Mpya kutoka kwa Sativa: Mafwele ameendelea kunitafuta, anataka nife, amedai bado hajamalizana na mimi

Mpya kutoka kwa Sativa: Mafwele ameendelea kunitafuta, anataka nife, amedai bado hajamalizana na mimi

Quran imeagiza kuhukumu kwa haki,mfano wako huu ni mfu,ungetumia labda wa wakatoliki,mtoto kalawitiwa na padre kwenda kigangoni kushtaki
Surat Al-Ma’idah (5:8): "Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi wa haki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mtoapo ushahidi msije mkachochewa na chuki za watu kuto hukumu kwa haki. Hukumuni kwa uadilifu, hilo ni karibu zaidi na uchaji Mungu. Na muogopeni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda."

Hapa, Qur'an inawataka waumini wawe waadilifu hata kama wanawahukumu watu ambao huenda wanachukizwa nao. Haki lazima itekelezwe bila kujali hisia za binafsi
 
N
Natamani kujua huyu mafwele ni nani na ana impact gani hapa nchini,kwa sababu huyu kijana ameokotwa amejeruhiwa vibaya kiasi samaia akatoa hela za matibabu na mara zote anatamka aliyemtendea hayo ni huyu mafwele.

Kuna ugumu gani kama kuna uchunguzi unaendelea wakaanza na huyu mtu?serikali inasubiri aumize wengine iseme itamtibu tena?ana uchawi wa nchi gani huyu maana hata kama ameloga basi huo uchawi siyo wa sayari hii.
Nasikia huyo mafwele ndio aliowakimbiza majambazi Arusha,,panyaroad dar na wale wahuni wa mkuranga na kibiti
 
Habarini wanajukwaa,

Siku ya jana, Sativa alikaa kwenye mahojiano na kituo cha habari cha Mwanzo TV Plus.

Katika mahojiano hayo Sativa aliendelea kusisitiza kuwa Faustine Mafwele pamoja na kikosi chake wanaendelea kumtafuta na kwamba Faustine Mafwele anataka afe.

Sativa aliendelea kusema kuwa Faustine Mafwele na genge lake wana-unfinished business naye na kuongeza kuwa iwapo lolote litamkuta basi Mafwele anahusika.

Soma Pia: Kwanini Polisi haijibu tuhuma alizotoa Sativa juu ya Faustine Mafwele kuhusika kwenye utekaji wake?

Hivi Mbowe na team huwa mnafanya nini? Hamuwezi hata kuajiri investigative journalists wabobezi wawaandikie report /documentary ya kuhusu Habari hizi na nyingi nyinginezo; kama ya Lisu, Kibao, ya huyu Sativa, Mbeya nk. Kila kitu mnacho kuwaa-indict hawa washenzi CCM na system yao. Tumieni fursa hizi hawa washenzi waondoke.
 
Habarini wanajukwaa,

Siku ya jana, Sativa alikaa kwenye mahojiano na kituo cha habari cha Mwanzo TV Plus.

Katika mahojiano hayo Sativa aliendelea kusisitiza kuwa Faustine Mafwele pamoja na kikosi chake wanaendelea kumtafuta na kwamba Faustine Mafwele anataka afe.

Sativa aliendelea kusema kuwa Faustine Mafwele na genge lake wana-unfinished business naye na kuongeza kuwa iwapo lolote litamkuta basi Mafwele anahusika.

Soma Pia: Kwanini Polisi haijibu tuhuma alizotoa Sativa juu ya Faustine Mafwele kuhusika kwenye utekaji wake?

Hapo sasa ni kuamua moja, ufanye mipango ukimbie nchi ama uwaache tu wakuue.

Maana ukiwa nchini hakuna wa kuwazuia.
 
N

Nasikia huyo mafwele ndio aliowakimbiza majambazi Arusha,,panyaroad dar na wale wahuni wa mkuranga na kibiti
Kwa serikali makini ingetambua kwamba huyu ameshakuwa cancer.

Kwa hiyo ni kusema serikali imempa favour ya kufanya chochote anachokitaka hata kuuwa watu kwa sababu tu alifanya kwa weledi alichotakiwa kukifanya,haya mambo utayakuta Africa tu.
 
Ingekua kweli wanamtafuta wangeshampata hana ulinzi huo wa kuwindwa kila siku na asipatikane, kama hadi muda wa kufanya interview anao basi hakuna anaemtafuta
Kwa hiyo unataka wavamie hapo kwenye interview na kuzua taharuki?

Hata kama wana uwezo wa kufanya hivyo na hakuna wa kuwazuia, nao hawapendi kujaza watu, wanaangalia mazingira rafiki.
 
Tumsaidie ndugu yetu Sativa jamani.....

Sativa ana matatizo ya kisaikolojia hwenda kabla ya madhila kumkuta na yamezidi baada ya madhila yale (post traumatic stress disorder).

Awe na amani ameshasikika na kila mtu kwani huyo Mafwele ndiye mwisho wa WAAMUZI WA NCHI HII ?!! 😲😲

Sativa anamkuza sana huyo mtu....

#Nchi Kwanza😍
 
Back
Top Bottom