Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Tatizo ile ya kwanza alifunga ya mke mmoja. Yeye angetalakiana na ndipo angefunga hii mpya.
Lakini hii haifanyi adaiwe fidia. Prof kama wakati wa kufunga hii ndoa mpya alidanganya kuwa hajaoa, basi anakuwa na kosa la jinai na sio la madai (la kudaiwa fidia)
 
Hivi kumbe ugoni unaweza kudai fidia na ukalipwa?
mama amechemsha huyo, hakuna kundi lenye michepuko kama mahakimu, majaji na mawakili. Hiyo kesi wataitupilia mbali. Amepeleka kesi ya mbuzi kwa machui...kwa kumhurumia watamwambia adai talaka kisha mali walizochuma na mumewe zigawanywe
 
Ukifunga ya pili ile ya kwanza inakuwa valid sawasawa na hii ya pili ambayo tayari inakuwa imefungwa, ndo maana ndoa zinatangazwa ili kama kuna aliye na pingamizi aweke, ikishafungwa inakuwa notolee hiyo.....
Hapana mkuu, kama ile ya awali ilikuwa ni ya mke mmoja, hii ya pili inakuwa batili hata kama haikupingwa.
 
Lakini hii haifanyi adaiwe fidia. Prof kama wakati wa kufunga hii ndoa mpya alidanganya kuwa hajaoa, basi anakuwa na kosa la jinai na sio la madai (la kudaiwa fidia)
Huwezi jua mke aliharibikiwa vipi baada ya kujua mme kafunga ndoa nyingine bila kumpa yeye talaka. Hiyo jinai nayo ni kesi nyingine.
 
Ukifunga ya pili ile ya kwanza inakuwa valid sawasawa na hii ya pili ambayo tayari inakuwa imefungwa, ndo maana ndoa zinatangazwa ili kama kuna aliye na pingamizi aweke, ikishafungwa inakuwa notolee hiyo.....
Hapana,kwenye vyeti vya ndoa huwa kuna viboksi vya kujaza ,kama ndoa ya mke mmoja ama wake wengi. Sasa kama alitick ya mke moja hapo akioa bila takala ni kosa.

Kwa Tanzania since hakuna mfumo base ,mtu anaweza kuoa/kuolewa hata mara mia na akapewa cheti kabisa. Maana hakuna base ile mtu akiingiza tu jina anaona ulishaoa.
 
Kuoa Mke mwingine kinyume na mkataba kumbe ni nini?

Wewe ni mweupe haya mambo,Sasa Kwa taarifa Yako hata kama hujaoa Kwa Cheti kabisa Cha ndoa na ukamuacha wa awali ukaoa mwingine anakushitaki vizuri na mashahidi ni majirani wenu ndio utaona moto..

Unatakiwa ujue Kwa sehemu kubwa Sheria za mahusiani zinawalinda wanawake na Watoto,mwanaume huna chako.
Hata na wewe mwenyewe ni mweupe, na bush lawyer tu. Ungekuwa mweusi, usingekuwa chawa wa mama.
 
Jiandae kulipa fidia!
Fidia ya nini MADAM T ? Kwani Prof. Katelekeza watoto? Kwanza kabisa ugoni between two consenting adults sio offence Tanzania. Cigarete atafute tu wa kumtuliza. Toto la Marangu lilishamzidi mbinu za kulea wahenga.
Namtakia cigareti maisha mema ya u single. Na Kama Hana mvuto imekula kwake.
 
Back
Top Bottom