Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

That is it!
Nilichoelewa ni Kwamba Odinga amechangia kukwamisha mradi wa bandari ya Bagamoyo.

Kwamba zile tripu za Odinga Dar na Chato alikuwa anatumwa na nchi yake kumlisha sumu Rais wetu kuhusu mradi wa Bagamoyo.

Kama kweli Odinga alipewa na tuzo kwa kazi hiyo, kama nchi inabidi tujitathimini.

Kifupi Odinga alikuwa jasusi wa kiuchumi kwa nchi yake kwa mjibu wa Zitto.
 
Soma na kuelewa!! Bandari za Djibouti na Eritria ni ndogo, Lamu itapokea meli kubwa na meli ndogo zitakuja hapo kubeba mizigo kupeleka huko kwenye vibandari vyao
Ethiopia imejenga railway to Djibouti mpaka bandarini, hiyo Lamu haina barabara ya kupeleka mzigo Ethiopia, itaanzaje biashara na Ethiopia?

Ethiopia saivi inatumia Djibouti na Eritrea kupitisha mzigo wake wote, Ethiopia haijawahi kupitisha mzigo wake Kenya hata siku moja
 
Mkuu hapo ni kweli kabisa, maana hata sakata la dhahabu iliyokamatwa Mwanza lilianzia Kenya ambako pesa kutoka falme za kiarabu zilipokelewa na Ruto kwa ajili ya dhahabu, dhahabu zilipokamatwa ilibidi Uhuru Kenyatta aje amwambie Jiwe kuwa ni za mabeberu wa kiarabu ndio kasalimu amri kuzirudisha na kuwaachia wale askari nane kwa maelekezo ya mabeberu wa kiarabu na Jiwe akanywea back to the point ccm wajinga sana yaani wamekubali nchi ipandikiziwe uongozi na Bahima empire, matokeo yake ndio haya sasa, Hutu linaiua hii nchi.
'Chief'..., eti unasemaje?
Mbona mambo yanazidi kuingiliana hapa kiasi cha kuleta mkanganyiko?

Kuna mambo mazito hapa nyuma ya pazia!

Hadi leo hii, lile sakata la dhahabu Mwanza, bado sielewi lilivyofunikwafunikwa na watu kulisahau kama halikuwahi kutokea! Lingetokea nchi zenye utawala unaoheshimu sheria, hili jambo lisingekwisha kishamba shamba vile.
 
Soma na kuelewa!!!!! Bandari za Djibouti na Eritria ni ndogo, Lamu itapokea meli kubwa na meli ndogo zitakuja hapo kubeba mizigo kupeleka huko kwenye vibandari vyao
Mkuu, unazo takwimu za uwezo wa bandari hizo (za Eritrea) nasi tuzione; maana haya mambo ya ku'declare' tu kuwa ni "bandari ndogo" hautusaidii chochote katika mada hii.
 
minyoo,
Mkubwa una mantiki kwenye pointi yako. Lakini tunakosea sana ku-underestimate uwezo wa watu wanaofanya maamuzi makubwa ya nchi hii. Huwa hawako sahihi kwa asilimia 100 lakini haina maana kuwa wanafanya hovyo. Kama serikali ingesaini mkataba wa bandari ya Bagamaoyo, tungekuwa nchi ya wajinga sana. Ulikuwa ni mkataba ambao unahatarisha usalama wa nchi yetu kwa miaka 99, na mambo mengine mengi ya ovyo. Infact lilikua ni jambo la kijinga sana.

Kenya wamepigwa bao sana kwenye mradi wa SGR na hiyo bandari ya (labda ni utaratibu wa LAPSET), kimsingi ni kama wamejiuza kwa bei rahisi huku wenyewe wakiwa na thamani kubwa. Angalia cost benefits analysis ya mradi huho utaona kuwa mjenzi ndio ananufaika, na sio anayejengewa.

Kimahesabu serikali yetu imefanya jambo la maana sana maana piga ua bandari yetu itakuwa chaguo rahisi kwa Rwanda Burundi na DRC, hata kama ya Lamu itakuwa kubwa na nzuri kiasi gani. Arguments za Zitto ni za kisiasa tu, ndio maana akiposto huwa harudi kuleta ufafanuzi.
 
