Moto warudi tena Soko Kuu la Kariakoo

Moto warudi tena Soko Kuu la Kariakoo

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
IMG_20210711_215817.jpg

Inasemekana moto umerudi tena Soko kuu la Kariakoo, bado zoezi la uzimaji moto katika Soko hilo linaendelea baada ya sehemu ambazo zilizimwa moto kufuka moshi na kuanza tena.

SOURCE: ITV
 
Huduma za uzimaji moto kwa kweli sisi bado ni kitendawili, kwa kweli unahitajika msasa wa nguvu. Na huku kusua sua hakujaanza leo, ni miaka na miaka
Siyo huduma za moto peke yake ni kila kitu. Imagine mtu ndiyo umepata heart attack au stroke. Ambulance mpaka ikakufikie ni kazi. Na ikifika si ajabu ikawa mbovu au ikaishiwa mafuta njiani.

Na paramedics waliomo humo wanaweza wasije na kifaa hata kimoja. Kwa hizi huduma aisee wenzetu huko duniani wametuzidi sana. Moto kama huo dakika 5 tu wameshafika na mamitambo ya kila aina. Hata huwa sielewi tatizo letu ni nini yaani.
 
Lazima kuwe na team special ku deal na majanga; moto, floods, tetemeko. Haya mambo si ya kumuachia Mungu peke yake ... kujiongeza ni muhimu
Mbona hiyo timu ipo, Soma Sheria ya wakala wa usimamizi wa maafa, 2014

7.-(1) Kutakuwa na Baraza la Usimamizi wa Maafa Tanzania.
(2) Baraza litaundwa na wajumbe wafuatao-
(a) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya
Usimamizi wa maafa ambaye atakuwa
Mwenyekiti;
(b) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye atakuwa Makamu wa Mwenyekiti;
(c) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
(d) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya mamlaka na tawala za mikoa na serikali za mitaa;
(e) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na fedha;
(f) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na afya na ustawi wa jamii;
(g) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
mawasiliano;
(h) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
mazingira;
(i) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
Kilimo; na
(j) Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Hali ya
Hewa Tanzania.
Kwenye makaratasi kila kitu kipo🤣
 
Siyo huduma za moto peke yake ni kila kitu. Imagine mtu ndiyo umepata heart attack au stroke. Ambulance mpaka ikakufikie ni kazi. Na ikifika si ajabu ikawa mbovu au ikaishiwa mafuta njiani. Na paramedics waliomo humo wanaweza wasife na kifaa hata kimoja. Kwa hizi huduma aisee wenzetu huko duniani wametuzidi sana. Moto kama huo dakika 5 tu wameshafika na mamitambo ya kila aina. Hata huwa sielewi tatizo letu ni nini yaani.
Na ndugu alipelekwa temeke Hosp akaambiwa anatakiwa akimbizwe muhimbili dah wakesema gari/ambulance hadi ijae ndiyo wapelekwe kwa ujumla
 
View attachment 1850015
Inasemekana moto umerudi tena Soko kuu la kariakoo, bado zoezi la uzimaji moto katika Soko hilo linaendelea baada ya sehemu ambazo zilizimwa moto kufuka moshi na kuanza tena.

SOURCE:ITV

Inasikitisha sana ,yaani management ya fire yote inatakiwa kufukuzwa kwa uzembe huu tena.
 
Back
Top Bottom