imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Morogoro ni namba moja, hilo nadhani halina mjadala.Ni mtu wa morogoro huyo,kina Hamisi gaga, fikiri magoso, n.k
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Morogoro ni namba moja, hilo nadhani halina mjadala.Ni mtu wa morogoro huyo,kina Hamisi gaga, fikiri magoso, n.k
Ahahaha,mkuu uliishi Moro mitaa gani,Ni mkoa mzuri sana na wenye vipaji lukuki lakini naungana na MINOCYCLINE hapo juu kwa hoja alizotoa maana ni ukweli mtupu,japokuwa vipaji ni kweli vipo aisee maana tukiangalia nyanja hizi tunapata jibu...
1.Kisoka...
Ukiachana na timu za Dar Morogoro inafuatia kuwa na timu nyingu zilizowahi kutwaa taji la ligi kuu nazo ni Mtibwa Sugar na Mseto ukiachana na Tukuyu stars ya Mbeya hakuna mkoa uliowah kufanya hivyo hapa Tz..na kuna timu ilikuwa inaitwa reli "kiboko ya vigogo" Simba na Yanga zilikuwa hazitoki zikicheza na timu hii
Morogoro ni nyumba ya vipaji vya soka tangu zamani Kina Mohamed Msomali,Malota Soma,Zamoyoni Mogella,Charles Boniface Mkwasa(alilelewa na dada yake mtaa wa karume Morogoro tangu akiwa kijana mdogo) na wengineo magwiji wa zamani,kwa sasa wapo kina Mkude kibabage,Dickson Job,Aishi Manula,Kelvin wa Genk,Shomari Kapombe,Kibwana Shomari n.k
2.Ngumi
Hakuna asiyejua kwamba ukitoa Dar Moro ina ufalme wake katika ngumi Francis Cheka,Cosmas Cheka,Twaha Kiduku,Mandonga na wengine kibao wanatoka Moro
3.Muziki
Zamani watu dansi walikuwa wanalifuata Moro kutoka dar kuja kuwaona Cuban Marimba ya Salum abdallah na baadae Juma Kilaza na Moro Jazz ya Mbaraka Mimi Mwishehe,,Wasanii wa Moro kwa sasa ni Rich Mavoco,Jay Melody,Belle 9,Dayna,Conboi,Tundaman na wengineo hata Salam, Babu Tale wanatokea Moro
Mwandishi wa comment hii aliishi Moro kuanzia 1982-1993
1.SumaleeTunaongelea talent kuanzia 1961 mpaka leo hebu wataje?
Kigoma unaiacha wapi?Mkoa wa morogoro ndio tunu ya sanaa, burudani na michezo. Huo mkoa umetoa vipaji adhimu na adimu sana na ndio tegemeo kubwa kwa taifa kwenye kuzalisha burudani na michezo.
Hapo Morogoro wametoka akina Albert Mangwea, mbaraka mwinshehe, twaha kiduku, francis Cheka, shomari kapombe n.k.
Huwezi kwa sasa Tanzania kuulinganisha mkoa wa morogoro kwenye burudani na michezo na mkoa wowote ule hata kigoma bado ipo mbali na itasubiri kwa morogoro
Miaka ya tisini tulikuwa tunaenda uwanja wa jamuhuri kuangalia mpira,Sasa tunakuwa hatuna pesa ya kiingilio, tukawa tunapenya kwenye mifereji ya kutolea maji nje ya uwanja, tulikuwa na hatari, Kuna mshkaji mmoja alivunjikaga mguu, alipanda ukuta wa uwanja kwa nje hili aingie ndani ya uwanja, eeh bwana hile anamaliza ukuta kwa ndani akachezea virungu vya Askari akajikuta amedondokea Tena nje na kuvunjika miguu,Morogoro ni namba moja, hilo nadhani halina mjadala.
Linapokuja suala la burudani hususani muziki, Kigoma iko sayari ya 7 kutoka sayari ya Tanzania.
Tangu huko nyuma kuna wasanii wengi nguli kama akina Bichuka n.k, hivyo vyovyote utakavyo linganisha, Kigoma hailinganishwi na mkoa wowote.
Ni sawa uilinganishe Mbeya na mkoa wowote kwenye masuala ya Ukristo(uimbaji wa Gospel, idadi ya nyumba za ibada n.k), hapo unakuwa unajilisha upepo maana ina watu ngulii haswaa kibao ambao mikoa mingine hawapo.
Hata Fifa pia ilizaliwa Morogoro.Morogoro jazz band
Ilianzishwa mwaka 1930 ndio band yakwanza Tanzania nzima na ndio chimbuko la band zote Tanzania. Mziki ulizaliwa morogoro na mpira ulizaliwa morogoro wengine wote wanafata.
Vipaji gani? Vya kama wakina Thomas Edson?Mkoa wa morogoro ndio tunu ya sanaa, burudani na michezo. Huo mkoa umetoa vipaji adhimu na adimu sana na ndio tegemeo kubwa kwa taifa kwenye kuzalisha burudani na michezo.
Hapo Morogoro wametoka akina Albert Mangwea, mbaraka mwinshehe, twaha kiduku, francis Cheka, shomari kapombe n.k.
Huwezi kwa sasa Tanzania kuulinganisha mkoa wa morogoro kwenye burudani na michezo na mkoa wowote ule hata kigoma bado ipo mbali na itasubiri kwa morogoro
😂😂😂 Msanii mkubwa ni afande Sela nakutajia vijana wa ngumi wawili Tena wadigo wakipigana nje mwakinyo na Salim mtangoMwenye listi kamili ya Morogoro kuanzia kwa akina Hayati Mbaraka Mwinshehe tunaomba aiweke hapa.
Kipaji kakipatia umakondeni au morogoro?Lakini pia ni vizuri kuangalia na asili zao wanakotokea je! ni wazawa wa Moro au maana kama hao akina Francis cheka hao ni wamakonde
Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
1.Tanga international bandAccumen Mo nitajie band kongwe Tanzania kuliko moro jazz band!