Mpenzi wangu ananisaliti huku naona kabisa

Habar zenu wadau, samahani kwa kuwasumbua kusoma chapisho hili.

Kuna mwanamke niko nae kwenye mahusiano sasa hivi yapata mwezi na kitu, ana mtoto mdogo wa miezi kama 7 hivi. Yeye anakaa na dada yake na wamepanga chumba jirani kabisa na nilichopanga mimi.

Toka tumekuwa kwenye uhusiano aliamua kuhamia chumbani kwangu kabisa. Sasa juzi niliona sms za jamaa mmoja anampongeza kwa walichofanya jana yake na kumuomba warudie tena siku inayofuata. Na mwanamke akakubali kabisa.

Siku iliyofuata yaani jana tar. 1 muda wa kulala ulivyofika, tukalale kama kawaida kwenye saa 5 usiku akaamka akajifanya anampelekea simu dada yake room kwao. Mtoto wake kamuacha kwangu kalala, nikajua mchezo umeanza.

Ilikuwa saa 5 na dakika 37 alivoondoka karudi saa 6 na dakika 30 hivi. Alivyorudi nikasikia mlango wa chumba cha dadake unafunguliwa nikajua anaenda kumfungulia mdogo wake ,nikakimbilia dirishani fasta, kweli nikamuona kasimama mlangoni anasubiri afunguliwe mlango.

Nikajirudisha zangu kitandani, alivokuja nikakausha kama sijui lolote vile. Sikumuongelesha lolote nikamuacha alale. Asubuhi ya leo nimejihimia job, yeye memuacha kalala kitandani kwangu.

Yaani inaniuma sana. Naombeni ushauri wenu wadau.
Huyo fukuza bro!!hakuna kitu hapo,utapata ngoma bule?kama huyo mtoto sio wako,basi bro unatembea na mke wa mtu,au wewe na huyo mwingine ni michepuko tu.
 
Mkuu unahitaji ushauri gani hapo??
Muweke chini mzungumze umchane makavu na kumkanya au kama bado unampenda na kumuhitaji fanya mpango mhame hilo eneo

Halafu unaonekana ni mpole so anakuchukulia poa act as a man acha uboyaaa!

Jitahidi kumkaza vizuri!
 
Achana na huyo mwanamke ambae anashindwa hata kumthamini mtoto wake. Hama hapo haraka sana.
 
Habar zenu wadau, samahani kwa kuwasumbua kusoma chapisho hili.

Kuna mwanamke niko nae kwenye mahusiano sasa hivi yapata mwezi na kitu, ana mtoto mdogo wa miezi kama 7 hivi. Yeye anakaa na dada yake na wamepanga chumba jirani kabisa na nilichopanga mimi.

Toka tumekuwa kwenye uhusiano aliamua kuhamia chumbani kwangu kabisa. Sasa juzi niliona sms za jamaa mmoja anampongeza kwa walichofanya jana yake na kumuomba warudie tena siku inayofuata. Na mwanamke akakubali kabisa.

Siku iliyofuata yaani jana tar. 1 muda wa kulala ulivyofika, tukalale kama kawaida kwenye saa 5 usiku akaamka akajifanya anampelekea simu dada yake room kwao. Mtoto wake kamuacha kwangu kalala, nikajua mchezo umeanza.

Ilikuwa saa 5 na dakika 37 alivoondoka karudi saa 6 na dakika 30 hivi. Alivyorudi nikasikia mlango wa chumba cha dadake unafunguliwa nikajua anaenda kumfungulia mdogo wake ,nikakimbilia dirishani fasta, kweli nikamuona kasimama mlangoni anasubiri afunguliwe mlango.

Nikajirudisha zangu kitandani, alivokuja nikakausha kama sijui lolote vile. Sikumuongelesha lolote nikamuacha alale. Asubuhi ya leo nimejihimia job, yeye memuacha kalala kitandani kwangu.

Yaani inaniuma sana. Naombeni ushauri wenu wadau.
Pole. Kama umehakiki kabisa anakusaliti basi hakuna mpenzi apo.
Kama unaweza hama mtaa kabisa. Kuepuka maneno "yule jamaa anachapiwa"
.
Au kama unakaa hapo hapo mfukuze kwako na utafute mwanamke mwingine.
Aking'ang'ania mwambie muwe friends with benefit tu.
 
Acha uzwazwa tafuta chumba uhame unaomba ushauri wa nini Sasa
 
Kati ya vitu nilinyimwaga uvumilivu ni kusalitiwa waziwazi alooooo!!
Hata uwe unanipa nini sijareeeeee🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮!!
Dada huna Kaba ukijua tu roho inalipuka😂😂
 
  • Thanks
Reactions: ITR
Back
Top Bottom