Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Kaka Paskali, bado ninataka kuwa na heshima na wewe. Mada yako ni ndefu sana lakini nitajikita kwenye kichwa cha habari. Nauliza tu, ndio hawa hawa ambao mvua ikipotea huwa mnawaita kufanya sala?? Ndio hawa mnawatumia katika kuelimisha jamii kuhusu ushoga, uasherati na hofu ya Mungu?? Ndio hawa hawa mnawatumia kuomba dua katika shughuli mbalimbali za kijamii?? Je ndio hawa hawa ambao taasisi wanazozimiliki kama mahospitali, shule na vyuo ni muhimu katika jamii?? Ndio hawahawa mnawatumia katika kampeni za chaguzi mbalimbali ili kupata kura??

Ni jambo lipi hasa ni la Mungu na lipi ni la kaisari?? Mimi nasema kila kitu na kila mtu na mamlaka aliyonayo - ni vya Mungu. Na dini inaonga maisha ya waamini katika mambo mengi. Uongo, wizi, si mambo ya kiimani???

Tunajenga taifa la hovyo sana! Taifa ambalo nafasi ya kiongozi wa serikali ni sahihi na inatoka kwa kiumbe mkamilifu!! Nilidhani ungetumia muda na nafasi kujibu hoja badala ya kushughulika na hoja inatoka kwa nani. Smart people talk about issues!!
Mkuki kwa nguruwe. Wanapolihitaji Kanisa huliita. Linapowapa ukweli huligeuka. Hoja za Maaskofu zijibiwe
 
Tuanzie hili .Je bunge hili ni wananchi????walilichagua??? Unajua alieliweka Mungu alimhukumu nini??Je kwa maneno haya ya kinafiki ili upate umaarufu kwankusoma nyakati .sisi wadogo zako bado tukikuona tukwambie shikamoo?? Naujibu toka moyoni mwako na MUNGU ataekuhukumu akusikie.Maneno umeandika ww ila tunaoaibika ni sisi wadogo zako

Kwani hata huo mkataba wa Muungano nani aliupigia kura ??
 
Kaka Paskali, bado ninataka kuwa na heshima na wewe. Mada yako ni ndefu sana lakini nitajikita kwenye kichwa cha habari. Nauliza tu, ndio hawa hawa ambao mvua ikipotea huwa mnawaita kufanya sala?? Ndio hawa mnawatumia katika kuelimisha jamii kuhusu ushoga, uasherati na hofu ya Mungu?? Ndio hawa hawa mnawatumia kuomba dua katika shughuli mbalimbali za kijamii?? Je ndio hawa hawa ambao taasisi wanazozimiliki kama mahospitali, shule na vyuo ni muhimu katika jamii?? Ndio hawahawa mnawatumia katika kampeni za chaguzi mbalimbali ili kupata kura??

Ni jambo lipi hasa ni la Mungu na lipi ni la kaisari?? Mimi nasema kila kitu na kila mtu na mamlaka aliyonayo - ni vya Mungu. Na dini inaonga maisha ya waamini katika mambo mengi. Uongo, wizi, si mambo ya kiimani???

Tunajenga taifa la hovyo sana! Taifa ambalo nafasi ya kiongozi wa serikali ni sahihi na inatoka kwa kiumbe mkamilifu!! Nilidhani ungetumia muda na nafasi kujibu hoja badala ya kushughulika na hoja inatoka kwa nani. Smart people talk about issues!!

Hivi lini serikali iliwaita maaskofu wakasome sala ya mvua , si wanaamua wenyewe ??
 
Ushauri wangu wa bure kwa Rais Mama Samia, kama hawa Maaskofu Katoliki wamewasilisha sauti ya Mungu wa kweli, uzoefu umeonyesha sio vizuri kuwakatalia Maaskofu, na mfano mzuri ni ushauri huu niliompa rafiki yangu Benard Membe
 
umesoma sheria lakini huna akili. yaliyo ya mungu apewe mungu na yaliyo ya kaisari apewe kaisari haikumaanisha kwamba wao hawana uhuru kutoa maoni yao. hata Yesu aliwasema mapolisi/serikali ya kipindi kile kuacha rushwa na kutosheka na kipato chao. na kwa taarifa yako, sababu kubwa na Yesu kusulibishwa ilikuwa kupinga serikali ya kipindi kile na walimwona kama mpinzani anayekuja kumpindua herode. na ndio maana watu wanahisi kuna rushwa imetembea ndio maana mnatetea sana huu mkataba, mwarabu kawalambisha pesa? toshekeni na mishahara yenu. lini utapata akili pasco?
Ungesoma bandiko lote ,ungeelewa P ,amemanisha
 
