Morrison huru kujiunga na Simba SC, kamati yasema mkataba wake na Yanga una mapungufu

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411


Baada ya vikao nenda rudi kwa siku takribani 3 hatimaye TFF wamejitokeza na kusema kuwa wamefikia uamuzi baada ya vikao vizito

Mchezaji raia wa Ghana, Bernard Morrison amepewa uhuru wa kujiunga na Simba Sc baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kusema kuwa Mkataba wake na Yanga Sc una mapungufu.

Pamoja na Yanga kuwasilisha picha wakati Morrison anasaini mkataba, kamati imesema inafanyia kaza nyaraka na picha haitoshi kuthibitisha.

Kuhusu fedha, Morrison amekiri kupokea dola 25,000 kisha kupokea 5,000 nyingine ambazo amesema atazirejesha Yanga.

> Morrison alisaini kujiunga na Simba Sc akitokea Yanga


==========

 
Morison yupo huru sawa, kwa nini anapelekwa kamati ya maadili?
 
Maamuzi yametolewa kuwa Morrison ni mchezaji halali wa Simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…