Kimahesabu serikali yetu imefanya jambo la maana sana maana piga ua bandari yetu itakuwa chaguo rahisi kwa Rwanda Burundi na DRC, hata kama ya Lamu itakuwa kubwa na nzuri kiasi gani. Arguments za Zitto ni za kisiasa tu, ndio maana akiposto huwa harudi kuleta ufafanuzi.
'Bongolander' nimekusoma kwa makini sana.
Naomba nitumie hoja yako hapa nami nieleze ninavyoona yanayojifunua kuhusu Bandari zetu hizi za Afrika Mashariki - yaani,
Mombasa, Dar es Salaam na sasa Lamu. Na pengine hapo baadae Bagamoyo.
Imani yangu ni kwamba Bagamoyo itajengwa, kama sio chini ya utawala huu wa Magufuli, tawala zitakazofuata lazima Bagamoyo (au mbadala wake), kama kule Mwambani Tanga. Vinginevyo tutakuwa tumekubali kuwaachia Kenya uwanja, wacheze wenyewe wanavyopenda.
Bandari ya Dar es Salaam haina nafasi kabisa katika ushindani huo peke yake.

Ningeweza kuchora ramani hapa ningetumia kukupa picha halisi ya biashara ya bandari itakavyokuwa katika ukanda huu, tokea sasa na kwenda mbele. Lakini ngoja nieleze tu, na unaweza ukatoa ramani kufuatilia ninayoyaeleza.

Bandari ya Lamu (bila ya ushindani) itakuwa mhimu sana. Meli kubwa zenye uwezo wa kupakia makasha zaidi ya 20,000 zitaitumia bandari hiyo, hasa kutoka China na nchi nyingi za maeneo ya huko. Haya mameli makubwa kituo chao kitakuwa Lamu. Makasha yatapakuliwa na kupakiwa kwenye meli ndogo ndogo zitakazosambaza kwenye bandari kama Mombasa, Dar es Slaam, na kwingineko. Hili sote sasa tunalijua vizuri.

Sasa ngoja nikupe habari ya Mombasa, ambayo wengi bado hatujaiwekea maanani, lakini wenzetu Kenya tayari wamelinasa vizuri sana.

Mombasa itakuwa Bandari mhimu sana (kuliko Dar es Salaam mara dufu), katika kusambaza mizigo toka Lamu na kuipeleka Kenya kwenyewe; Uganda, Sudan Kusini, TANZANIA, Burundi, Rwanda, DRC.

Hapa ndipo inapokupasa uchukue ramani ya maeneo ya nchi hizi na kuisoma vizuri. Eneo lote la Kaskazini mwa Tanzania litakuwa eneo la kusambazia mizigo na kupitisha mizigo toka Bandari ya Mombasa. Nazungumzia mikoa hii yote ya Tanzania kuhudumiwa na Mombasa, na sio Dar es Salaam: Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Singida, Shinyanga, Simiyu, Mara, Mwanza, Geita, Kagera... Tazama ramani. Kuna barabara nzuri kabisa ya lami tupu, toka Mombasa, Voi, Taita Taveta, inavuka mpaka pale Holili, inaingia Moshi, Arusha, inateremka chini kuja kuunganisha Singida. Tokea hapo, inapandisha kuelekea Shinyanga na kutokomea zake kwenda Rwanda na Burundi.
Barabara hii ni fupi, kuliko kutoka Dar es Salaam.

Hiyo ni mosi.
Bandari ya Kisumu imefanyiwa ukarabati mkubwa na tayari imekwisha kamilika inasubiri tu kuzinduliwa. Meli kubwa la mizigo, MV Uhuru, nalo limekarabatiwa na tayari linasafiri kwenda Port Bell Uganda.
Ziwa Victoria itakuwa njia nzuri sana ya kusambazia mizigo toka Bandari ya Mombasa hadi mikoa yote ya Tanzania inayolizunguka ziwa - Mara, Mwanza, Simiyu, Geita na Kagera. Mikoa hii nayo ipo karibu na Mombasa kuliko ilivyo karibu na Dar es Salaam.

Sasa lililobaki ni wewe, na wengine kunieleza kwamba sheria haitawaruhusu Mombasa kusambaza mizigo yao Tanzania.
Kama sheria hii ipo, itabidi mnieleze, na kwa maoni yangu ni kwamba, sheria hiyo itakuwa inapingana na kila kitu kinachosimamiwa katika umoja wetu wa EAC. Je, tutaamua kupinga na kujiondoa kwenye umoja huo?