Wanabodi,
Declaration of Interest
Mimi ni Mkatoliki, tena sio Mkatoliki mlei tuu, ni miongoni mwa Wakatoliki wacheche waliokwenda kuhiji Israel, na waliofika St. Peter's Basilica, Rome, Italy, nikiwa mdogo nimehudunu utumishi kanisani chini ya Muadhama Laurian, Cardinal Rugambwa, na nimemhudumia Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Nimelisoma tamko hili, News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu in disbelief, hili kweli ni tamko la TEC, au tamko la Fr. Kitima?. Naulizia, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Kama Mama Samia ndiye Mkuu wa nchi, ameikubali DPW, ameileta, Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, na kuridhia ile IGA ya DPW, CCM ndio chama tawala na chama pekee cha Watanzania, wameikubali DPW, mhimili wa Mahakama umeikubali DPW, kwa kuipiga chini kesi ya kupinga DPW, who the hell is TEC ikatae DPW?!.

Si wengi wanajua kuwa kila rais wa JMT anapokuwa ni Mkristo ni lazima awe Mkatoliki!, Nyerere alikuwa Mkatoliki, Mkapa Mkatoliki na Magufuli Mkatoliki, na abatenfuatia Mama Samia ni lazima awe Mkatoliki!, je kuna uwezekano Wakatoliki wamedekezwa na sasa wameota pembe na kuthubutu kumgomea Mama kwasababu sio Mkatoliki?.

Tuambiane ukweli, jiulize, rais angekuwa ni MkatolikinMagufuli ndio ameileta hii DPW, TEC wangetoa waraka huu?.

Kuna mabaya mangapi yamefanywa na marais Wakatoliki lakini TEC wamenyamaza?. Kuna kosa kubwa zaidi ya rais wa JMT kukiuka katiba?. Mbona rais Mkatoliki alikiuka katiba na TEC walikuwepo, mbona sikuona waraka?.

Bwana wetu Yesu Kristo alituasa tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari na tumpe Mungu yaliyo ya Ki Mungu, jee waraka mzito kama huu, haujachanganya ya Ki Mungu na ya Kaizari?.

Pia Bwana wetu Yesu Kristo alituusia tuwe makini sana na manabii wa uongo, niliwahi kuandika hivi humu Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.

Sipingi uhuru wa Maaskofu Katoliki kutoa kutoa maoni yao binafsi kuhusu jambo lolote, lakini maoni ya kupinga jambo lolote la kisiasa yanayotolewa na TEC, ni sawa na amri kwa Wakatoliki wote kuikataa DPW!, kitu ambacho kitawakwaza Wakotoliki wa CCM, Serikali, Bunge na Mahakama, wanao unga mkono DPW, hivyo baada ya tamko hili, wakiendelea kuunga mkono DPW ni kama kwenda kinyume cha msimamo wa Kanisa Katoliki!.

Sina tatizo kiongozi yoyote wa dini akihubiri amani, mimi mwenyewe ile 2010, JK alipokuwa na hali mbaya, nimezunguka nchi nzima na Askofu Moses Kulola kuokoa jahazi Askofu Kulola: Kuna mtandao wa kisiasa makanisani

Niliwahi kuuliza maswali haya kuhusu viongozi hawa wa dini
Hitimisho
Kufuatia waraka huu kunasibishwa na Sauti ya Mungu mwenyewe, kumaanisha Vox Populi is Vox Dei, hii maana yake waraka huu ni sauti ya Mungu wa kweli, na kama hawa Maaskofu Katoliki sio manabii wa uongo, ushauri wangu wa bure kwa Rais Mama Samia, kama hawa Maaskofu Katoliki wamewasilisha sauti ya Mungu wa kweli, uzoefu umeonyesha sio vizuri kuwakatalia Maaskofu, na mfano mzuri ni ushauri huu niliompa rafiki yangu Benard Membe, Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo tangu Membe alipoupuuza ushauri huu,... (naomba nisimalizie), ila hakuchukua round!.

