Lazima kuwe na team special ku deal na majanga; moto, floods, tetemeko. Haya mambo si ya kumuachia Mungu peke yake ... kujiongeza ni muhimu
Mbona hiyo timu ipo, Soma Sheria ya wakala wa usimamizi wa maafa, 2014
7.-(1) Kutakuwa na Baraza la Usimamizi wa Maafa Tanzania.
(2) Baraza litaundwa na wajumbe wafuatao-
(a) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya
Usimamizi wa maafa ambaye atakuwa
Mwenyekiti;
(b) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye atakuwa Makamu wa Mwenyekiti;
(c) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
(d) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya mamlaka na tawala za mikoa na serikali za mitaa;
(e) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na fedha;
(f) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na afya na ustawi wa jamii;
(g) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
mawasiliano;
(h) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
mazingira;
(i) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
Kilimo; na
(j) Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Hali ya
Hewa Tanzania.
Kwenye makaratasi kila kitu kipo🤣