Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda


Meli kubwa ya Puma huwa ikija Tanzania hitia Nanga mbali sana kutokana na kuwa na kina kifupi ndipo meli ndogo za zinaenda kuchota mafuta kuleta Bandari ya Dar huo ni usumbufu na hasara na gharama pia, Bandari ya Dar sasa ni kichochoro ni kama kale kabandari ka congo ni Aibu miaka 50 kuendelea kuwa n Bandari inayoleta foleni za meli kwenye maji kupisha uchochoro mwembamba
 
Kwahiyo wewe mtu akisema anakuja kujenga nyumba kwenye kiwanja chako na kwakuwa ni kwa pesa zake utakenua tu meno na kusema Sawa kwakuwa utakuwa unafurahia kuangalia lijumba limejengwa kwenye kiwanja chako ambapo huna ruhusa hata ya kuingia na kwenda kukaa humo.?
 
Akili zako zinakueleza kuwa JF ni sehemu ya kujadili Wema Sepetu na Diamond tu, eti? Moja ya kazi zake kama mbunge ni kutoa elimu ya siasa na kuamsha mijadala yenye lengo la kuchochea mabadiliko. Kwa nini likisemwa tu jambo lolote PATHETIC PEOPLE hukimbilia hoja ya uchochezi kwa serikali?

Wewe kama una hoja kinzani juu ya huu mradi, mpinge Zitto hapa na sisi tujifunze kutoka kwako, sio kubadili matumizi ya jukwaa.
 

Bungeni 85% ni wabunge wa CCM na wabunge wa CCM kwa idadi kubwa ni wabunge ndiyo mzee hata kama wanajua kitu ni kibaya kwa Taifa, Bungeni zito alisema na hapa JF ni jukwaa kubwa world wide usipadharau JF humu kila mmoja yupo huru kuchangia kuliko huko Bungeni kwenye udikteta mpaka ndungai mwenyewe kanywea baada ya kupigwa mkwara wa kuporwa kadi ya CCM akaukosa ubunge .
 
Umeandika stori za kusadikika mkuu [emoji23][emoji23][emoji23]Haya mambo waachieni wataalamu nyie endeleeni kushabikia siasa.
 
Mkuu jibu zitto kwa hoja....kama suala ulielewi soma comment za wengine, Zitto is true Wa Kenya sio mchezo kwa dirty game kama kuhujumu uchumi wa Tz
 
Man, kwenye hili la bandari unatakiwa ukajipange upya manake maelezo yako yana mapungufu kadhaa!!!

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba, kupitia China's Belt & Road Initiative, Mchina alijipanga kuwekeza kwenye miundombinu sehemu kadhaa duniani. Hili nalifahamu vizuri kwa sababu nilikuwa mbeba mikoba wa Beberu moja la Kimarekani wakati wa kufanya research, na moja ya case study ni Bandari ya Bagamoyo!!!

Katika kufikia hilo, Mchina akawa ameigawa dunia kwa mafungu... kule Ulaya akawekeza pesa ya kutosha kwenye Bandari ya Piraeus nchini Greece!!!

Kama alivyo beberu langu lile la Kimarekani linavyopinga hii miradi including mradi wa Bagamoyo, Mabeberu ya Ulaya yakaanza kumwekea figisu figisu Mchina kwenye Bandari ya Piraeus! Kuna wakati EU, huku Italy wakiwa ndi viherehere zaidi, wakaanza kusema kwamba China inaitumia Bandari ya Piraues kufanya biashara haramu!!

Cha ajabu, miezi kadhaa baadae, Italy ile ile ikaingia mkataba wa kibiashara na bandari ile ile!! Na bandari ile ile ambayo walikuwa wanaisemanga, leo hii imeingia kwenye Top 10 of largest terminal ports in Europe wakati uendelezaji wala hujafika ukingoni!!

Hilo ni la Ulaya! Mchina huyo huyo akataka kwenda kumchezea sharubu Marekani kwa kutaka container terminal ya South California! Hadi mara ya mwisho nafuatilia, Senate likaanza kutoa povu hawataki Mchina achukue terminal pale South Port!!

Hilo ni la Marekani!!