Hivyo mimi nikiwa ni mmoja wa wana jf wenye kauli umba "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia
Nakushauri tuu Mama, pamoja na mema yote DPW waliokutendea during Expo Dubai, and after, kubaliana tuu na ushauri wa TEC, huu ni ushauri Mungu, hili jambo la DPW achana nalo kwa sasa, kisha anzisha upya mchakato wa kumpata a strategic investor wa Bandari yetu kwa kufuata a due process, hakuna strategic investor mwekezaji wa Bandari wa kushindana na DPW!, hivyo DPW atakuwa ameingia kwa heshima, and very honourably.

Paskali.
Rejea za Mwandishi kuhusu DPW na Bandari zetu
  1. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
  2. Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!
  3. Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
  4. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?
  5. Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
  6. DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?
  7. Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?
  8. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  9. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  10. Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!
  11. Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do
  12. Wito: Hoja za Kisheria za TLS, Prof. Shivji na wengine wote kupinga IGA, zisijibiwe Kisiasa kwa maneno matupu!, zijibiwe Kisheria kwa Vifungu!.
  13. Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?
  14. IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria vilaza wa Ajabu. Je, Bunge letu na Serikali navyo ni vya Ajabu?
  15. Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?
  16. IGA ya DPW imetusaidia mambo mengi. Kwanza kuonyeshea tuna wanasheria wa aina gani, pili kuidogosha fani ya sheria na sasa kila mtu ni Mwanasheria?
  17. Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?
  18. Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
  19. Na kufuatia baadhi ya watu wenye akili fupi humu kudhani mimi ni chawa, nawahakikishia mimi sio chawa Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
  20. Chawa hawezi kupandisha bandiko kama hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Kwamba CCM ndiyo chama tawala na chama pekee Tanzania...
Mungu atusadie sana waja wake ! Case closed.
 
Maoni ya kupinga jambo lolote la kisiasa yanayotolewa na TEC, ni sawa na amri kwa Wakatoliki wote kuikataa DPW!, Wakotoliki wa CCM, Serikali, Bunge na Mahakama, wanao unga mkono DPW, hivyo baada ya tamko hili, wakiendelea kuunga mkono DPW ni kama kwenda kinyume cha msimamo wa Kanisa Katoliki!.
 
Baraza la maaskovu haliruhisiwi kutoa kauli (matako) ya kukemea au kuipinga uonevu,unyonyaji na ukandamizaji? Kanisa pia lina kazi ya kutetea haki za wananchi kwa kupaaza sauti linapoona haki zao zinakanyagwa na serikali.

Mkuu Pascal Mayalla ameandika andiko lililoyumba. Maana analysis yake ameponda tamko la Maaskofu. Hitimisho ameshauri Mh Rais Samia akubaliane na Maaskofu. Huku ni kuyumba kiuandishi!

Kimsingi mchango wa Kanisa kijamii hapa Tanzania haupimiki. Ukitizama shule za msingi za kanisa, o level na a level schools, vyuo na vyuo vikuu ambavyo vipo affiliated na kanisa, hapo hatujagusa idadi ya hospital na vituo vya afya, na mipango kedekede ya kanisa kwa Kaya masikini kupitia shirika lake la Caritas. Hivyo ni ngumu sana kutenganisha kanisa na jamii na siasa za Tanzania.

Zaidi ikumbukwe Watumishi wengi (sio wote) wa ngazi za juu Serikalini wamefaidika na mifumo hii ya kanisa. Ndiposa taasisi hii ya kanisa katoliki ina-exert special threat kwa Serikali yoyote iliyopo madarakani.

Itoshe kusema, matawi ya filosofia - Epistemolojia na Ontolojia - ni silaha hatari sana ambazo ndio msingi wa kanisa.

Mkuu Pascal Mayalla amefanya haraka sana kukosoa tamko la Maaskofu. Sio kawaida kwa Pascal Mayalla kuandika ima kukosoa ima kupongeza pasina tafakari ya kina.

Unfortunately, this time around mwandamizi Mayalla ameloa.
 
