Watumishi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA Kwa vyeo vya chini tuna hari ngumu saana tunaomba Jamii forums mtusaidie kupaza sauti kwenye platform zenu zote ili kero hii iweze kuwafikia Viongozi.
Tangu mwaka 2020 tulibadilishwa kutoka mfumo wa utendaji kazi wa kiraia na kuwa katika mfumo wa kijeshi lakin Cha kushangaza mpaka sasa takribani Miaka mitano hatupewi staiki zetu kama majeshi mengine kama ilivyo Kwa TAWA, Ngorongoro Magereza, Uhamiaji, Police n.k, stahiki kama Ration, Vinjwaji, hakuna tunalipwa posho Kwa mfumo wa OC ambapo kwa kiasi kikubwa wanaojilipa pesa nyingi ni Viongozi tu Askari wa chini tunakadiliwa.
Mfano, Hifadhi ya Taifa Nyerere Tunakadiliwa TSH 280,000 ambayo tunakaa baada ya miezi 4 ndipo tunapewa hyo pesa.
Kwahiyo, Hali ni ngumu na inapelekea kushusha morali ya kufanya kazi pamoja na kushawishika kujiingiza kwenye uharifu ama rushwa, Tunaomba serikali kupitia Wizara yetu pendwa ya maliasili ituangalie tupo kwenye mazingira magumu na tunafanya kazi ngumu ya kujitoa uhai kwaajiri ya kulinda rasilimali za Taifa hili kwaajiri ya kizazi Cha sasa na kijacho.
Tunaomba MH Waziri Dkt Pindi Chana, Raisi wetu mpendwa Dkt Samia suluhu Hassani atuangalie tunafanya kazi usiku na mchana mvua yetu, jua letu kwaajiri ya kuzilinda hizi maliasili lakini Wizara yetu ni kama imetusahau.
Bodi ya wakurugenzi ni kama wametusahau hii transformation ya kutuingiza kwenye mfumo wa malipo ya kijeshi kama Ration na Pesa za vinywaji inachukua muda mlefu kwasababu Viongozi wetu wa TANAPA wanajuwa wao ni wanuafaika wa malipo ya OC kwahiyo tukienda kwenye ration tutalingana kitu ambacho wao hawapendi wanaangalia matumbo Yao tu wakati watendaji wakuu ni sisi.
Tatizo jingine ambalo linatukumba ni kwamba TANAPA inalipa mishara watumishi wake Kwa kuchelewa mnoo yaani hakuna mwezi TANAPA imewahi kulipa mishahara watumishi wake kuanzia tar 25 kushuka chini kama ilivyo Kwa taasisis nyingine na mashilika ya kiselikali, je Nini kimejifiacha kwenye hili ?? TANAPA kulipa watumishi wake mishahara tar 30 kwenda mbele mpaka wakati mwingine malipo ya Mishahara kuvuka mpaka mwezi mwingine tar 1 mpaka 5 ndio mnalipwa.
Watumishi Kwamfano hifadhi ya Taifa Nyerere tunadai pesa za malipo ya likizo, Pesa za malipo ya Nyumba tangu mwaka 2025 mwezi 11 mpaka Leo ni miezi 5 lakin hakuna malipo yeyote je familia zetu zinaishije ?? Mishahara inalipiwa tar 30, hakuna posho Wala malipo yeyeote hapo katikati wakati huo kiongozi anakutuma kazi mjini, au kijijini na unatakiwa kutumia huohuo mshahara kutekeleza majukumu ya mwajiri hivyo tunajikuta pesa yote ya mshahara inaishia kutekeleza majukumu ya mwajiri huku familia zikitaabika.
Asanteee naomba kuwasilisha na kuwaomba ndugu zetu Jamii forums kama mlivyo jitoa kuwa sauti ya wanyonge basi mtusaidie kutupazia sauti hii changamoto ambayo inatukumba Watumishi wa TANAPA ikiwezekana hata kuja kufanya mahojiano ili msikie kero zetu Kwa Askari wa rank za chini mkiwahoji Viongozi makamishna na ma officer hamtopata ukweli watauficha maana wao ndio wanuafaike na haya mateso yetu 🙏