Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Anhaa, sawa hapo nimeelewa vyema kabisa, Mungu akubariki kwani umenijuza jambo jipya kabisa.
At least Mungu huyo angekuwepo angeweza kunibariki na kubariki kila kitu.

But unfortunately Mungu huyo hayupo kunibariki au kubariki chochote.

Mungu huyo ni dhana ya kufikirika tu, isiyo katika uhalisia.

Imaginations just an illusion.
 
Kwahiyo Mheshimiwa, wamwaminio mungu ni vinyani na vingedere na vikima au sio?!... Hiyo emoji uliyomalizia nayo hapo inamaana gani?!

Ujue una utani sana Mheshimiwa?! 😂😂😂
Mungu hafanani na wala hafananishwi na chochote...

hata hivyo gentleman,
sijakupata vyema unalalamika au unazungumzia nini hasa? vinyani, vingedere au emoji? 🐒
 
Kama huamini sasa nithibitishe kipi ambacho utaamini, unataka niiandike maneno mengi tu bila sababu, baki na imani yako ya HUMANISM.
Uthibitisho si suala la kuamini, ni suala la kuhakiki.

Kuamini tu unaweza kuamini hata uongo.

Sasa, uthibitisho unaangalia na kuchambua hiyo imani, je, unachoamini ni kweli au uongo?

Wewe unahakikishaje kwamba imani yako kuwa Mungu yupo ipo kwenye ukweli kwamba Mungu yupo, na si imani iliyojengwa kwenye uongo, kwamba Mungu hayupo?
 
Mungu hafanani na wala hafananishwi na chochote...

Ulijuaje na unathibitishaje, Mungu huyo hafanani na hafaninishwi na chochote?

ilihali hata kuthibitisha kwamba huyo Mungu yupo huwezi.
hata hivyo gentleman,
sijakupata vyema unalalamika au unazungumzia nini hasa? vinyani, vingedere au emoji? 🐒
 
Huwezi kujibu maswali yangu, kwa vile huyo Mungu unayesema amekupa mume bora ni uongo tu.

Ni juhudi zako binafsi ndizo zilikupatia huyo mume bora wako wala si huyo Mungu.

Kuna kundi kubwa la wanawake linamlilia na kumuomba huyo Mungu wapate waume bora lakini hawapati.

Automatically huyo Mungu wa kutoa mume bora hayupo, ni juhudi zako binafsi ndizo zilikupatia huyo mume wako bora.
nafsi na moyo wako vikiwa tayari kutambua na kuskia wito wa sauti ya Mungu katika maisha yako, ni rahis kupata utakacho kwa hakika na kwa wakati muafaka , na kwakweli utadumu nacho kwa amani na furaha sana 🐒

ukitumia nguvu na utashi wako mwenyewe binafsi bila kukiri nguvu na uwezo uliona nao ni Neema na Baraka za Mungu utatangatanga sana, utababaika mno na unaweza kufanikiwa na ukose furaha na amani kwa ulichofanikiwa bila kumshirikisha Mungu.....

hata hivyo ni hiyari na uamuzi wako kuchagua Nuru au Giza 🐒
 
Uthibitisho si suala la kuamini, ni suala la kuhakiki.

Kuamini tu unaweza kuamini hata uongo.

Sasa, uthibitisho unaangalia na kuchambua hiyo imani, je, unachoamini ni kweli au uongo?

Wewe unahakikishaje kwamba imani yako kuwa Mungu yupo ipo kwenye ukweli kwamba Mungu yupo, na si imani iliyojengwa kwenye uongo, kwamba Mungu hayupo?
Huo ni mtazamo wako na mawazo yako, mimi sina cha zaidi mkuu.
 
nafsi na moyo wako vikiwa tayari kutambua na kuskia wito wa sauti ya Mungu katika maisha yako, ni rahis kupata utakacho kwa hakika na kwa wakati muafaka , na kwakweli utadumu nacho kwa amani na furaha sana 🐒
Nimeshapata nitakavyo na napata chochote nitakacho mwenyewe bila msaada wowote wa huyo Mungu.

Huyo Mungu hayupo kutoa chochote.
ukitumia nguvu na utashi wako mwenyewe binafsi bila kukiri nguvu na uwezo uliona nao ni Neema na Baraka za Mungu utatangatanga sana, utababaika mno na unaweza kufanikiwa na ukose furaha na amani kwa ulichofanikiwa bila kumshirikisha Mungu.....
Nimeshafanikiwa vitu vingi sana bila huyo Mungu.

Na watu wengi sana wamesha sali sana kumuomba huyo Mungu lakini bado hawajapata kitu, kwa vile Mungu huyo hajawahi kuwepo na hayupo kutoa chochote.
hata hivyo ni hiyari na uamuzi wako kuchagua Nuru au Giza 🐒
At least Nuru na giza vipo. Ila huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Uhai na afya
Kwamba hutakufa sio na hutakaa uumwe?

Au siku ukifa au ukiumwa huyo Mungu atakuwa amesahau majukumu yake.

Au utakuwa umesahau kumshukuru huyo Mungu unayedai anakupa uhai na afya?

Je waliokufa na wanao umwa mahospitali unadhani hawakuwa wanamshukuru huyo Mungu kwa uhai na afya kabla hawajaanza kuumwa?
 
Ulijuaje na unathibitishaje, Mungu huyo hafanani na hafaninishwi na chochote?

ilihali hata kuthibitisha kwamba huyo Mungu yupo huwezi.
ni nafsi hai iliyoko na nguvu za kipekee sana na isiyo na sura wala mfano wa kitu, na inafanya kazi ya pekee sana ndani ya kila mwanadamu mathalani wew unae ona, unaeandika, unaehoji na pengine kubisha makuu ya Mungu aliyokukirimia bure kwa mapenzi yake kwako....

kwamba eti unataka kuthibitishiwa uhai ulio nao kama ni kwa Neema na Baraka za Mungu 🤣

hana hasira hata ukimkana kwamba akili, nguvu na utashi ulio nao ni kwa Neema zake, lakini wew unadai ni zako....

hata ukihisi njaa,
akili na utashi vinavyokusukuma utafute chakula ni wako mwenyewe na si Mungu...
Hakasiriki bali atakusamehe bure tu 🐒
 
Back
Top Bottom