Wanabodi,
Declaration of Interest
Mimi ni Mkatoliki, tena sio Mkatoliki mlei tuu, ni miongoni mwa Wakatoliki wacheche waliokwenda kuhiji Israel, na waliofika St. Peter's Basilica, Rome, Italy, nikiwa mdogo nimehudunu utumishi kanisani chini ya Muadhama Laurian, Cardinal Rugambwa, na nimemhudumia Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Nimelisoma tamko hili, News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu in disbelief, hili kweli ni tamko la TEC, au tamko la Fr. Kitima?. Naulizia, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Kama Mama Samia ndiye Mkuu wa nchi, ameikubali DPW, ameileta, Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, na kuridhia ile IGA ya DPW, CCM ndio chama tawala na chama pekee cha Watanzania, wameikubali DPW, mhimili wa Mahakama umeikubali DPW, kwa kuipiga chini kesi ya kupinga DPW, who the hell is TEC ikatae DPW?!.

Si wengi wanajua kuwa kila rais wa JMT anapokuwa ni Mkristo ni lazima awe Mkatoliki!, Nyerere alikuwa Mkatoliki, Mkapa Mkatoliki na Magufuli Mkatoliki, na abatenfuatia Mama Samia ni lazima awe Mkatoliki!, je kuna uwezekano Wakatoliki wamedekezwa na sasa wameota pembe na kuthubutu kumgomea Mama kwasababu sio Mkatoliki?.

Tuambiane ukweli, jiulize, rais angekuwa ni MkatolikinMagufuli ndio ameileta hii DPW, TEC wangetoa waraka huu?.

Kuna mabaya mangapi yamefanywa na marais Wakatoliki lakini TEC wamenyamaza?. Kuna kosa kubwa zaidi ya rais wa JMT kukiuka katiba?. Mbona rais Mkatoliki alikiuka katiba na TEC walikuwepo, mbona sikuona waraka?.

Bwana wetu Yesu Kristo alituasa tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari na tumpe Mungu yaliyo ya Ki Mungu, jee waraka mzito kama huu, haujachanganya ya Ki Mungu na ya Kaizari?.

Pia Bwana wetu Yesu Kristo alituusia tuwe makini sana na manabii wa uongo, niliwahi kuandika hivi humu Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.

Sipingi uhuru wa Maaskofu Katoliki kutoa kutoa maoni yao binafsi kuhusu jambo lolote, lakini maoni ya kupinga jambo lolote la kisiasa yanayotolewa na TEC, ni sawa na amri kwa Wakatoliki wote kuikataa DPW!, kitu ambacho kitawakwaza Wakotoliki wa CCM, Serikali, Bunge na Mahakama, wanao unga mkono DPW, hivyo baada ya tamko hili, wakiendelea kuunga mkono DPW ni kama kwenda kinyume cha msimamo wa Kanisa Katoliki!.

Sina tatizo kiongozi yoyote wa dini akihubiri amani, mimi mwenyewe ile 2010, JK alipokuwa na hali mbaya, nimezunguka nchi nzima na Askofu Moses Kulola kuokoa jahazi Askofu Kulola: Kuna mtandao wa kisiasa makanisani

Niliwahi kuuliza maswali haya kuhusu viongozi hawa wa dini
Hitimisho
Kufuatia waraka huu kunasibishwa na Sauti ya Mungu mwenyewe, kumaanisha Vox Populi is Vox Dei, hii maana yake waraka huu ni sauti ya Mungu wa kweli, na kama hawa Maaskofu Katoliki sio manabii wa uongo, ushauri wangu wa bure kwa Rais Mama Samia, kama hawa Maaskofu Katoliki wamewasilisha sauti ya Mungu wa kweli, uzoefu umeonyesha sio vizuri kuwakatalia Maaskofu, na mfano mzuri ni ushauri huu niliompa rafiki yangu Benard Membe, Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo tangu Membe alipoupuuza ushauri huu,... (naomba nisimalizie), ila hakuchukua round!.

Hivyo mimi nikiwa ni mmoja wa wana jf wenye kauli umba "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia
Nakushauri tuu Mama, pamoja na mema yote DPW waliokutendea during Expo Dubai, and after, kubaliana tuu na ushauri wa TEC, huu ni ushauri Mungu, hili jambo la DPW achana nalo kwa sasa, kisha anzisha upya mchakato wa kumpata a strategic investor wa Bandari yetu kwa kufuata a due process, hakuna strategic investor mwekezaji wa Bandari wa kushindana na DPW!, hivyo DPW atakuwa ameingia kwa heshima, and very honourably.

