Morogoro: Watu 22 Wamefariki dunia kwenye ajali ya Basi la Ahmed linalofanya safari kati ya Tanga-Mbeya. Limegongana na Lori

Morogoro: Watu 22 Wamefariki dunia kwenye ajali ya Basi la Ahmed linalofanya safari kati ya Tanga-Mbeya. Limegongana na Lori

Hadi tutakapoamua kuukubali ukweli!!
Chanzo kukubwa cha ajali za Tanzania ni ubovu wa miundombinu na si mwendokasi kama tunavyoaminishwa na mamlaka za juu.
Head on collisions hata tupunguze speed limit iwe 40km/h bado kuna sehemu korofi zitasumbua
Highway ni vichochoro alafu zina mashimo na rasta hapo lazima zikutane uso kwa uso tu.
 
Dereva wa Lori ndio chanzo kumbe.
Kamanda wa polisi ndo kadai hivyo, alihama ku overtake bodaboda..........unaendesha lori utadhani unaendesha crown, kwamba ku overtake linakuwa ni jambo rahisi tu.
 
Hadi tutakapoamua kuukubali ukweli!!
Chanzo kukubwa cha ajali za Tanzania ni ubovu wa miundombinu na si mwendokasi kama tunavyoaminishwa na mamlaka za juu.
Head on collisions hata tupunguze speed limit iwe 40km/h bado kuna sehemu korofi zitasumbua
Sio tuu speed,ni upuuzi kuendesha kwenye barabara single carriage on opposite lanes.

Tuanze kujenga dual carriage roads
 
Kamanda wa polisi ndo kadai hivyo, alihama ku overtake bodaboda..........unaendesha lori utadhani unaendesha crown, kwamba ku overtake linakuwa ni jambo rahisi tu.
That boils down to miundombinu ya barabara ambalo ni jukumu haswa la Tanroad
Unaporuhusu bajaji bodaboda and the likes zitumie njia moja katika safari zake , clearly usalama unakua sio kipaumbele chako.
 
Wenye mikataba na kizimu wameshika madaraka ,kafara za ajali Tena zimeanza...
Tulisha sahau hzi Mambo.
Ajali za barabarani hazijawahi kupungua , sema kuna kipindi media zilifumbwa mdomo .
 
pengine hapo una mipango kibao ila yote imepelea hewani ndani ya sekunde tu

mlale salama
 
Ajali mbaya maeneo ya Mzumbe maiti ni nyingi.

Walioko Mzumbe tujuzeni basi la Mbeya.

UPDATE:

1). Basi la kampuni ya Ahmed Coach linalofanya safari Kati ya Tanga kuelekea Mbeya, limepata ajali maeneo ya Sangasanga Mkoani Morogoro muda si Mrefu, chanzo na Habari zingine tutatoa baada ya uchunguzi kufanyika.

UPDATES;

2). Watu 13 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ahmeed baada ya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likisafirishwa kwenda nje ya nchi lenye namba za IT 2816 katika eneo la Melela Kibaoni Barabara kuu ya Morogoro-Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Fortunatus Muslim amethibitisha kutokea kwa ajalim hiyo.

UPDATES;

3). Morogoro. Vilio na simanzi vimesikika kila kona katika eneo la Malela Kibaoni wilayani Mvomero, Morogoro kufuatia ajali iliyohusisha basi la abiria na lori la mizigo.

Katika ajali hiyo, watu kadhaa wamejeruhiwa wakati lori lenye namba za usajili za IT 2816 lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda DR Congo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ahmeed lenye namba za usajili T732 ATH.

Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema ajali hiyo imetokea leo saa 10.30 jioni na kusababisha vifo vya watu 16.

Kamanda Muslim amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori hilo kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki maarufu bodaboda hivyo, kupoteza mwelekeo na kukutana na basi hilo uso kwa uso.

Kwa mujibu wa Kamanda Muslim, basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam. Miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Hata hivyo, Kamanda Muslim ametahadharisha kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa kuwa, kazi ya uokoaji bado inaendelea kwenye eneo hilo.

View attachment 2155660View attachment 2155661
View attachment 2155663
View attachment 2155702
So sad news. Why is this happening? My sincere condolences.
 
Aisee...kweli hakuna ajuae kesho....marehemu walikuwa na mipango mingi sana,sasa imekuwa ndoto
Hakuna kabisa ajuaye kesho. Hata wahanga wa iyo ajali walikuwa wanasoma na kuona ajali zingine zikitokea kama sisi humu hawakujua maskini hata wao watakumbwa. As long as tunaumia vyombo vya moto tujue tu hata sisi ni watarajiwa tu. Piga picha kwa familia zao na wapendwa wao sasa hivi wanavyopitia wakati mgumu. Na waliojeruhiwa maumivu wanavyopitia. Mungu hatusaidie tu kuepukana viburi vya afya na uzima
 
Back
Top Bottom