Mfanya biashara yeyote hutafuta njia nafuu ya kufanya biashara yake. Mombasa wamekwishaweka miundombinu bora ya kusambaza mizigo; nasi pia tumewasaidia kwa kuwajengea barabara za kupitisha mizigo yao kwa urahisi, hadi kufikia nchi jirani za Burundi, Rwanda na Congo.

Nadhani nimekwishajieleza vya kutosha. Ngoja niishie hapa nisiwachoshe. Ambayo sikuyasema hapa jazieni wenyewe kuangalia fursa tuliyowapatia Kenya, na hasa kama tutaendelea kuchelewa kuijenga Bagamoyo au Bandari nyingine yoyote mbadala wake.
Dar es Salaam itaendelea kuhudumia mikoa iliyokaribu nayo, na nchi za jirani kama Zambia Malawi, na Kusini mwa Congo.
 
Tulichelewa tulikuwa wajamaa, wenzetu mapebari, we are a bit wiser, we ll catch up soon enough.
Ni aina ipi ya ujamaa inayokataza nchi kuhodhi bandari na viwanja vya ndege vikubwa na hatimae kuwa gateway, not due to geographical position tu bali kutokana na miundombinu!!

Hivi issue hapa ni ujamaa au yale mawazo ninayoyaita ya kiujima?!

4 years ago, nimeongea sana hapa masuala ya gas lakini wale wenye mawazo ya kijima hadi karne ya 21 wanakuambia gas haiozi!! Gas haiozi wakati techlojia inabadilika kwa kasi ya roketi?! Usije ukashangaa hadi watu tunapata akili, tayari wengine wameshagundua jinsi ya kutengeneza "natural gas" commercially kwenye mahabara!
 
Inaamanisha wanatumia peasa za ndani na za nje.

Ila uchumi utakua na hili deni bado ni sustainable ukilinganisha na madeni ya nchi nyingi duniani.

Kama hauwezi kulipa deni wajanja hawakupi mkopo, wanaangalia indicators, trajectory, return on investment, wapi una-invest.
Ndicho wanachotaka raia waamini au wanataka waamini kwamba Serikali ya Magufuli inapiga kazi kweli kweli kiasi kwamba miradi mikubwa inatumia pesa za ndani!

Sijawahi kumsikia Magufuli akiwa majukwaani kuzungumzia kukua kwa deni la taifa lakini ni kawaida sana kumuona akitamba kama sio yeye, hiki na kile kisingekuwepo na vyote hivyo anavifanya kwa pesa za ndani!!!!!
 
@="Chige,

Bandari ya Dsm ni uchochoro kina cha maji ni kifupi na mfumo wake wa utendaji ni wa usumbufu mwingi hakuna mgeni anaipenda Bandari hiyo tena ndiyo maana wengi hutumia Bandari ya msumbiji na Mombasa ambapo hakuna usumbufu mwingi kila kitu kimewekwa vizuri kwa mpangilio bora.
Tena bora hilo la kina kwamba wanaweza kuchimba, lakini watu wanasahau au hawafahamu kwamba, hata ule mlango wa bahari kwa mega ships, nao haitoshi ukiangalia dunia kwa miaka 50 ijayo!

Lingine, ambalo hapa nimeshalisema sana, wazawa wenzangu wa Kurasini watakuwa wanalifahamu vema hili!

Back in 1900's, nyuma ya Malawi/Zam Cargo, kule yalikuwa ni makazi ya watu! Watu wa mwanzoni kabisa kuathirika na Bandari ya Dar es salaam, ni sisi tuliokuwa tunaishia kule.

Miaka michache baadae, wakavuka Bandari ya Mandela na kuingia upande wa pili (kushoto ya Mandela Rd kama unaelekea mjini). Wakati huo lilibomolewa eneo dogo tu... hata Shimo la Udongo hawakufika!!!

Kuanzia 2007 hadi sasa tunapoongea... asilimia kubwa ya Kurasini imebomolewa na kilichobaki ni majengo ya serikali!! Mivinjeni imebaki less than 25%! It's a matter of time kabla haijaingiliwa Keko!

Lakini pamoja na makazi yote hayo kubomolewa, bado Bandari ya Dar es salaam haijafikia uwezo wa ku-handle makasha angalau kama yale yanayokuwa handled na Bandari ya Mombasa!!