Tukija Africa sasa, Mchina anafahamu fika kwamba Africa ni emerging market.Strategy yake ikawa kuigawa Afrika kwa blocks! Kwenye Horn of Africa, akawekeza Djibouti ili hatimae mizigo yake itakayoenda ukanda wa Horn of Africa ipitie Djbouti!

Afrika Mashariki tukawa na competition kati ya Kenya na Tanzania huku Kenya akimkaribisha Mchina ajenge Lamu!!! Kenya walitoa incentives kibao lakini Mchina akachomoa na kuchagua Bagamoyo!

Unlike Djibouti na sehemu zingine Africa, Mchina alitaka kuifanya Bagamoyo iwe ndo central unit! I wish ungeiona ile plan, ambayo in the long run, makao makuu ya mkoa wa pwani yangehamishwa kutoka Kibaha to Bagamoyo!!

Ili kuifanya Bagamoyo kuwa Central Unit kwa kufuata mfumo ule ule wa Shenzhen Uchina, ikapangwa kujengwa not just a port but a megaport! Pamoja na hii megaport, pia na industrial complex pamoja na railway network to connect Bagamoyo na nchi zingine za ukanda wa maziwa makuu pamoja na kusini... Malawi, and Zambia in particular!!

Awamu ya 4 ya nne watu wamekula posho na kusafiri hadi Shenzhen kujifunza jinsi Shenzhen ilivyogeuzwa kuwa a fishing village like Bagamoyo!!

So, what was the idea?! Mega ships kutoka China zingekuwa zinafaulisha mzigo Bagamoyo na mzigo huo kuchukuliwa na meli za kawaida na kusambazwa sehemu zingine za Africa, na mali zingine zingetumia reli kwenda landlocked countries.

Pale Industrial Complex kungetokea mambo mawili!! Hivi sasa Uchina labor cost inapanda kila uchao! Kutokana na hilo, kulikuwa na uwezekano mkubwa Mchina akaifanya Bagamoyo Free Economic zone kama sehemu ya kuzalisha baadhi ya bidhaa zake za kulisha Afrika na maeneo mengine!

Kutokea Bagamoyo, bidhaa hizo zingesafirishwa kwa meli na zingine kwa reli kwenda landlocked countries!!!

Sasa unadai kwamba Kenya hatapata mizigo... man, unajidanganya!!! Salama yetu ni Mchina kurudi Bagamoyo vinginevyo, ile plan ya Bagamoyo anaweza kuihamishia Lamu ambako Kenyatta tangia mwanzo alisema msipojenga, tutajenga wewe!!!

Yule Beberu wangu kwavile sawa na mabeberu wenzake wanaipinga hii miradi ya Uchina, Bagamoyo Port included, moja ya hoja yake ilikuwa eti Bagamoyo Port will be too big for Tanzania's Economy, na kwahiyo Bandari ya Dar es salaam inatosha sana!!

Nilipomuuliza ikiwa na umaskini wetu wote huu pamoja na majirani zetu bado wakati mwingine Bandari ya Dar es salaam huwa inaelemewa! What if uchumi wa Tanzania na majirani zake ukipanda angalau kwa mara mbili tu hasa tukizingatia hata ukipanda mara mbili bado tutakuwa maskini!!
 
Hili moja ya Andiko kubwa sana na lenye maana kubwa sana katika nchi yetu. Kila mara ,kila wakati nimekuwa nikivutiwa sana na mawazo mazuri kama haya yenye lengo la kujenga nchi yetu,,,Tatizo kubwa ni kwamba wenzetu upande wa pili wamekuwa si watu wa mijadala,. Ni vizuri hili likawa msingi wa mjadala wetu,,Lugha ya Kipropaganda au lugha za matusi haziwezi kusaidia mjadala wa kujenga taifa.
 
