Ndio maana ndoa nyingi sana za siku hizi zinavunjika ovyo ovyo tena mapema sana.
Kwanza kabisa hayo mambo ya imani mlitakiwa kuyaweka sawa sawa mwanzoni kabisa mwa uhusiano wenu na sio muda huu wa kufunga ndoa.
Pili ni kichekesho kikubwa cha kiimani kwa mtu kuhama imani yake kisa kumpata mwanamke au mwanaume. Imani ya mtu ni zaidi ya ndoa yake. Msilazimishe ndoa kuwa msumari wa kupigiliwa kwenye kila kitu cha kimaisha.
Tatu, ndoa ni jambo la kiimani, huwezi kuitenganisha ndoa na imani, kama imani zenu haziwezi kukubaliana kuhusu ndoa yenu ni vyema msioane wala kulazimisha kuoana maana mtaishia kupoteza kimoja. Sasa ili muweze kupata vyote (ndoa na imani) katika maisha yenu ni vyema mkaachana sasa ili kila mtu akatafute mtu wa imani yake wakuja kuoana naye. Wanawake na wanaume wanaotafuta wachumba wa kuoana wamejaa kwenye jamii, na wengi wako vizuri tu kitabia na kimuonekano, nendeni uko.