Sasa mtu utamsikia "...kwanini isipanuliwe Bandari ya Dar es salaam" bila kuzingatia kadri bandari unavyoipanua na kupokea mzigo mkubwa zaidi, ndivyo unavyotakiwa kupanua eneo la kuweka makontena!

Unfortunately, Dar es salaam imepungukiwa sana na maeneo unless waendelee kuvunja makazi ya watu! Na uvunjwaji wa siku hizi utakua na ugomvi kweli kweli kwa sababu sie ambao tulivunjiwa back in 1990s, tukaambiwa kuna viwanja Yombo!! Leo hii mtu utamwambia aende wapi wakati kila mmoja anataka kuishi Dar es salaam!!
 
Bandari ya Bagamoyo ingeleta faida haraka kuliko Ndege, kwanza mji wa Bagamoyo utakuwa kiuchumi mzunguko wa pesa ungeongezeka na hata ndege za mizigo zingeanza kumiminika kuja kupakia.

Reli wangefanya biashara zipo faida nyingi sana kuliko huko kwenye Ndege ambapo kuna ufisadi mkubwa kwenye service zake na ujanja ujanja mwingi ikiwemo 10% kwenye ununuzi wa cash nk
Yaani ukiangalia ile plan in detail... kama ingefanikiwa kama walivyofanikiwa Wachina kwa Shenzhen ambayo ndiyo ilikuwa model kwa ajili ya Bagamoyo, Tanzania ingekuwa the biggest hub in Africa, let alone East Africa!!

Na ki ukweli, suala la ndege huzi kulinganisha na ule mradi hata kwa 10%. Ndege hamna kitu mle, ni sifa tu kwamba "...tunamiliki ndege!" Bado Tanzania hatuna mazingira ya ufanisi wa airline business!
 
Ingekuwa hiyo mikataba inawekwa wazi basi tungeona la kuchangia tatizo ni gizani
 
Nimesoma andiko la Mh. Zitto kiukweli nilichokisoma kinasikitisha sana kama ni kweli Bandari ya Bagamoyo imehujumiwa kwasababu za kisiasa,

Dhambi za kuhujumu bandari hii itavitafuna vizazi na vizazi.
 
Magufuli na Wasaidizi wake kina kakoko kuuacha huu mradi ni Kuturudisha nyuma sana, this is the biggest project in Tz ,itachangia pakubwa kwenye uchumi wa nchi,kutokana na revenue inyopatikana hapa unaweza jenga au kupanua bandari zingine zikawa saw kisasa zaidi,ni kujidanganya mchana kweupe kuachana na hii project na ukajikita kwenye upanuzi tu wa vibandari vidogo,kina kakoko wana mdanganya Rais na kumpa Matumaini fake ya uwezo wa Bandari ya Dar, tukae na Wawekezaji Tujadili haraka Kuondoa hizi vikwazo hatimaye Bandari ianze kujengwa.
 
Magufuli na Wasaidizi wake kina kakoko kuuacha huu mradi ni Kuturudisha nyuma sana, this is the biggest project in Tz ,itachangia pakubwa kwenye uchumi wa nchi,kutokana na revenue inyopatikana hapa unaweza jenga au kupanua bandari zingine zikawa saw kisasa zaidi,ni kujidanganya mchana kweupe kuachana na hii project na ukajikita kwenye upanuzi tu wa vibandari vidogo,kina kakoko wana mdanganya Rais na kumpa Matumaini fake ya uwezo wa Bandari ya Dar, tukae na Wawekezaji Tujadili haraka Kuondoa hizi vikwazo hatimaye Bandari ianze kujengwa.
inasemekana wapambe wa mtukufu akina Bashite na wenzao wana 10% kwenye ununuzi wa Ndege na ndiyo maana hawataki kumsikia CAG ananusa huko kwenye manunuzi, na mradi wa Bagamoyo wameukwamisha mpaka Wachina na waarabu walete 10% kwanza, pengine tatizo siyo mtukufu magufuli mwenyewe tatizo lipo kwa wapambe zaidi.
 
1572519693834.png


Oil dealers shun Mombasa for Dar
 
Mtukufu Magufuli ameahidiwa vingi na Kenya kwa ajili ya uchaguzi wa 2020 lakini China siyo wajinga wapo kimya wanamhadaa kama wapo pamoja nae lakini moshi wa Ruangwa waliuona na hawapo mbali na ule moshi na pia wanajua kila kitu hata Spika ndungai mpaka leo anaumia moyoni.

