DOKEZO Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Shida hapo wewe upo position mbaya sana, akikamatwa lazima mwenye nyumba nawe ukamatwe, sasa usipokamatwa watajua wewe ndio umewachoma...Israel...
Mtafute Masauni uongee nae
 
Kwenye mkataba wa kupangisha nyumba nafikiri Kuna kipengere kinamukataza mpangaji kutofanya shughuli zozote tofauti na kukaa, na siyo godown au kiwanda. Chukua mtendaji, police na Mwanasheria wako. Fukuza huyo kwa kuvunja masharti ya mkataba. Huyo atakuwa mchaga wengi ndo zao kutengeneza pombe fake

View: https://youtu.be/yJmml9e7eFs?si=NQwXk--fLOB_J_gK
Angalia yanaweza kukuta kama huyu mzee kupangisha mtu bila kujua historia yake, kafanya mauwaji uko na wakati huo anakaa kwenye nyumba yako, unaunganishwa kwenye case ya kunyongwa.
 
Hii dunia haiko fair kabisa jamani eee watumishi tufanye biashara tuwe madon Sasa ona mwamba kajenga ila kajamaa kamemlipa hela ya miaka miwili kakenua meno yote kisa Kodi ya Miaka miwili .

Kimbembe mwamba ana kiwanda ndani ya nyumba na kaweka na ulinzi kwanini wewe mwenye nyumba usiwe mtumwa ? Hapo mwanangu wewe mfuate huyo mkemia mchane unahitaji nyumba yako maana unarejea dasalam ila mpe hela iliyobaki lakini akitoka tu ,fika ofisi ya mjumbe na balozi pamoja na mtendaji waeleze kilichokuwa kinaendelea na nini uliamua kufanya ili uwe salama .

Maana hata ukimuamisha sio kwamba tutaacha kuja kuchukua posho hapo ,ni lazima tutakuja tu kikubwa ni nyumba ile ile .
 
mjinga wewe, sasa unaleta huku ni polisi au mjumbe?
 
Nenda ukaripoti Polisi hilo jambo

Ukizembea Siku Moja Zitakuja Mamlaka husika za Serikali kama vile TBS/TMDA n.k ambapo Kwa Sheria iliyopo,

Wanaweza kutaifisha mitambo pamoja na Mali zote ikiwemo hiyo nyumba yako wakiamini ni sehemu ya Mali za hao waharifu kumbe hao jamaa hiyo nyumba wamepanga kwako tu
 
Chagua la kufanya:-
  • Muuzie hiyo nyumba
  • Muite mzungumze kama mwanzoni alivyokufuata na mkaingia mkataba (hakikisha hapa usiwe peke yako), na umpatie utaratibu wa kuhama kama ataendelea kuzalisha vinywaji.
  • Tafuta mwanasheria akushauri kwenye hili jambo
 
...Nilivyojitambulisha getini Mlinzi hakufungua geti alinizuia kuingia(imagine nyumba yangu lakini nazuiliwa kuingia).... Nijuavyo mimi nyumba ukiikodisha/ ukimpangia mtu maana yake kwa kipindi cha huo mkataba nyumba inakuwa kwenye utawala wa mpangaji kwa maana ya masharti mbalimbali kuhusiana na hiyo nyumba. Otherwise kuna kitu nimejifunza kwenye hili...
 
Watataifisha nyumba kwani iko chini ya Jina lao? Wewe umepangisha, yanayoendelea hapo huna udhibiti nayo, tena akijua umemshtaki unaweza shitakiwa kwa kusababisha au kuvunja mkataba kabla ya muda mliokubaliana.
 
Mtafute yule mmiliki wa smart gin..ni bilionea yule ila anapatikana kirahisi sana.. mwambie kuna gin zinatengenezwa hapo kwa nyumba Yako na uyo mpangaji..I hope atakusaidia sana na unaweza pewa na nyumba nyingine bure sabb anawatafuta sana watu wanaoharibu biashara zake!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…