Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

mkuu aanza wewe
amenitoa mbali mno,
kumbuka nilienda kugombea ubunge kwa mara ya kwanza nina tsh laki5 pekee mfukoni. ugumu niliokumbana nao alinionyesha njia na kunifanyia wepesi nikavuka salama, fedheha na aibu nilizopitia ni Mungu pekee alinifuta machozi na kunipa ujasiri wa kutokukata tamaa, bidii na nguvu za kupambana bila kuchoka....

naamini huyu Mungu aliona na alijua nia na dhamira ya Moyo wangu kwa wanaichi, na hata akanishika mkono.....

Mpendwa,
leo hii, hivi nilivyo ni kwa Nguvu ,Neema na Baraka za Mungu tu , na wala sio kwa ujanja wangu...

tuendelee kumuamini, kumshukuru kwa sadaka na shukrani, kumtumaini, kutubu na kuambatana nae, na daima tumtegemee yeye pekee, kwani anaweza yote katika wote wamwaminio 🐒
 
so wewe ni mbunge
 
Cha kwanza kuniumba mwanaume Cha pili kunijalia kuipata riziki kwa wepesi kwani sihangaiki kuipata kama watu wengine
 
Kwanza kabisa, thibitisha Mungu yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…