JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Zaidi ya Watoto 100 wa Kitongoji cha Maloweke Wilayani Gairo wamekwama kupata elimu ya shuleni licha ya kuwa na umri wa kwenda shule kutokana na kukosekana kwa shule katika eneo wanaloishi.
Inaelezwa shule za karibu zipo umbali wa kilometa 11 kutoka eneo, hali inayowapa ugumu Watoto kutembea kwenda vijiji vya jirani kwa ajili ya kusoma.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabir Makame ameagiza Halmashauri kuhakikisha wanapeleka mwalimu eneo hilo baada ya wazazi kukamilisha zoezi la ujenzi wa madarasa ili Januari 2023 watoto waanze kupata elimu.
Chanzo: Azam TV