Ukiwasikiliza wengi wa wanaojiita viongozi Tanzania ni wenye ufinyu wa akili na wasioweza kupambanua mambo
matokeo yake ndio kama hayo, wako radhi wanunue ndege au kujenga SGR na kuacha miradi sahihi kwa maslahi ya nchi na wananchi.

mimi nasubili nije nione SGR na ndege zitakavyoleta faida mwisho nchi ina 80pct ya electricity accessibility na ina ziada ya MGWT 300 out of 1500. Investments ya mgwt 2100 ya nini kwa sasa au hata miaka 20 ijayo tutakuwa na consumption ya chini ya mgwt 2500 mpaka hapo hatuna optimal resources allocation.Wachumi na wenye akili kubwa watanielewa logic yangu
 

Mtu akija kujenga mnakaa mnajadiliana mnakubaliana nikiwa na nia nzuri na ya haraka, lakini nikiwa na nia ya kutaka 10% naanzisha vikwazo na pia nikikutana majirani wabaya wasiotaka maendeleo nawasikiliza pia, huo ndiyo mfano uliopo kama magufuli anavyowasiliza kenya huku na yeye akiwa na vyake moyoni
 
Kuna Meli gani kubwa duniani kwa sasa ambayo haziwezi kutia nanga kwenye bandari ya Dar?
Sikiliza hiyo video, kina cha bandari ya Dar Ni kikubwa zaidi na kinao uwezo wa kuhudumia meli ya ukubwa wowote duniani
Unaweza kunipa tofauti kati ya huyu jamaa na akina Mruma waliosema Acacia tunawadai matani kwa matani ya dhahabu yenye thamani ya matrilioni ya pesa kiasi kwamba kwa kutumia takwimu hizo, Tanzania inaifanya kuwa among Top 3 Gold Producers duniani!!!
 
Kwanza nataka kukutahadhalisha kuwa Tanzania ya leo inaupungufu mkubwa wa wajinga.

  1. Mradi wa bandari ya Bagamoyo umewekwa katika hali ambayo sisi tunauza ardhi yetu kwa miaka 99.
  2. Hatuna mamlaka na bandari hiyo kiuendeshaji, kimapato na hatuna nafasi ya kufanya mabadili hata kama yako wazi kwa miaka 33.
  3. Na kama wao wamekekosea katika business plan yao ni sisi tutalipa gharama za mradi ambazo ni bilion 10 USD.
  4. Hatutokuwa na nafasi ya kukagua mapato au kodi zozote kwa miaka 33, tutapokea kadiri watakavyo tangaza wao.
  5. Tutaweka dhamana ya taifa letu kwa mradi huo.10 Billion USD.
  6. Kutakuwa tunalipa interest ya 3% ( 300 million USD) kwa mwaka kama hautoenda inavyotakiwa, au kinyume na matarajio.
  7. Ajira haina kipengele chochote wakati mradi ukijengwa na hata utakapo anza kutoa huduma.
  8. Viwanda vitakavyo jengwa kuusadia biashara ya eneo ( free economic zone) leseni watatoa wao. Hata ikiwa viwanda vya kutengeneza silaha.
  9. Ukubwa wa eneo linalo husika kwa kujenga bandari pamoja na maeneo ya kuweka mizigo na reli na viwanda unalijua ? karibu nusu ya Bagamoyo distric ya leo.

Ingewezekana sana wakati wa zamani. Kuna upungufu mkubwa wa viongozi wajinga na wenye kukosa uzalendo Tanzania ya leo.
 
Kagame aliwahi kumwambie Kikwete yafuatayo:-

" I will Just Wait For You At the Right Place And I will Hit You, "

MWISHO WA KUNUKUU.
CC Magufuli. Kagame amekutumia Rais wetu kumkomoa Kikwete. Maumivu ya kumkomoa Kikwetu ni watanzania wote kwa vizazi na vizazi.
 
Sidhani kama uko vzr kichwani, kwani ulichoandika hakina uhusinao hata kdg na hoja ya mwandishi. Ni vzr ukawa unatulia na kusoma kilichoandikwa badala ya kukurupuka kama kile kitu'.
Nimesoma vizuri sababu alizotoa ZK na pia nimesoma sababu za serikali kusita kusaini mkataba huo kabla ya mambo kadhaa kurekebishwa.[ ambapo tunaelezwa kuwa mazungumzo yanaendelea].
Kuhusu bandari ya Lamu ni kweli imejengwa ila kama mambo yanavyoendelea kenya sidhani kama reli ya SGR kuelekea Uganda itajengwa hivi sasa kwani serikali ya Kenya ina matatizo makubwa ya kifedha kiasi kuwa vigumu kupata mikopo ya kuendelezea miradi mikubwa ya miundo mbinu kama hiyo.
 
