Mpwayungu yupo sahihi, hii kazi ya ualimu ni ngumu sana

Kazi gani ni rahisi? Ukiona imekushinda hujalazimishwa unaweza kuacha ukatafuta kazi nyingine

Hakuna kazi rahisi ndugu, lakini hii kazi ina drain akili sana especially ukiwa kwenye taasisi inayobana, amini nakwambia hauwezi kuwa mwalimu competent unless u devote akili yako yote na nguvu katika masomo unayofundisha na usifikirie kitu kingine.

Pia kazi zingine kama kusahisha madaftari, class management, kuandika ma lesson plan, kujaza log books, kusimamia zam etc. Ukumbuke kazi ya ualimu ni kutumia akili 100% sasa unapokuwa na activities zingine zinazokubana bado na personal life issues ni ngumu sana ku focus.
 
Lakini si unalipwa mwisho wa mwezi hilo ndo kubwa ndugu
 
Upo sahihi kabisa kiongoz, kama una ishu ingine mfano business ya kukuingizia hata kipato kidogo achana na hiyo kazi ya laana, naijua vizuri kabla sijaingia kwenye business niliifanya for almost 10 years, a totoal waste of time!
 
90% ya waliochagua ualimu wametoka familia za kawaida ambao walivyutwa na mkopo na ajira za uhakika otherwise hakuna anayependa ualimu ni asilimia chache sana ya watoto wa kishua wanaoenda ualimu kwasababu hakuna future mi siwalaumu walioenda huko ni familia zetu ndio zimesababisha yote hayo hakuna anayependa ada million 3 kwa mwaka ya kam college itatoka wapi.
 
Walimu wanajenga nyumba wanausafiri na maendeleo mengi tuu
 
Advance!?masomo GANI hayo!?

Usi complicate mambo kufundisha simple sana!

TENA advance!unatumia mbinu gani!?au we BADO unatumia teacher centred Ili uwaonyeshe upo deep sio!!?

Mi napiga chemistry na bios ordinary level and never suffocate!!

Ugumu unaufanya wewe mwenyewe!!!

"Easy does it" norman vincent peale!!
 
whatever, hii sio kazi.inatakiwa iwe last option kama umekosa kila kitu ndo uwe mwalimu .
 
Tulishaga wambia lakini hamtaki kuelewa ualimu sio kazi ni utumwa wa mwili na akili, ondoka haraka sana kwenye hiyo kazi ya kitumwa! mke wangu alikaa mwaka mmoja tu akasalim amri ,sasa ivi ameajiriwa sheli kama pump operator vyeti vya ualimu katupa huko.huwa najaribu kumuuliza kimtego ,hiyo kazi ya sheli si ni ngum sana bora urudi kwenye ualimu anasema BORA KUKESHA SHELI KULIKO KUFANYA KAZI YA LAANA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…