Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Hawa jamaa walifanya hii michezo yao ya kihuni kwenye serikali za mitaa watu wakakaa kimya, sasa wanajaribu tena kuifanya na uchaguzi mkuu, wasijidanganye, hapa mambo hayatakuwa kama serikali za mitaa, CCM twendeni kwenye uchaguzi tukashindane, mnaogopa nini?!

Nyie si huwa mnajiita chama dume, kumbe ni majike tu.
 
Sasa mkurugenzi kakosea nini hapo?

Wewe unapewa fomu kisha unasem ni feki halafu unataka uirudishe kwa aliyekupa fomu feki tena.

Huyo jamaa wanayemuita katibu analisauti likubwa tu na anaongea saana ila kichwani hamna kitu.

Hata mimi nisingeipokea...nenda kqnishtaki nimekupa fomu feki...ili nishtakiwe kwa kujaribu kukurubuni.
Ukiwa kiongozi unaendeshwa kwa sheria na taratibu huku busara na hekima vikikuongoza.

Huwezi fanya mambo kama upo kijiweni.
 
Kwangu logic itakataa nitakapo msikia mkurungezi akisema aliwapa wagombea wengine fomu zisizo fanana bila sababu maalum mkuu.

Kwa hiyo wagombea wa vyama vingine hawajarudisha! Je, zimepokelewa au wanasubiri uteuzi kisha waambiwe fomu zao ni feki.

Uteuzi haupo mbali tusubiri tuone...maana kwa maelezo ya mwenyekiti wa CDM sio CDM tu waliopewa hizo fomu...hata NCCR.

Je, NCCR wamesharudisha? Zimekubaliwa? Tusubiri kwenye uteuzi.

Wakati wa uteuzi itasemekana fomu zao sio sahihi.
 
nyambafu mlifikiri chadema itakufa kwa kuwanunua wakina jua kali,pokea fomu tuwanyooshe
 
Wagombea wa CHADEMA Moshi wakataliwa kupokelewa fomu zao na Mkurugenzi

Huu ujinga niliutarajia sana tu, kama kuzitoa hizo fomu ni kwa mbinde basi kwenye kuzirudisha ni lazima figisu zitakuwepo sana tu na hata wakizipokea bado wagombea wengi wa upinzani wataenguliwa tu
 
Huyo Mkurugenzi kwa nini hawezi kutoa majibu kwa mambo rahisi anazunguka tu?
 
Tanzania kuwa na DEDs kama huyu hakika maendeleo tutayaona kwenye runinga. Mbabaishaji sana sana.
 
Lililopo..

Nimekupa fomu kisha ukasema ni feki...

Nonsense!!

Tuko kwenye hali mbaya sana kama bado tuna mifumo ya kijima namna hii. Hukusikia habari ya “watermark”? Hiyo kitu iko kwenye original document TU. Kama hatuwezi kuwa na haki kwenye hatua ya mwanzo hivi - kwenye kupiga kura, kujesabu na kutangaza marokeo itakuwaje?

Ni hilo ni mwanzo tu, ngoja utasikia sababu za form kutokukubaliwa baada ya 26/08. Namba ya simu, nukta, NA badala ya N/A, form feki, risiki feki nk. Ukiona mkurugenzi anasema “hapa ni mjini, kila mtu anaweza kuchonga muhuri” ujue ni hatari sana. Hatukupaswa kuwa hapa baada ya miaka zaidi ya 50 ya uhuru!!
 
Huu ujinga si wa kuachwa upite bure, natamani wahanga eneo husika watoe somo ujinga huu ukome.
 


CHADEMA wataka TUME YA UCHAGUZI kumuondoa msimamizi wa uchaguzi Moshi Vijijini ambaye ni mkurugenzi wa wilaya Castory Msigala kwa vile hawana imani naye kutokana na matendo na mienendo yake ktk kazi ya kusimamia mchakato mzima wa kuelekea katika kufanyika uchaguzi mkuu ulio wa haki na huru oktoba 2020.

Mfano fomu walizopewa CHADEMA zinautofauti mkubwa na zile fomu walizopewa wagombea wa CCM.

Risiti kwa ajili ya malipo walizopewa CHADEMA kwa ajili ya fomu zinautofauti na risiti walizopewa CCM kwa ajili ya kufanyia malipo.

Mkurugenzi amekiri fomu zina utofauti na mkurugenzi hana uwezo wa kutambua fomu halali au la.

Chanzo: Mwananchi digital

kataeni kabisa huyo mkurugenzi , ikiwezekana fanyeni jambo la kukumbukwa milele
 
Sasa mkurugenzi kakosea nini hapo?

Wewe unapewa fomu kisha unasem ni feki halafu unataka uirudishe kwa aliyekupa fomu feki tena...
Sawa Daby, lakini Wewe Yanga, utakubalije goli la Kagere?! Wewe fisi(em) hukumu kondoo inaachaje kuwa kifo?! Swala hili huwezi kuhukumu kwa haki wakati Wewe ni ccm mboga mboga! (sitakutendea haki nkisema ccm damu damu!!)
 
Upinzani hakuna kukata tamaa, mbele kwa mbeleeeee.
 
Chadema ujuaji utawaponza sana. Fomu amewapa yeye lakini na vyama vingine vimepewa. Kwanini nyinyi ndio munaona mumeonewa?. Hao wengine wanasemaje? Kama kuna hofu ya hivyo kwanini musiende wote kwa pamoja na vyama vingine kulitatua hilo suala?
 
Bado kuna majinga hayaoni kuna shida nchi hii!!
Kwenye nukta ya Mkurugenzi kukataa fomu, namuunga mkono kwa asilimia zote. Mtu yeyot mwenye akili timamu hawezi kukubali hilo, yaani udai fomu ni feki, kisha unirudishie tu, nipokee, hili haliwezekani kabisa, lazima uthibitishie hicho unachokidai, kisha mengine yaendelee.
 
Back
Top Bottom