Katika mazingira ya kisiasa na kiuchumi tunayoyapitia kwa sasa, nchi yetu inapaswa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa. Hapo ndipo vichwa vyenye uelewa mkubwa wa mambo kama Mh. Zito Kabwe vitaweza kupewa nafasi nyeti serikalini ili kuweza kushiriki ktk kuiletea maendeleo ya uhakika nchi yetu.

Uongozi wa CCM kwa kupewa dhamana ya kuiendesha serikali yetu, kwa sehemu walipofikia naona wanaridhika na mipango ya muda mfupi tu, na tena ile ambayo inawekwa ktk awamu husika. Kila awamu huja na vipaumbele vyake, huku ikitoa dosari na mapungufu luluki kwa ile iliyowekwa na watangulizi na kuitelekeza, ili kujijengea sifa binafsi.

Hii ni nchi yetu sote, chama tawala, washindani wao wa kisiasa na hata wale wasiofungamana na vyama kisiasa. Ni vyema kama taifa tukaainisha "economic potentials" ambazo zitaifaidisha nchi yetu kwa miaka mingi ijayo. Tuangalie ubora wa hoja zitolewazo pasipo kuangalia itikadi za kisiasa. Viongozi wa upinzani mara nyingi huwa na mawazo na mapendekezo mazuri sana, ila kwa upande wa CCM hupuuzia mazuri yote kisa kukwepa kuwapa umaarufu wa kisiasa.

Mh. Zito ameelezea kwa kina juu ya umuhimu wa bandari ya Bagamoyo, huku akijielekeza ktk "grand vision" yake, lkn wachangiaji wengine wanatoka ktk mada yake ya msingi aliyoiweka mezani na kuzichanganua hoja zake, wao wanaleta hoja nyingine, ambazo zipo mbali kabisa na mada yake.
 

Brother umeongea point.

Shenzhen ilikuwa ni pilot project ya Deng Xiaoping katika move yake ya kuibadiri China kutoka uchumi ule uliofeli wa Mao Tse Tung kuwa Uchumi wa kisasa ambao tunauona leo hii wachina wakinufaika nao.

Lazima Tuelewe, Kama Mababeru walivyokuwa wakipinga miradi ya nishati ya umeme ndivyo hivyo hivyo watakavyopinga maendeleo ya bandari, sababu ni mbili, Moja Afrika isijitegemee, pili Kuicontain China

China mwenyewe alipokuwa akitafuta uwekezaji kwa makampuni ya Mabeberu alijishusha kinyama, akakubali hata watu wake walipwe kiduchu ili kusustain investment. Leo hii mchina ana mihela mingi hadi anawakopesha hao mabeberu mapesa.

Just Imagine leo hata nchi ya Israel kwa kuona umuhimu wa investment ya wachina nao wameipa Uchina eneo ijenge bandari kama ambavyo Walitaka kujenga bandari nchini.

Tumepoteza nafasi hii kwa sababu ya EGO, EGO ya Jiwe badala ya kuangalia picha nzima za Tanzania ya miaka 100 ijayo yeye anaangalia Kampeni za uchaguzi za mwaka 2020
 
Kiongozi haya unayapata wapi? Kwani kuna Mkataba wowote uliokuwa signed unaoeleza hayo
 

Ununuzi wa Ndege kwa cash umemshangaza mpaka Rais wa Dunia ndugu Trump kashangaa Nchi masikini kununua kwa cash kumbe hajui kuwa ile cash ina 10% ya wajanja wachache waliochukua chao mapema kwa cash ndiyo maana CAG hathubutu kunusa kwenye ununuzi wa Ndege.
 
Nimekuwa nikipitia mambo mengi anayoandika ZK mengine ninakubaliana naye lakini mengi sikubaliani na mitizamo yake na hasa hii ya kipindi hichi ambacho hayumo kwenye kamati za bunge.
 
Huna lolote wewe tumeshakuzoea na uvuvuzela wako! Awamu hii ya 5 wamekushika penyewe!! Hapa Kazi Tu!

Awamu ya tano imemshika nani? Kama wangekuwa wanakubalika iweje wazuie mikutano ya siasa kinyume cha Sheria na katiba ya vyama vingi? Hapa kazi tu ni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi kwenye chaguzi mbalimbali? au hapa kazi tu ni kula 10% kwenye ununuzi wa Ndege na miradi mikubwa yote na mtu akigoma kutoa 10% mnamkwamisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…