Paskali.
Rejea za Mwandishi kuhusu DPW na Bandari zetu
  1. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
  2. Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!
  3. Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
  4. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?
  5. Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
  6. DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?
  7. Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?
  8. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  9. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  10. Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!
  11. Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do
  12. Wito: Hoja za Kisheria za TLS, Prof. Shivji na wengine wote kupinga IGA, zisijibiwe Kisiasa kwa maneno matupu!, zijibiwe Kisheria kwa Vifungu!.
  13. Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?
  14. IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria vilaza wa Ajabu. Je, Bunge letu na Serikali navyo ni vya Ajabu?
  15. Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?
  16. IGA ya DPW imetusaidia mambo mengi. Kwanza kuonyeshea tuna wanasheria wa aina gani, pili kuidogosha fani ya sheria na sasa kila mtu ni Mwanasheria?
  17. Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?
  18. Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
  19. Na kufuatia baadhi ya watu wenye akili fupi humu kudhani mimi ni chawa, nawahakikishia mimi sio chawa Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
  20. Chawa hawezi kupandisha bandiko kama hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Hebu kidogo fafanua. Kwani Rais anaemfuata mama lazima awe mkristo? Kama ni zamu kati ya wakristo na waislamu basi huo nao ni udini unaleta. Kwani katiba inasema hivyo? Mbona zile zamu za kupishana kati ya mtu kutoka znz na Tz bara siku hizi hamzitaji? mnasema katiba haijaweka zamu lakini kwenye udini mnaashiria kuwe na zamu!
 
Mwandishi mwandamizi na mwanasheria Msomi, ndugu yangu Pascal Mayalla andiko lako hili limeyumba mno. Sidhani kama ulipata wasaa kufanya tafakuri ya kina kabla hujashika kalamu kuweka wino kwenye karatasi.

Kifupi sana, headline ya andiko, analysis yako na hitimisho ulilofikia ni sawa na wasemavyo Wazaramo: zilongwa mbali, zitendwa mbali! Hoja uliyokusudia kufikisha kwa hadhira haieleweki. Ima ulikusudia kuwachanganya wasomaji, faima hadhira imesoma andiko la mwandishi aliyechanganyikiwa.

Vyema upitie upya andiko lako hili walau kuwe na coherence (mtiririko sawiji) wa headline, analytical content na conclusion. Itapendeza!

Nikutakie heri.
 
Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, na kuridhia ile IGA ya DPW, CCM ndio chama tawala na chama pekee cha Watanzania, wameikubali DPW, mhimili wa Mahakama umeikubali DPW, kwa kuipiga chini kesi ya kupinga DPW, who the hell is TEC ikatae DPW?!.
Andaa andiko lingine la kuomba radhi mkuu muungwana akivuliwa nguo huchuntama sasa chuntama omba radhi, 'who the hell is....' unaelewa maana yake omba radhi umewakosea wazee wa baraza
 
DINI KWENYE ELIMU SAWA,NDIO MAANS WANAJENGA SHULE.DINI KWENYE AFYA ZA WANANCHI SAWA, NDIO MAANA WANAJENGA HOSPITAL. DINI KWENYE SIASA ETI NO NO NO NO NO KWANINI???? ILI UHUBIRIWE UELEWE, INABIDI UWE NA UELEWA MZURI( ELIMU) NA AFYA NJEMA. LAKINI PIA LAZIMA IWEPO AMANI. AMANI INATOKANA NA SIASA SAFI. HAPO DINI UTAITENGAJE NA SIASA.MBONA BUNGENI KUNA MAASKOFU NA WACHUNGAJI?
Hata Mimi nashangaa Ila Mambumbumbu wanakataa
 
Maoni ya kupinga jambo lolote la kisiasa yanayotolewa na TEC, ni sawa na amri kwa Wakatoliki wote kuikataa DPW!, Wakotoliki wa CCM, Serikali, Bunge na Mahakama, wanao unga mkono DPW, hivyo baada ya tamko hili, wakiendelea kuunga mkono DPW ni kama kwenda kinyume cha msimamo wa Kanisa Katoliki!.
Well said mkuu!

