Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

amenitoa mbali mno,
kumbuka nilienda kugombea ubunge kwa mara ya kwanza nina tsh laki5 pekee mfukoni. ugumu niliokumbana nao alinionyesha njia na kunifanyia wepesi nikavuka salama, fedheha na aibu nilizopitia ni Mungu pekee alinifuta machozi na kunipa ujasiri wa kutokukata tamaa, bidii na nguvu za kupambana bila kuchoka....

naamini huyu Mungu aliona na alijua nia na dhamira ya Moyo wangu kwa wanaichi, na hata akanishika mkono.....

Mpendwa,
leo hii, hivi nilivyo ni kwa Nguvu ,Neema na Baraka za Mungu tu , na wala sio kwa ujanja wangu...

tuendelee kumuamini, kumshukuru kwa sadaka na shukrani, kumtumaini, kutubu na kuambatana nae, na daima tumtegemee yeye pekee, kwani anaweza yote katika wote wamwaminio 🐒
Kwahiyo Mheshimiwa, wamwaminio mungu ni vinyani na vingedere na vikima au sio?!... Hiyo emoji uliyomalizia nayo hapo inamaana gani?!

Ujue una utani sana Mheshimiwa?! 😂😂😂
 
Huyo Mungu Alikuletea mume bora wapi?

Au ni juhudi zako binafsi zilikufanya umpate huyo mume bora?

Wanawake wangapi wanamuomba huyo Mungu wapate waume bora na hawapati?

Au huyo Mungu ni mbaguzi na mwenye upendeleo kwa kukupa mme bora wewe tu, ilhali kuna kundi kubwa la wanawake linamlilia kuomba waume bora?
Mbona umeandika comment ya kunifokea hivi kwa kweli sitajibu maswali yako mpaka utakapo weka chochote kitu tumboni (chai)
 
Mbona umeandika comment ya kunifokea hivi kwa kweli sitajibu maswali yako mpaka utakapo weka chochote kitu tumboni (chai)
Huwezi kujibu maswali yangu, kwa vile huyo Mungu unayesema amekupa mume bora ni uongo tu.

Ni juhudi zako binafsi ndizo zilikupatia huyo mume bora wako wala si huyo Mungu.

Kuna kundi kubwa la wanawake linamlilia na kumuomba huyo Mungu wapate waume bora lakini hawapati.

Automatically huyo Mungu wa kutoa mume bora hayupo, ni juhudi zako binafsi ndizo zilikupatia huyo mume wako bora.
 
Ni lipi hasa ungependa kupata uthibitisho kulihusu? Au unataka umuone Mungu kwa macho yako kabisa?
Thibitisha huyo Mungu ni nini?

Ulijuaje yupo?

Unathibitishaje yupo?

Na si hadithi na mawazo yenu ya kufikirika tu mliyo aminishwa na kukaririshwa na dini zenu.
 
Thibitisha huyo Mungu ni nini?

Ulijuaje yupo?

Unathibitishaje yupo?

Na si hadithi na mawazo yenu ya kufikirika tu mliyo aminishwa na kukaririshwa na dini zenu.
Kueleza kuhusu Mungu pasipo kutumia vitabu vyake haiwezekani. Kama huamini ni maamuzi yako tu mkuu, be free with your Reasoning and humanist beliefs.
 
Back
Top Bottom