Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Mpaka sasa unamshukuru Mungu kwa jambo gani kuu alilokutendea maishani mwako?

Cha kwanza kuniumba mwanaume Cha pili kunijalia kuipata riziki kwa wepesi kwani sihangaiki kuipata kama watu wengine
Umerithishwa kiwanda nini ndugu much know... Au unaibia watu mtandaoni, TIGOPESA na SELCOM...
maana hiyo kauli ya

"riziki kwa wepesi, kwani sihangaiki kuipata kama watu wengine"

Inatia mashaka kwa mwenye akili... Au una chuma ulete? 😂🙌
 
Mkuu nimerudi, ibada ilikuwa ndefu kdgo.

Hapo juu umeandika vizuri sana, kweli kabisa yeye ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo na upendo kwa wote.
Mkuu,

Sijaandika yeye ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote.

Nimeandika Mungu huyo hayupo.

Wewe hujui kusoma.

Na huo ni uthibitisho mwingine Mungu hayupo.

Angekuwepo, ungejua kusoma kwa ufahamu.
 
Mkuu una muda tuzungumzie niliyo jifunza wakati nimeenda ibadani?
 
Hata mabaya, maovu na mateso sio?
Mabaya, maovu na mateso ni matokeo ya dhambi, na kwa kuwa tunaishi katika Ulimwengu wa dhambi nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, neema na rehema zake kwani hata nyakati za magumu bado alinipa amani ya moyo na ujasiri wa kushinda.

Hivyo ntamshukuru daima kwa kila kitu. Thank you Jesus🙏🏿
 
Kwanza anza kuthibitisha Mungu yupo, unataka kunifundisha habari za ibada ya Mungu ambaye hata kuthibitisha yupo hujathibitisha?
Mkuu, humu tunatumia maandishi, sasa kama ni uthibitisho lazma niuweke kimaandishi.

Na uthibitisho huo ni kwamba Mungu yupo, whether you accept it or not.
 
Achilia mbali zawadi ya uhai, afya na maisha aliyokujalia na bado anakukirimia wewe na mimi bure bila malipo wala gharama yoyote....

Nafahamu, Mungu amekutendea mambo mengi mno maishani mwako, na huenda ukiulizwa kuyasema, kwasababu ya muda na ufinyu wa platforms, usimalize kuyaorodhesha yote...

Hebu mbele ya hadhara hii ya familia ya wanaJF,
Shuhudia matendo mema na makuu ya Mungu kwa uchache, alioyokutendea maishani mwako, ili kwa pamoja kama watoto wa Mungu, tushuhudie sifa na utukufu wake kwa watoto wake katika ulimwengu huu....

Neema na Baraka za Mungu, ziandamane na kuambatana nawe daima, katika familia yako, kazi na majukumu yako ya kila siku daima na milele....

Amen..
Asee ni pumzi jombaaa..
 
Uliyeandika uzi huu ukiuliza hili swali; uko hai?
 
Back
Top Bottom