Mpwayungu yupo sahihi, hii kazi ya ualimu ni ngumu sana

Mpwayungu yupo sahihi, hii kazi ya ualimu ni ngumu sana

Screenshot_20230924-144603.png
 
Ukimchukua leo mtoto wa tajiri mmoja ambae alikua anapewa 500k kwaajili ya matumizi yake madogo madogo ya shuleni, ukimpa ajira ya mshahara wa 700k ni lazima ataitukana hiyo kazi na ataiacha haraka sana.

Ila ukimchukua mtoto wa masikin aliekua anapewa matumaini tu kuwa nenda shule nikipata ntakutumia hela ya matumizi na anaondoka akiwa hana kitu ukimpa kazi ya mshahara wa 700k ni lazima ataithamini sana.

Unajua kwanini? Maisha magumu ndo yanatufundisha kuthamani vitu, hakuna anaependa kufanya kazi ngumu.
 
90% ya waliochagua ualimu wametoka familia za kawaida ambao walivyutwa na mkopo na ajira za uhakika otherwise hakuna anayependa ualimu ni asilimia chache sana ya watoto wa kishua wanaoenda ualimu kwasababu hakuna future mi siwalaumu walioenda huko ni familia zetu ndio zimesababisha yote hayo hakuna anayependa ada million 3 kwa mwaka ya kam college itatoka wapi.
A comment with minerals...superb!
 
Umenena vyema umaskini wa ualimu upo kwenye muda,

Ratiba ngumu kufundisha , usome . Nyumbani uandae kazi ya kesho , ujasahisha , ratiba nyingine mpaka jumamosi . Mshahara aungozeki hata mia ,no overtime,kwa nini usife maskini
Kazi gani ya kuajiriwa ina muda? Kila kitu ni mipango lazima ujipe muda wakufanya maendeleo binafsi
 
Habari za asubui ndugu zanguni,

Nimefanya kazi ya ualimu katika shule x mkoani Dodoma kwa miaka 3 sasa nikifundisha masomo ya A level kwenye shule moja ya private.

Lakini naona kama hii kazi inakua ngumu sana kwangu kuendelea nayo sababu na experience citu vifuatavyo vinavyoniumiza na kunidrain energy yote na morale ya kufanya kazi.

Kwanza nimegundua hii kazi inakugeuza kuwa mwanafunzi kabisa maana unahitaji kusoma mara kwa mara ili uweze kuwa competent katika kufundisha. Sasa hiii ya kusoma mara kwa mara inadrain energy vibaya mno maana kichwa kinahitaji pia kufikiria na mambo mengine ya kimaisha.

Mbaya zaidi vitu tunavofundisha ni ma theory tu kwaiyo unabaki tu kumeza mavitu ili ukayateme darasani lakn haudevelop practical skill yoyote na ukiacha kusoma yanapotea unless uwe umefundisha miak mingi sana ndo material yanastick kichwani.

Pili, Ratiba hasa katika private schools iko so tight unakua na ma vipindi kibao mpaka usiku sometimes. Siku nzima unafanya kazi ya kupiga kelele darasani.

Tatu, kazi ya kukimbizana na wanafunzi, tena hawa ma teenagers ni kazi ngumu sana.

Sijui kama ma teacher wenzangu mmenotice hii kitu kama mimi, Mpwayungu alishaliona hili zamanii sana na kulisemea.
Ngoja nichambue matches za jackpot kwanza.
 
Back
Top Bottom