Tatizo huu uzi umeingiliwa, yaani badala ya kujadili hoja iliyoletwa kwa mustakabali wa mpira wetu, tunaaza kulingaisha eti ipi bora. Huu ujinga wa usimba na uyanga utatufikisha pabaya.
Sisi mashabiki wa giant teams tupunguzi hisia na uhasama kati ya team zetu, maana tunaonekana wote wajinga kumbe kuna mapung'alo wachache ambao vichwa havina ubongo bali vimejaa makamasi ndo wanaotuharibia mpira wetu.
Hatuwezifika mahali. Mimi pia nimeona magoli yote mawili ya SBS yanakasoro.
Faulo ya penalty: mshambuliaji ali-dive na haikustahili kuws penalty bali kadi ya njano.
Goli la pili: Aliyetoa pasi ya mwisho alikuwa offside wakati anaipokea hiyo pasi. Hivyo mwamuzi msaidizi alipaswa kuamuru offside hata kabla hajatoa pasi ya goal.