Habari za asubui ndugu zanguni,
Nimefanya kazi ya ualimu katika shule x mkoani Dodoma kwa miaka 3 sasa nikifundisha masomo ya A level kwenye shule moja ya private.
Lakini naona kama hii kazi inakua ngumu sana kwangu kuendelea nayo sababu na experience citu vifuatavyo vinavyoniumiza na kunidrain energy yote na morale ya kufanya kazi.
Kwanza nimegundua hii kazi inakugeuza kuwa mwanafunzi kabisa maana unahitaji kusoma mara kwa mara ili uweze kuwa competent katika kufundisha. Sasa hiii ya kusoma mara kwa mara inadrain energy vibaya mno maana kichwa kinahitaji pia kufikiria na mambo mengine ya kimaisha.
Mbaya zaidi vitu tunavofundisha ni ma theory tu kwaiyo unabaki tu kumeza mavitu ili ukayateme darasani lakn haudevelop practical skill yoyote na ukiacha kusoma yanapotea unless uwe umefundisha miak mingi sana ndo material yanastick kichwani.
Pili, Ratiba hasa katika private schools iko so tight unakua na ma vipindi kibao mpaka usiku sometimes. Siku nzima unafanya kazi ya kupiga kelele darasani.
Tatu, kazi ya kukimbizana na wanafunzi, tena hawa ma teenagers ni kazi ngumu sana.
Sijui kama ma teacher wenzangu mmenotice hii kitu kama mimi, Mpwayungu alishaliona hili zamanii sana na kulisemea.