Zaidi, wakatoliki wakiingia mzigoni, wapwa wao wanaosali jumapili easily wana-join the party! Halafu kwa agenda yenyewe hii ya kuuza rasilimali za nchi, siioni namna Muslems watakataa kushiriki hii sherehe pamoja na Catholics!

Signals mbaya kabisa kwa CCM.
 
Nimesoma tamko la TEC

Kwanza tamko limesomwana mtu mmoja bila kuwepo na askofu mwingine yeyote.

Aliesoma na kuandika tamko amekuwa miongoni mwa watu wanaopinga mkataba wa bandari kwa nyakati tofauti hata kabla ya tamko la leo.
TEC imetumika kama Jukwaa lilisaidia slaa na kitima kufikisha hoja zao.

Rejea mjadala mdaharo uliowashirikisha Rostam,Kitila mkumbo,Zitto,Lema,Shekh Ponda,Balile na Dr Kitima mwenyewe.

Kwenye madaharo watu wote walikubaliana kuhusu umuhimu wa uwekezaji,Kitima pekee ndie alikuwa na hoja tofauti, akasema haoni sababu ya kukabidhi uhuru wetu kwa waarabu,akapinga uwekezaji na kutaka mkataba tuachane nao,tuwaachie vijana wa kitanzania waendeshe,akaongeza kuwa hata wakiiba watatumia pesa hizo humuhumu nchini(ingia youtube andika mdaharo wa bandari utaona ninachokisema)

Leo ameibuka kama katibu wa TEC nafasi iliyowahi kushikwa na Dr.Slaa.

Anatoa tamko kwamba TEC inapinga uwekezaji na wanamuamuru Rais Ufute mkataba.
Kwenye andiko lake ametoa hoja kubwa tatu.

1.Kwenye andiko lake anadai Mihimili iheshimiane,isiingiliwe hapa alimaanisha Kesi ya mwabukusi ambayo kwa vyovyote Kitima alihusika kuifungua .

Kushindwa kwa Mwabukusi ni sawa na kushindwa kwa Kitima,lazima Kitima atafute plan B.

Kitima kwenye andiko lake anasema mihimili isiingiliane,kila muhimili uwe huru.

Kwake anaamini walishindwa kesi kwakuwa mahakama haikuwa na uhuru wa kufanya maamuzi,Kitima ni kama anasema mahakama ilishinikizwa kutoa yale maamuzi.

Halafu anafanya makosa kwenye andiko hilohilo kuhusu hoja hiyo kwa mushinikiza Rais Samia kutengua maamuzi ya bunge ambao ni muhimili mwingine wa dola ambao awali amesema mihimili isiingiliwe.

Hapa anahalalisha kuingiliwa kwa munimili wa Bunge ili kufanikisha malengo yake.

Rais akiingilia bunge atakuwa naendelea kuvunja katiba, kukosea kwa kufanya kile ambacho Kitima anapinga kwenye Tamko lake.

2.Kuhusu hoja ya kutaka Bandari iendeshwe na wazawa,kwamba haijawahi kuendeshwa na wageni,amesahau kuwa Bandari imeendeshwa na TICS kwa miaka 22 hakulisema hili kwa makusudi,huenda anatamani TICS ndio iendelee badala ya DP-World ili kulinda maslahi binafsi aliyonayo bandarini.

Hapa Kitima ni kama ana msalahi binafsi anayoyapigania kwa kutumia mwamvuli wa TEC,hoja yake inamashaka.kumbukeni sakata la ESCROW kuna hadi viongozi wa dini ambao walinufaika na wizi wa ESCROW sio wasafi kwa kiwango hicho.

3.Kitima na Dr.Slaa ni watu wenye Itikadi kali ya ukristo(Udini)

Kuna Wakristo wasiokuwa na ubaguzi halafu kuna Slaa na Kitima waliopea kwenye Udini.

Sio utamaduni wetu Watanzania kunadiliana habari za udini ma Ukabila,lakini kwa muktadha huu nitalisemea ili muwajue vizuri.

kwa nyakati tofauti Kitima ameonesha ni mtu mwenye chuki ya kidini na mdini sana tangu akiwa Makamu mkuu wa chuo cha St Augustine Mwanza.

