nimesikia mvutano bungeni baadhi wakitaka nchi yetu iridhie mkataba wa kuuza bandari kwa miaka sijui 100 na tetezi zinazoendelea baadhi ya wabunge wamehongwa milioni 10 ili wapitishe azimio hilo la kuuza nchi yetu.
nimejiuliza kwanini mwinyi, mkapa, kikwete na hayati magufuli hawakuwahi kuja na uamuzi huu badala yake tumekuwa tukiona mikakati ya kuziboresha tu bandari na zinafanya vizuri.
kiini cha kuuza bandari zetu kwa mwarabu ni nini? ni kushindwa kwa waziri kusimamia tpa? au ni kukosekana fedha za kuboresha? lakini tumeambia kuna zaidi ya trilioni 8 zimepotea kwenye ripoti ya cag kwanini fedha hizo zisingetumika kuboresha bandari?
au kuna nini ambacho watanzania hatukijui.. na je mnadhani watanganyika watakaa kimya mali zao ziuzwe?