Morogoro: Zaidi ya Watoto 100 wakosa elimu kutokana na kitongoji kukosa shule

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Zaidi ya Watoto 100 wa Kitongoji cha Maloweke Wilayani Gairo wamekwama kupata elimu ya shuleni licha ya kuwa na umri wa kwenda shule kutokana na kukosekana kwa shule katika eneo wanaloishi.

Inaelezwa shule za karibu zipo umbali wa kilometa 11 kutoka eneo, hali inayowapa ugumu Watoto kutembea kwenda vijiji vya jirani kwa ajili ya kusoma.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabir Makame ameagiza Halmashauri kuhakikisha wanapeleka mwalimu eneo hilo baada ya wazazi kukamilisha zoezi la ujenzi wa madarasa ili Januari 2023 watoto waanze kupata elimu.

Chanzo: Azam TV
 
Nchi hii jamani. Bado tuna visa vya hivi kweli? Sasa V8 za nini kama kuna watu hawaendi shule kisa tu hakuna madarasa na walimu?
 
Back
Top Bottom