Kwa kifupi Bandari ya Bagamoyo ingeleta mapinduzi makubwa kiuchumi na kuipelekea Tanzania kupiga hatua kubwa kimaendeleo, wapinzani wengine wa Bandari ya Bagamoyo ni msumbiji na Bandari ya Darban ambayo pia ina uwezo wa kupokea meli kubwa.

Maendeleo ya kweli yaaanzia kwanza kwa mwananchi mwenyewe: unaweza kua na miradi mikubwa na bado wananchi wakawa maskini wakutupa:: So how do we do it?

[SKILLS]: unaweza ukawa na miradi dunia nzima hakuna lakini kama hauna watu wana uelewa mzuri na huo miradi ni kazi bure: mfano, Tanzania ni monopoly nation kwenye Tanzanite, lakini hatuna watu wanaoweza kuleta faida kutokana na hio tanzanite: why are we even going to the next project? kama tungekua na plants za kutumia Tanzanite in a productive way , that itself would have taken us a step ahead: tatizo watu wanadhan kua na miradi mingi ndo wananchi watakua matajiri, serikali yenyewe inategemea kodi ijiendeshe( fedha zenyewe hazitoki serikalini) , wewe unategemea vp serikali ambayo yenyewe ina sehem inategemea: at the end of the day, tutakua tunaimba tu Tanzania ni nchi inaokua kwa kasi ilihali watu wake wana matatizo kibao: tunahitaji miradi michache tu ambayo tutaiwekea mkazo kwa manufaa ya taifa,'

kuna nchi nyingi tu hazipo upande wa bahari na zimeendelea kutuliko sisi:
 
Kama unadhani just by geography, Tanzania tayari inastahili kuwa gateway to East and Central Africa; kwanini basi ni Jomo Kenyatta International Airport ndiyo inatambulika kama "gateway" na sio Julius Nyerere International Airport?!
Kwa bahati mbaya sana na wewe umetekwa akili na propaganda za waKenya kuhusu JKIA kuwa gateway. Kwa nini sifa hiyo isiiendee Bole Airport ya Ethiopia?
Hilo ni swali.
Lakini epuka kulishwa na kumeza kila kitu unachosikia kutoka kwa hao jamaa. Sifa yao kubwa ni majigambo na kujipa sifa wasizostahili kuwa nazo.
 
The article sums it all up the future direction battle of the neighbouring ports and their respective countries in terms of future strategic planning. Whatever they do either in infrastructure projects or policies objectives; consumer needs and expectations from point of entry must come first.

From the article the bottom line is that price sensitivity remain an issue and efficiency (speed to clear goods) is far more important tha the time factors of moving good from one nation to the other under the current business environment.

Ndio maana wengine tunaona bandari ajenge mchina au nchi zenyewe and regardless of their sizes most important factor remains meeting the needs of those services users which are; cost, speed, access options from point A to B, security, less red tape; etc with their needs.

Mambo ya sijui meli kubwa na ndogo kwa sasa is not in their mind kwa ivyo wacha mchina aende na mziki wake na nchi ziende na zao, kujenga port tu kisa kubwa kwa mkataba wa ovyo ni kukosa busara.

But then mkataba wa ovyo ukoje wanaojua hayo ni wataalamu wa serikarini thus far; personal from how they have handled business policies (korosho comes to mind) and advice given to the president I would not pay such called experts even to write a simple corner shop business plan they just don’t have it, let alone leave them scrutinise a complicated long terms port contract which demands all manner of business discipline at once.

Ningemuona Zitto wa maana akipigania hawa wataalamu watoe aspect za hiyo mikataba ijadiliwe bungeni kuliko watu wachache kujifungia, kuamua na kuliingiza taifa zima mkenge.
 
Mambo ya sijui meli kubwa na ndogo kwa sasa is not in their mind wacha mchina aende na mziki wake na nchi ziende na zao, kujenga port tu kisa kubwa kwa mkataba wa ovyo ni kukosa busara.
Ukifikiri kwa undani kuhusu andiko lako lote utagundua kwamba unaliua kwa mistari hii miwili uliyoweka hapa.
"...mkataba wa ovyo..." hili hatulijui.
 
Back
Top Bottom