Mpaka leo najiuliza, ilikuwaje mpaka Magufuli akawa Rais?

Kwani mkuu hujarudishwa kazini au kulipwa marupurupu vyeti feki walizuia ajira za wengi!
 
Makosa ya magufuli ni kutetea rasilimali za Tanzania kupiga vita mafisadi na kuwafukuza wenye vyeti feki na hizi ni kelele za vibaraka wa mafisadi
Kama alifukuza vyeti feki mbona hakumfukuza bashite?
 
Hii ni baada ya ccm kuogopa kupasuka hvyo wakaamua watafute mtu ambae hana watu katika chama ndo wakampata huyo mwehu
 
Mkuu haya umeorodhesha hapa hayakupi room ya kuona mtu ni mbaya.
Learn kupokea vitu positive hata kama havijakufurahisha as long as haijaondoa uhai wako.

Mzee aliwahi kutwa na dhahama flani kazini,uongozi wa mtawala flani,alikuwa manager,tulikipitia sana,sikuwahi msikia analaani au kuzidi kulaani yule mtawala.
Alifika mbali sana baada ya pale.


kumbe ilikuwa njia ya kumvusha.

Maisha hayako hivyo,kila mtawala ana makando kando yake na mazuri yake.
 
2005 mliteleza wapi?
Issue kubwa nliyoona kwa Magufuli ni Mafisadi na Vyeti Feki. Wewe utakuwa kwenye vyeti fake. Nakuelewa lazima iwe hivi kwako. Mimi aliniathiri kwenye ufisadi. Tukiungana hapo badamu batamwagika.
 
Wewe nae vp?Kufanya maendeleo katika nchi kuna upinzani wa mabeberu!!Jk alijenga shule za kata nchi nzima,sio maendeleo?Alinunua mabasi ya mwendo kasi,magufuli akaja kuyafungua,sio maendeleo?Aliunganisha mikoa yote kwa lami isipokuwa kigoma na mtwara,sio maendeleo?Jk alifanya hayo yote na mengine mengi,hao mabeberu hawakwepo?Mbona hawakumpinga?Na mbona aliyafanya yote hayo bila kuua na kutisha watu?Leo maendeleo yanafanywa kwa kasi.Vituo vya afya nchi nzima,madarasa ya kisasa nchi nzima,n.k.Mabeberu hapo? Mbona hawapingi?Magu wenu alikuwa na kasoro kichwani,kubali usikubali.Yaani kujenga reli hadi uue mtu,ukataze mikutano ya kisasa,uwazibe watu midomo!!Ni wazi alikuwa na kasoro kichwani.Au alikuwa mshirikina.Washirikina hawawezi kujenga ghorofa bila kuua mtu, hawawezi kujenga kiwanda bila kuua,hawawezi kujenga shule bila kuua,n.k.Sasa mtu wa namna hiyo ni tatizo kupewa nchi.Angefanikisha kuifanya Tanzania kama ulaya basi watanzania tungebaki milioni 10 tu.Wengine tungekuwa tumetolewa kafara.
 
Hata Yesu tunaamini alikuwa mtu mwema kabisa lakini Wayahudi walimkataa na kumkejeli huyo ndio hulka ya binadamu

Any way ulimjua Magufuli akiwa raisi tu au tokea yupo wizara ya uJenzi?

Maana kama Kuna tunzo ya mawaziri waliopita wizara ya ujenzi kihaki kabisa hiyo tunzo ilitakiwa apewe Magufuli

Na hata kama Kuna tunzo ya maraisi waliopita pia kihaki inatakiwa apewe Magufuli
 
Unaongea kinyume chake nahisi
 
Wewe ni nani katika hii nchi?

Kinyangarika tu hata ubalozi huna!

Magufuli alikuwa rais wa nchi na amiri jeshi mkuu, na nafurahii aliwapelekea moto mpaka mkaamua kumdondosha. [emoji1787]

Chuma kinaliaa chumaa HA HA HA chumaa! Weweeee!!
Na aliwanyoosha mpuuzi yule hahaha hawawezi pona majeraha Ni ngumu mno, anapiga Kama netanyahu vile
 
Ilikuwa VITA VYA PANZI {jasusi} vs {Rafiki}...
matokeo yake KUNGURU{jiwe}AKAPATA MLO.
 
Ilikuwa VITA VYA PANZI {jasusi} vs {Rafiki}...
matokeo yake KUNGURU{jiwe}AKAPATA MLO.
Hiyo vita ingweza kuendeshwa kistaarabu na rais mstaarabu, na tukapata matokeo chanya.
Mama Samia anaendelea vema ingawaje amezungukwa na watu wa Magufuli.

Magufuli alitumia njia za kuwaangamiza maadui physically, lakini hata waswahili husema, auaye kwa upanga ataangamizwa kwa upanga.
Au kwa wahindi wanasema KARMA!
 
Uoga wa JK bwana white hair angechukua nchi......hapo tuuu
 
Kauwa wangapi?
Kwani sasa hivi watu hawafi?. Kwani wakati wa kikwete waatu hawakutekwa na kuuwawa.. Au ulikuwa mdogo?

Utofauti wa JPM na wengine ni kutogawa Asali tu. JPM alitaka pesa zote ziende kwenye maendeleo ila wanasiasa na wanaharakati wakawa wanataka wapewe mafungu. Kitu ambacho sasa hivi wanapewa na wanagombana wenyewe kwa wenye. Watu wengi tu wanatekwa na kufa alkini kelele ni chache kwa sababu ya asali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…