Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Mimi siku zote namshukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kutambua uwepo wake na kumtegemea yeye katika kila jambo, Hakika Mungu ni wetu sote.
 
Kumponya mama yangu mzazi, kwa kweli Mungu yupo namshukuru sana na utukufu wake nitautangaza popote.
Wagonjwa wanaokufa ndugu zao hawamuombi huyo Mungu awaponye?

Mama yako ana u special upi wa kusema Mungu kamponya?

Au huyo Mungu ni mbaguzi anaponya watu kwa ubaguzi na upendeleo kwa kuruhusu wengine wapone halafu wengine wafe ilhali wote mnamuomba awaponye?
 
Mimi siku zote namshukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kutambua uwepo wake na kumtegemea yeye katika kila jambo, Hakika Mungu ni wetu sote.
Kwa hiyo huyo Mungu alitoa uwezo wa kutambuliwa uwepo wake na watu wachache kama wewe, Halafu anataka kila mtu amtambue yeye yupo?

Huyo Mungu kama ni wetu sote, kwa nini atambuliwe na watu wachache kama wewe, halafu atoe uwezo wa kutambuliwa uwepo wake na watu wachache kama wewe?

Huyo Mungu, Alishindwaje kutoa uwepo kwa kila mtu akamtambua yeye yupo siku zote kwa wakati wote?
 
Kwa kuniletea Mume bora Maishani mwangu.
Huyo Mungu Alikuletea mume bora wapi?

Au ni juhudi zako binafsi zilikufanya umpate huyo mume bora?

Wanawake wangapi wanamuomba huyo Mungu wapate waume bora na hawapati?

Au huyo Mungu ni mbaguzi na mwenye upendeleo kwa kukupa mme bora wewe tu, ilhali kuna kundi kubwa la wanawake linamlilia kuomba waume bora?
 
Back
Top Bottom