Nakumbuka wakati wa utawala wa Rais Kikwete kwenye kipindi cha star TV chini ya Dotto Bulendu kitima aliilaumu serikali ya Rais kikwete kwa kuruhusu waarabu wenye ndevu hadi kifuani kuzagaa Kariakoo,alisema kwamba wale wenye ndevu ndio magaidi.kwamba serikali inawatazama haiwachukulii hatua.

Yaani kwenye ule mjadala, kitima akaona ndevu ni tishio kwake.
Ndio maana Tangu utawala uchukuliwe na Rais Magufuli,Mkatoliki mwenzake Kitima hajawahi kujitokeza hadharani kuipinga serikalinya magufulipamoja na chamgamoto zote za Utawala wa Magufuli.

Kadhalika Dr.Slaa,kwenye utawala wa Magufuli hakuwahi kuishambulia serikali kwa lolote hata pale palipokuwa na makosa ya wazi,baadae Slaa alipewa zawadi ya cheo kuwa balozi wa tanzania kwa kazi nzuri ya Kuhujumu demokrasia yetu.

Baadae alirudishwa nyumbani baada ya kumaliza muda wake wakati wa utawala wa Rais samia,hadi hivi karibuni kwenye sakata la mbowe,Slaa alisema mbowe anaweza kuwa gaidi kwamba mashtaka aliyoshtakiwa nayo yalikuwa halali,hapa alitoa kauli ya kumfurahisha Rais samia kwa lengo la kuwinda zawadi ya cheo kipya.
Rais Samia amejipambanua kuwa hataki wapambe,ni kiongozi anaetembea kwenye 4R,msisitizo ukiwa mwafaka wa kitaifa.

Watu kama slaa ambao wanashangilia mauaji na uonevu Rais samia aliona hawawezi kumsaidia.

Pia Rais Samia anaamini katika uongozi wa vijana.Slaa ana zaidi miaka 78.

Baada ya Slaa kukiridhisha kuwa utawala wa Rais Samia hauna mpango wa kumtumia,ndipo akaamua kuungana na Dr.Charles Kitima kuishambukia serikali

Kama Slaa angepewa cheo,muda huu angekuwa anatetea Mkataba wa DP World.

Huu ni uthibitisho kuwa Kitima na Slaa ni wadini sana ambao Kuingia kwa Rais Samia madarakani kwao waliona ni suprise.

Hawakujiadaa kuongozwa na Rais Samia ndio maana Wamekuwa mbogo sio kwenye mkataba wa bandari tu bali kwenye utawala wa Rais Samia kwa ujumla.

Rejea mahojiano ya Slaa na star tv baada ya Rais samia kuapishwa,Slaa aliishambulia serikali na kuituhumu kuhusu kifo cha Rais Magufuli,Slaa akamalizia kwa kusema kama wanataka wanikamate,siogopi kukamatwa.,alionekana ni mtu mwwnye hasira ya kukosa cheo.

Kwa msingi huo,huu ni uthibitisho kuwa Tamko lililoitwa la TEC lina msukumo wa kidini kuliko msukumo wa kisheria na kisiasa.

Nchi yetu ina dini kubwa Mbili,Wakristo na waislaam,tujaalie hilo ni tamko la wakatoliki.

Je na waislaam nao wakitoa tamko lao linalopingana na tamko la TEC?

Vipi walokole nao wakiunga mkono uwekezaji,serikali itafuata msimamo wa dini gani?

Ndio msingi uliosababisha serikali kutamka kuwa haina dini,lengo nikuepuka misuguano inayoweza kuliingiza taifa kwenye machafuko.

Tumeshatoa maoni,serikali imeyasikia na ndani ya serikali kuna watu wa dini zote na wasiokuwa na dini.,kuna wanasheria kuna vyombo mbalimbali vya dola.

Ni imani yangu kuwa Swala la uwekezaji wa Bandari watalifanyia kazi kwa kulinda maslahi ya taifa.

Viongozi wa dini wasiingile utendaji wa serikali ambayo kila mmoja anatambua haina dini.
Tuwapuuze Slaa na kitima,wanataka kutuingiza kwwnye vita yao ya maslahi binafsi kwa Kisingizio cha kulinda rasilimali ,tuulinde umoja wetu uliodumu kwa zaidi ya miaka 50.
Tujifunze Burundi na Rwanda,mauaji ya kimbali yalihamasishwa na viongozi wa dini.
 
Back
Top Bottom