hata njiwa itanilipa.
Mkuu; Ulitumia Utaratibu gani katika kufanya hayo? i.e. Uliwashirikisha akina nani e.g. uongazi wa mtaa/kitongoji/kijiji ili iwe ni ushahidi dhidi ya Ukorofi wake au ulifanya kimya-kimya kama ulivyomfungia humo ndani kimya kimya?? (Utani lakini au ni kwa kicheko; Ukataji gogo ilikuwaje mkuu?
 
Niliamua kuwa mpole tu aondoke. Sipendi shari. Au ningeng'oa bati si eti
 
Hakuna haja ya kung'oa bati lakini sheria ingembana alipe malimbikizo na halafu kuondoka kwa hiari bila shuruti.
Tambua, mimi ni tukio lingine sio Morogoro alikofungiwa huyo kamanda, ila ni kweli, mpangaji wangu nilimruhusu andoke na deni la miezi mitatu na bill ya maji ya miezi 6, KIROHO safi, sijui balozi, au mashahidi sikutaka.
 
Ukilipwa kodi kwa haraka hakikisha pia nyumba inakarabatiwa, maji yapo na unatoa notice stahiki ukitaka mtu ahame
Yeah. Haki iendane na Wajibu. Mwenye nyuma awajibike kwa yale yanayompasa ili kuhalalisha Malipo ya kodi na Mpangaji naye alipe kodi ili kwa kodi hiyo kumwezesha mwenye nyumba atimize yale yanayostahili.
 
Na wewe una m
Angekuwa Salum au Asha kafanya hivyo, tungeipata Waislam wote humu JF na Tanzania nzima.

Lakini kwa kuwa kafanya kondoo mwenzao wa kilimanjaro, wote kimyaa.
Na wewe una majini kama vile Shehe Sule anasema waislam na hata mtume alikua na majini!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…